Hii chapati niliyotengeneza, usipokua makini utajing'ata Vidole

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,483
54,853
Heshima kwenu wakuu,

Nmegundua kumbe kutengeneza chapati simple sana. Nimetengeneza chapati sikutegemea kama zitakua tamu hivi. Yaani ni tamu balaa.. Nikimpikia mgeni itabidi nimwambie awe makini asijing'ate kidole au ulimi.

Ila bado kuna tatizo, kama mlivyo nifundisha kutengeneza chips, Nimejaribu kukaanga Chips sijafanikiwa sana, msaada jamani

Naomba niongezewe utaalam wa chapati. Nataka nikija kuoa mke wangu asipate tabu pale anapoumwa au kusafiri. Chapati ninazotengeneza hazitazamiki halafu mafuta yanadondoka kama asali.

Je, nyie mwatengenezaje na mwatia viungo gani?
FB_IMG_1521300299226.jpg
 
Hizo ni chapati za maji?
Nakushauri ingia youtube utakutana na mwanamama Aroma kila aina ya pishi utalikuta kwake, ni vema kuangalia na kufanya kuliko kusoma.

Me pia mapishi mengi nimejifunzia youtube.

Turudi kwa topic yetu, chapati za maji, weka yai/mayai, vitunguu maji, karoti na hoho au kimoja wapo katika hivyo ili kuleta ladha na kukata ile harufu ya yai.

Mchanganyiko wako usiwe mzito sana wala mwepesi sana, size ya kati. hapo utatoa kitu mwake mwake, mafuta weka kiasi sio kama unakomoa, unapakaza tu juu ya chapati sio unamwagia.
 
Kumbe tuko wengi tunaomfatilia aroma,yani huyo dada ndo mwalim mkuu wangu wa mapishi
 
Heshima kwenu wakuu,

Nmegundua kumbe kutengeneza chapati simple sana. Nimetengeneza chapati sikutegemea kama zitakua tamu hivi. Yaani ni tamu balaa.. Nikimpikia mgeni itabidi nimwambie awe makini asijing'ate kidole au ulimi.

Ila bado kuna tatizo, kama mlivyo nifundisha kutengeneza chips, Nimejaribu kukaanga Chips sijafanikiwa sana, msaada jamani

Naomba niongezewe utaalam wa chapati. Nataka nikija kuoa mke wangu asipate tabu pale anapoumwa au kusafiri. Chapati ninazotengeneza hazitazamiki halafu mafuta yanadondoka kama asali.

Je, nyie mwatengenezaje na mwatia viungo gani? View attachment 717776
Ulikua unajaribu kupika chapati maji?

Cc: mahondaw
 
Mwanaume anajua mpaka kuunga mchuzi wa nazi anawahi kuoa kutafuta nn

Unakuta kwake kuna kibao cha chapati,cha kukunia nazi na kinu hahaha hao hawaoagi
Ukimkuta mwanaume anajua yote hayo lakini hataki kuoa ujue hana mpango wa kupata watoto. Nayajua yote hayo lakini faida yake kwangu ni kuwa hata mke akiumwa naingia jikoni mwenyewe then hawezi kunigomea kwenye kupika, hawezi kunilaza njaa
 
Mtu ukiolewa na mwanaume anaejua kupika ni kazi sana,utapika mchuzi wako vzur atakosoa mpaka ujione mdogo,pika andazi lako atalitoa kasoro hadi ujiogope,mara vitunguu hujakaanga vizuri,mara nyanya hazikuiva,mara mafuta umetia mengi,mara andazi halijaumuka yan tabu
 
Mtu akiolewa na mwanaume anejua kupika ndio anakuwa makini balaa, na anafit sana jikoni kwani anajua akifanya vitu ovyo mumewe anaelewa. Sasa mtu alieolewa na mume asiejua kitu Chakula kiunguzwe, kipikwe ovyo kisiwive vizuri ye anaona sawa tu, tena anaogoa hata kusema ukweli anaogopa asije akaambiwa apike yeye kama anaweza. Lakini anaejua haoni tabu kukosoa anajua hata akiambiwa pika mwenyewe anaweza
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom