Hii bajeti ni nzuri kuisikia lakini haitekelezeki hata kwa asilimia 50%

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
3,086
4,881
Hebu jiulize kila mwaka bajeti ikisomwa watu wengi wanaisifia lakini ukifika muda wa utekelezaji vijisababu vingi sana mara Covid 19 mara vita vya urussi na ukraine kitakachotekelezwa katika bajeti ni kodi tu na vitu vichache kama elimu bure lakini suala la serikali kubana matumizi kwa safari na matumizi ya magari ni gumu sana labda ingepunguza magari yake ya kifahari kwa viongozi wake kwa kuwauzia.

Pia misafara ya viongozi imekuwa mikubwa sana nayo ni tatizo katika kubana matumizi.

Mishahara kwa viongozi walioenguliwa kuendelea kulipwa kabla ya kuenguliwa huo nao ni wizi mkubwa.

Kuwalipa mishahara na posho Wabunge 19 wasio na sifa ya kuwa wabunge kwa mujibu wa katiba huko nako ni matumizi makubwa ya fedha za serikali.
 
Inawezekana km maajabu yatatokea.

According to Mwigulu, makusanyo yote ya kodi na yasio ya kikodi kwa mwaka jana yalikua T21. Bajeti itakua 41T...hapo inahitajika miujiza kufidia hilo gape la 20T...makusanyo yaongezeke kwa 100% otherwise itatekelezeka kwa 50% tu.

50% tutajipa moyo mipango sio matumizi...
 
Kuna mazingira ambayo yamewekwa Ili bajeti iweze kutimilizika. Kama ukifuatilia kwa asilimia kubwa wamepunguza ushuru wa forodha kwa ajili ya malighafi kadha wa kadha Ili kustimulate uchumi.

Kuna Kodi kama Kodi ya mapato kwa Kila lorry na basi na kufanywa flat rate ya 3.5mil kwa mwaka. Hiii itaenda kuongeza mapato kwa kiwango kikubwa kwani hapa hakutakuwa unakwepaji maana zamani ilikuwa inacheza na faida ambayo Mwenye lorry au angepata halafu ndo atoe asilimia 30 kama kodi, wengi walikuwa wanaweza foji mapato halisi ila sasa hivi itamlazimu kwa Mwenye basi au lorrry kulipa hicho kiwango

Mfano kidogo
Tuchukulie tuna mabasi na malori 300000 kwa nchi nzima
Itakuwa 300k*3.5mil=1.05tril sawaa na USD 1.05tr/2320=452,586,206.897
Hiki ni kiwango kikubwa sana kwa vyombo vya usafiri tu

Kwangu hii bajeti imekaa vizuri wakikomaa inaweza kutuboost sana
 
Kuna wachumi/wachambuzi wa maswala ya uchumi huu ndio muda wao wa kutamba wakihama kutoka chombo moja cha habari kwenda kingine kutoa pongezi.

Mwaka Hadi mwaka ukimuona tu hutegemei jipya. Na pengine ni dokta akitoka hapo anarudi kuwapa vizazi vijavyo maarifa yatakayotuondoa kwenye dimbwi tulipo.
 
Hii awamu ya tozo itatufikisha 2025 tukiwa tumechoka na kuchakaa kweli kweli! Na kwenye huo uchaguzi mkuu wakubali tu kukabidhi nchi kwa kutumia njia ya amani.

Maana hatutawachagua kwa kweli. Lakini pia hatutaendelea kuvumilia ule uhuni wao wa kumtangaza mtu aliyeshindwa, chini ya ulinzi mkali wa policcm wenye silaha za moto na magari yenye maji ya kuwasha
 
Kuna mazingira ambayo yamewekwa Ili bajeti iweze kutimilizika. Kama ukifuatilia kwa asilimia kubwa wamepunguza ushuru wa forodha kwa ajili ya malighafi kadha wa kadha Ili kustimulate uchumi...
Do u know how long it took us kufikisha mapato ya 21T....unadhani in a year tutaweza ku double hayo mapato ili kufikisha io 41T?
 
Do u know how long it took us kufikisha mapato ya 21T....unadhani in a year tutaweza ku double hayo mapato ili kufikisha io 41T?
Tumefikia tr21 tukiwa hii, uchumi ukiwa umedorora, sekta utalii ikiwa imekufa kabisa, mahoteli yakiwa yamefungwa , Kila kitu kikiwa shaghala baghala ila kwa dizain aliyokuja nayo at least tunaweza nyanyuka
 
Inawezekana km maajabu yatatokea.

According to Mwigulu, makusanyo yote ya kodi na yasio ya kikodi kwa mwaka jana yalikua T21. Bajeti itakua 41T...hapo inahitajika miujiza kufidia hilo gape la 20T...makusanyo yaongezeke kwa 100% otherwise itatekelezeka kwa 50% tu.

50% tutajipa moyo mipango sio matumizi...
Mnajadili vitu msivyokua na elimu navyo..tangu Uhuru bajeti ya Tanzania/tanganyika mbali na mapato ya ndani,hutegemea mikopo,wahisani na misaada..pamekua na juhudi za kuziba deficit hiyo kwa vizazi,mkiwekewa tozo mnalia,Kodi mnakwepa
 
Back
Top Bottom