Hii dhana ya kusema tulitoka mavumbini na mavumbini tutarudi huwa siyo ya kweli

Ikitotanzila

JF-Expert Member
Sep 22, 2020
1,409
2,263
Huwa nashangaa sna watu kusema tulitoka mavumbini. Hivi ni kweli tulitoka mavumbini au tulitoka kwenye matumbo ya mama zetu kwa kutumia reproductive organ zao?

Au tumbo kwa lugha nyingine ni vumbi! Mi huwa nakuwa confused kabisa.

Labda huu msemo ubadilishe uwe 'tulitoka tumboni mwa mama zetu na tunaelekea mavumbini' hapo ndo imekaa sawa. Au mnasemaje waungwana.
 
Tatizo umesimama bondeni huwezi kuona mbali; unaona hatua nne kutoka miguuni pako. :) Originally & naturally mwanadamu ni mavumbi, our first Ancestors -- Adamu na Hawa kipenzi chake -- walifinyangwa na Maulana kwa kutumia mavumbi.
 
Sasa huo msemo bado ni valid mpaka sasa au imebaki ni story tu!
 
Mwanzo 3:19 kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.

NO COMPROMISE
Yaani utaishi Kwa kupambana ili ule, hata hvyo mwisho wake utakufa , na ukifa utarudi kwenye udongo( kaburini) hakuna atakayekupeleka angani .... Na kwenye ardhi utaoza na mwili utageuka kuwa mavunbi....
 
Jamaa ana hoja msimbeze. Of course vitabu vyote vya dini vinasema tumetoka mavumbini na mavumbini tutarudi lakini ukiuangalia mwili wako na huu udongo (mavumbi) unaoukanyaga vinafanana? Adam na Hawa kweli tunafundishwa walifinyangwa kwa udongo, je umewahi kujiuliza ni huu huu udongo tunaoujua au mwingine? Adam na Hawa tunaambiwa walikuwa ndio binadamu wa kwanza na walizaa watoto wawili Kaini na Habili. Kaini alimuua ndugu yake na akakimbilia nchi (sehemu) nyingine na akaoa, Je alimuoa nani wakati dunia ilikuwa na watu wanne tu yaani Adamu na Hawa na hawa watoto wao wawili? Kwa hiyo inabidi tutumie akili kufikiria badala ya kuitikia ndio mzee. Huenda hayo mavumbi aliyoumbiwa Adam yana maana tofauti na haya mavumbi tuyajuayo kama inavyoonekana dhahiri kuwa Kaini alienda kuoa mwanamke nchi nyingine wakati tunaambiwa dunia ilikuwa na watu wanne tu.
 
Kwa muujibu wa vitabu vya dini...

Ila ukifuata uhalisia ni kweli tumetoka viunoni mwa baba zetu na kuishi kwenye matumbo ya mama zetu mpaka kuzaliwa...
 
Sisi sote na vingine vyote vikiwemo Sayari Miezi na Jua tumetokana na vumbi la Nyota iliyolipuka (Supernova) miongo mingi iliyopita sisi tumetokana na Star Dust
 
Planetary scientist and stardust expert Dr Ashley King explains. 'It is totally 100% true: nearly all the elements in the human body were made in a star and many have come through several supernovas. '
 
Huwa nashangaa sna watu kusema tulitoka mavumbini. Hivi ni kweli tulitoka mavumbini au tulitoka kwenye matumbo ya mama zetu kwa kutumia reproductive organ zao?

Au tumbo kwa lugha nyingine ni vumbi! Mi huwa nakuwa confused kabisa.

Labda huu msemo ubadilishe uwe 'tulitoka tumboni mwa mama zetu na tunaelekea mavumbini' hapo ndo imekaa sawa. Au mnasemaje waungwana.
Angalia,...vyote unavyokula vimetoka kwenye udongo,... hata kama ni nyama ya ng'ombe, ng'ombe huyo amekula majani yaliyoota ardhini (mavumbini). Hata hewa ya oxygen tunayopumua imetokana na mimea iliyoota ardhini (mavumbini) kwa njia ya photosynethesis. Mimi ni mwanabiologia najua wazi kwamba miili yetu imetoka ardhini na itarudi huko na sehemu kubwa ilisharudi ardhini kupitia apoptosis (cell death) ambapo kila siku mwanadamu hupoteza kadiri ya cell 10,000,000,000,000.
 
Back
Top Bottom