Hii Barua mpelekee Dada/kaka, uifiche vizuri mtu asiione...

Lovebird

JF-Expert Member
Sep 27, 2012
5,723
7,559
Nakumbuka nikiwa mdogo (darasa 3-4) nilikuwa nikipewa barua nimpelekee Dada/kaka, mdau alikuwa akiniambia ifiche vizuri mtu asiione...mwenzenu nilikuwa mtiii napeleka na sijuu nini kimeandikwa mle....baada ya kukua (darasa la 5-7) ndo nkajua dada/kaka walikuwa wakiwasiliana na viburudisho vyao wakiombana ku-siginanaaaaa

Msimu ule wadau walikuwa wakijitahidi kuandika vizuri na kuremba mwandikoo...waliopitia haya maisha hadi leo wana miandiko mizuri kuliko kizazi cha doti com

kipindi hicho kiliendana na viatu vya skuna/gogo gogo/ukipasi nguo unaweka alama ya nyota kwenye shati/ suruali za bwanga etc

Old is gold
 
Unanikumbusha machungu, nilishawahi kula za uso kutoka kwa kakaye mwafulani baada ya kunasa barua yangu kabla ya kumfikia mlengwa..
Sintakuja kumsahau BARADHULI yule......
 
Unanikumbusha machungu, nilishawahi kula za uso kutoka kwa kakaye mwafulani baada ya kunasa barua yangu kabla ya kumfikia mlengwa..
Sintakuja kumsahau BARADHULI yule......

ha ha ha pole sana mwenyewe ukairemba na makopakopa
 
Unanikumbusha machungu, nilishawahi kula za uso kutoka kwa kakaye mwafulani baada ya kunasa barua yangu kabla ya kumfikia mlengwa..
Sintakuja kumsahau BARADHULI yule......
hahahahahaha na wewe ulikua hauko makini lol.
 
halafu ilikuwa unasigina tuu hakuna kukojoa!!!barua inakua na kaua ka LOVE rangi hakuna unapka hiyo hiyo ya penseli.unavizia akitumwa dukani kununua mafuta ya taa na ni kulala chini kwenye kahawa giza likisha ingia
 
Nakumbuka nilipewa barua nipeleka pahala na nikaambiwa ukimkuta umpe mkononi . Sasa nilipofika muhusika sikumkuta si ikabidi barua niirudishe na kuiweka juu ya meza mwenyewe nikaenda kucheza rede ili baadae niipeleke pengine muhusika atakua kaudi. Loh huko nyuma barua ikabambwa na wazazi alinilaumuje muhusika maana alidhani sikwenda. Siisahau siku hiyo nilitiwa masingi na nilikosakosa kichapo.
 
amu@Mtambuzi ulishawahi kuweka hii
 
Attachments

  • love.jpg
    love.jpg
    2.8 KB · Views: 400
Last edited by a moderator:
Hakika mkuu umenikumbusha mbali sana, niliwahi kumuandkia njiwa wangu alikuwa akisoma weruweru bahati mbaya sana alikuwa kwenye hatua za kunikataa. Aliponijibu majibu yangu headmaster akafungua na kuisoma na kwa sababu alikuwa akinichukia sana akaja nayo paredi na kuisoma mbele ya wanafunzi wenzangu! Hakika nilishushuliwa sana kwani majibu yenyewe hayakuwa positive, baadaye nikapokea kichapo na kurudishwa nyumbani nikamlete mzazi aelezwe mambo ninayofanya shuleni! Mzee alikuwa mjeshi baada ya kuja alianianza kwa boot na kuishia na makofi; kamwe sitasahau siku hito katika maisha yangu.:A S kiss::nod:
 
AISII, Msichana umekosa, njukuti umechapwa, mabuti umekula na Shuleni aibu!!!! Pole sana.

Mimi kuna mtu alikuwa anapenda sana kunibebesha barua, ila bana barua moja ili ikamilike inamchukua kama
masaa 10 (si utani)..........ataandika atachana, ataandika atachana mpaka apate hati safii.
 
Unanikumbusha machungu, nilishawahi kula za uso kutoka kwa kakaye mwafulani baada ya kunasa barua yangu kabla ya kumfikia mlengwa..
Sintakuja kumsahau BARADHULI yule......
Ndiyo maana naamini ule msemo wa wahenga, "ukiona nyani mzee ujue amekwepa mishale mingi" Pole sana Kaka.
 
ahahahahhh na mishale ya kumwaga katikati ya kopa lol! chezea enzi za mwalimu weye........kweli yakale ni dhahabu
ha ha ha pole sana mwenyewe ukairemba na makopakopa
 
Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom