Zurie
JF-Expert Member
- Jul 6, 2014
- 2,002
- 5,534
Leo mida ya saa Tano asubuhi nimepita maeneo ya Millenium Towers. Katikati ya jengo la Millenium Towers na petrol station ya Oilcom kuna Parking ya magari nzuri tu iliyojengwa vizuri na kuwekewa uzio ikiwa na mlinzi wa magari hayo.
Kilichonishangaza ni kuwa, ndani ya parking ile kulikuwa na gari moja tu huku upande wa pili wa barabara nikishuhudia magari mengi yakiwa yameegeshwa kiholela pembeni ya barabara yakiwa karibu kabisa na mfereji wa kupitishia maji.
Mpaka sasa najiuliza, Je tatizo ni kuwa wenye magari hawapendelei kupaki magari yao sehemu salama (kuna ulinzi), au ni gharama za huduma hiyo kuwa juu sana au kuna tatizo lingine?