Hii chapati niliyotengeneza, usipokua makini utajing'ata Vidole

Mtu akiolewa na mwanaume anejua kupika ndio anakuwa makini balaa, na anafit sana jikoni kwani anajua akifanya vitu ovyo mumewe anaelewa. Sasa mtu alieolewa na mume asiejua kitu Chakula kiunguzwe, kipikwe ovyo kisiwive vizuri ye anaona sawa tu, tena anaogoa hata kusema ukweli anaogopa asije akaambiwa apike yeye kama anaweza. Lakini anaejua haoni tabu kukosoa anajua hata akiambiwa pika mwenyewe anaweza
Umewaza kiutu uzima. Wewe una akili sana mkuu.
 
Hahaha mkuu figganigga ulivyoanza kujisifia kumbe ni chapati za maji aiseee...

Sasa pancake ama chapati za kumimina itakuaje si utataka uanzishiwe jukwaa lako kabisa hahaha


Anyway, naona chapati yako iko poa tu jitahidi kupunguza mafuta na usipike na moto mwingi.


Kwa chapati za kusukuma tafuta thread yangu humu nilifundishwa na my wife Evelyn Salt.

Halafu Jolie Jolie umeongea kama kweli vileee [HASHTAG]#thinking[/HASHTAG]
Asante mkuu. Ile ya kusukuma sina tatizo. Sababu nanyunyuzia mafuta kidogo na kijiko huku naigeuza hadi inaiva. Tatizo na kuitengeneza iwe ya duara. Chapati nikisukuma umbo lake ukaona picha. Unaweza cheka hadi mbavu ziume.

Nanunua zile za dukani mi napasha moto tu.

Wewe kwa mapishi upo Vizuri. Ila kwa sasa hutanitisha chochote sababu hadi urudi, utakuta nshakua mtaalam sababu nimepata wadhamini wa mapishi. Mzigua90 ndani ya nyumba. Nataka nikufunike.

Nikishajua kuoa ntafikiria, nikiulizwa naoa lini ntakua najibu bado nipo nipo kwanza.
 
Chapati zote lazima niweke sukari kiduchu na chumvi kiduchu yaan kama hakuna sukari sijui nazionaje walai.
Mi hapana sukari kweny chapati naweza rudisha chenchi,yupo shoga ye mpaka za kusukuma anatia sukari,na za maji hatii chumv ni sukari tu uwiii
Sukari imenishinda kwenye chapati ya maji.
Naonaga inanoga ukiblend yai unga na chumvi. Ukishapata rojo ndo ukate kate kitunguu hoho na carrot unaikwangua.
 
Back
Top Bottom