Tulimumu
JF-Expert Member
- Mar 11, 2013
- 14,409
- 13,260
Ukifuatilia habari za matukio ya ajali iliyotokea Arusha na kuua wanafunzi 32, walimu 2 na dereva 1 ni kama vile waliokufa ni wanafunzi tu. Yaani walimu na dereva wanazungumzwa kwa kiasi kidogo sana.
Watoa rambi rambi, waimbaji, magazeti, redio, televisheni, mitandao ya kijamii na mijadala mbali mbali yaani habari ni wanafunzi tu lakini hao marehemu wengine yaani walimu na dereva kiukweli ni kama wamesahaulika kana kwamba wao hawajafa.
Mimi naona hii sio sawa kwakuwa nao wana ndugu ambao wanapata uchungu kama ndugu wa hao wanafunzi.
Samahani jamani lakini haya ndiyo ninayoyaona wakati huu tukiendelea na maombolezo.
Naombeni tuwaomboleze wote kwa pamoja bila kubagua jamani hata kama waliokufa wengi ni wanafunzi!