Hii dunia imenajisiwa sana, mengi tumepotoshwa na ni zaidi ya tuijuavyo

toplemon

JF-Expert Member
Mar 26, 2017
4,581
4,631
Ukitafakari sana dunia yetu utagundua dunia imekwishanajisiwa na baadhi ya watu kwa makusudi.

Historia ya dunia imepindishwa

Ukweli umegeuzwa uwongo

Uwongo umegeuzwa ukweli

Propaganda ndo zinarun dunia

Mambo mengi yanapromotiwa yana maangamizi

Mambo yamekua vise versa unaambiwa nenda hivi ndo kuna njia kumbe huko sio

Historia ya dunia imepotoshwa,mengi yamepotoshwa,ukweli na haki vimefichwa kuna mengi,

Wenye haki wamezimwa michango yao duniani imezikwa na wanaonekana wao ndo walifanya sio

Dunia ni siri tu mambo mengi sio kama tuyaonavyo vingi vimefichwa, ukiwaza sana utaumia na full stress

Dunia imefungwa mdomo na ukweli wa kihistoria umefichwa kwa faida za wachache wanufaike wakati wao sio waliostahili

Sayansi imefichwa na tunadanganywa

Siasa zimegeuzwa juu chini

Uchumi wa dunia ni siri kuna watu wapo behind ya kila kitu cha dunia hii.

Afya na magonjwa ndo usiseme huku ndo dunia imepigwa upofu kibayolojia na kimind set zetu inauma mno.

Vyakula na vinywaji hapa ndo dunia inauliwa kikatili mambo mengi ni kinyume na mfumo, biashara za nyuma ya ajenda kali dhidi ya wanadam na vita ya chakula na dawa ni vita vya dunia nzima kuna vita kubwa sana mengi yamefichwa mfumo ndani ya mfumo.

Africa ilikwisha uawa na kuzikwa na wenye nia zao dunia imenajisiwa inauma sana.

Africa yenyewe ndo yale yale ukihoji uhuru wa nchi nyingi siri ipo kwa waasisi hayo mafile ya kupewa uhuru mkionyeshwa mtakua na kifua?yaani mtu akupe uhuru aache madhahabu na diamond na kila utajiri akupe tu uhuru akuachie ulaji?hvi mnadhani hakuna makubaliano ya siri wanaoyajua waasisi pekee na wakoloni? Ukiondoa bendera kuna nini chengine?

Africa yenyewe mambo mengine yamefichwa na tunaendelea kufichwa na watawala wetu mambo mengi yanayotokea na kuhabarishwa sio kweli kama tuambiavyo.

Viongozi wazalendo wanakufa tu wanauliwa na maajent wa ndani ya nchi au nchi za magharibi kwa kupandikizwa magonjwa tu na hizi teknolojia lakini hatutoyajua watu wetu wanamalizwa tu tunaangalia hatuoni hii dunia haina haki mengine yanafanywa ili kuprove wrong misimamo yao Africa Africa

Viongozi wakiwa na misimamo wakikataa mambo wataitwa wabaya madikteta na majina yote mabaya na sifa zote mbaya lengo ni kuwaprove wrong tu hii dunia hii

Kuna wakati naamini duniani hakuna haki wala ukweli mbinguni ndo haki na ukweli wote wa dunia ulipo vitu vingi sio kama vinavyoonekana wapendwa.
 
Lete ukweli sasa unaoujua tafiti hupingwa kwa tafiti, ndiyo maana hata mahakamani huagiza ushahidi {kidhibiti} sasa wewe unasema uongo kwa kitu tunachokiona wewe tuonyeshe cha chako cha ukweli!
 
Mimi nilipogundua kwamba hata ramani ya dunia iliyopo kwenye vitabu, atlas nk sio ya kweli ndio nilichoka kabisa..
mimi siku hizi nipo tuu naangalia wanaoambiwa kuna sehemu nzuri inajengwa tutakuwa huko nachokaga akili nikija ya ramani ya dunia north kuwa south na south kuwa north nilisha achaga enzi hizo kufikiria

Nikikuta Kijana ana chapa maneno kumkingia kifua mlaji nacheka sana

Hapo sijamuacha yule kijana wa kila Jumapili au ijumaa na kutosahau jumapili anakimbia Juu juu kashikilia vitabu huku hajui hata maana ya upendo huku tukiaminishwa sadaka ya kanisani ndio inakupeleka sehemu nzuri lakini kumsaidia mwenzio unaona moyo mzito nacheka sana

Nikija kwenye mfumo wa elimu ila hapa naweza sema mfumo wa elimu kwa chini yaa kama shule za msingi na form four sidhani kama una msaidia mtoto asiekuwa na interest ya kusoma ukiona una mwanao na hawezi perform vizuri darasani mlete kwenye maisha halisia yaani hela ya kumsomeshea mfungulie biashara aanze maisha halisi aache ndoto

Maana maisha haya watu wenye elimu siku hizi vichwa vinawauma hasa wale waliotegemea elimu tuu ila walio kuwa na mikakati zamani hizo wana pangua matofali tuu

Kiufupi maisha yaishi tuu usijue mengi yatakutesa maana utatamani ubadili vitu usivyoviweza na mwishoe akili zikakuruka,maana ukishajua ukweli hata asilimia 0.09 kila kitu duniani utakuona hakipo sawa na hapo lazima uonekane una tatizo kuwa makini

Being wise sometimes it's a curse and self torturing you'll want to change everything that comes your way!
 
Mungu wa dunia hii ni shetani ndiyo maana mambo yako hivyo. Ukitenda haki unaangamizwa mara moja maana hapa si kwako. Wabaya ndio wanaostawi. Inasikitisha hata wale wanaokwenda kanisani kusali ni kujionyesha tu.

Huku nyumba wanatenda ubaya sana. Wametuibia kura zetu tukiwaangalia hivi hivi kwa sababu wanajiona wako juu ya sheria. Siku ya hukumu yaja kila mtu atachukua mzigo wake mwenyewe.

Wewe unayedhania ni wa Mungu endelea kutenda haki na waovu waendelee kutenda maovu.
 
Back
Top Bottom