Hii desturi ya wasafisha mitaro Temeke, wahusika hawaioni

AMMARITO

JF-Expert Member
Dec 5, 2015
989
1,000
Mara baada ya zoezi la ,kuondo wamachinga kukamilika ikaja kampeni ya kusafisha mitaro, ambayo ni kitu kizuri sana.
Kitu cha kushangaza sijawahi kuona yale marundo ya uchafu yanayowekwa pembeni kuondolewa na waliopewa ile kazi.

Kuyaacha pale pale ya marundo kunaletea vitu viwili

1.Mchanga na uchafu kurudi mule mule mtaroni, hivyo mitaro kuziba tena, hivyo mkandarasi analipwa tena kwa kazi aliyokwisha kuifany.
2.Marundo yakibaki juu, yanapunguza nafasi ya barabara hivyo kuletea msongamano na ajali barabarani.

Nachojiuliza hivi wanaowapa kazi hawakagui kazi inapokamilika, au ndio wote wapo ktk mgao.
View attachment 2025910
 

aise

JF-Expert Member
May 16, 2018
2,872
2,000
Mitaro hii hii ya barabarani au mitaro kama mitaro
Kuna tofauti kubwa kati ya
"kusafisha mitaro"
na
"kufukua mitara".

Kwa mujibu wa mtoa mada anazungumzia kusafisha mitaro ya barabarani.

Ila angesema "kufukua mitaro" hiyo ingekuwa kesi nyingine.
 

JAYJAY

JF-Expert Member
Oct 31, 2008
4,911
2,000
Mitaro hii hii ya barabarani au mitaro kama mitaro
Kiswahili siku hizi kimekuwa na utata sana. Mimi mwenyewe niliposoma title tu ikanichanganya. Mitaro ipi tena!?

Kondakta anamuuliza jamaa "unaenda!?" Jamaa anamjibu "acha lugha zako tata hizo"
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom