RUSTEM PASHA
JF-Expert Member
- Jan 26, 2016
- 4,332
- 10,539
Wakuu,
Hii imekaaje kuwa ukimtumia mtu pesa wakati anaitoa, serikali itakuwa inachukua kodi ya 10%?.
Nikimtumia mtu sh laki tano,serikali inakata kodi ya elfu hamsini, hivi kuna ukweli wowote hapo?
Wakuu nisaidieni.
Hii imekaaje kuwa ukimtumia mtu pesa wakati anaitoa, serikali itakuwa inachukua kodi ya 10%?.
Nikimtumia mtu sh laki tano,serikali inakata kodi ya elfu hamsini, hivi kuna ukweli wowote hapo?
Wakuu nisaidieni.
juzi juzi hapa mitandao ya simu imepandisha huduma ya miamala hizo mnazoweka nyiyi kama mifano ni siku nyingi sana makampuni ya simu yamesha achana nazo, kwa maana hiyo hii kodi ni sawa na wewe unapokwenda kununua kitu mlimani city kuna 18% ya VAT.
Sasa na huku utakapofanya muamala kuna hiyo 10% itakayokatwa ukituma au kutoa pesa gharama ya muamala utakaotuma ndiyo itakayokatwa hiyo 10%. hivyo basi makampuni yatakuwa na option kama tatu hivi.
1 yataongeza gharama ya miamala kutoka kiwango yanachotoza sasa hivi.
2 yatapunguza gawio kwa mawakala wake ili kubana hicho kiwango yanacholipa yaendelee kupata faida kupitia huduma hizi.
3 yataacha hali ilivyo iendelee japo wigo wa faida utapungua kidogo kupitia miamala hii.
tusubiri tuone PRACTICE NOTICE ZA TRA ZITAFAFANUA VIPI HILI SUALA.
Kuna kipindi pia hili suala liliibuliwa bungeni kama mnakumbukumbu kwenye bajeti ya Mgimwa (RIP) lenyewe lilikuwa kwenye kodi ya SIMCARD,kuilipia kila mwezi sikumbuki kiwango kilikuwa ni kiasi gani lakini lilileta mjadala mzito sana bungeni kamati ya bunge chini ya Chenge ilipinga hili suala pamoja na kambi ya Upinzani Bungeni, na wananchi nao tulipaza sauti Mungu akasaidia Dr Mgimwa akasitisha kodi ile sasa imeletwa tena na bwana Mpango zamu hii kwa Mlango wa Nyuma lengo nikuhakikisha kila alipo masikini ananyonywa hadi anaishiwa hata kidogo alichonancho.
MAKOFI KWA SERIKALI YA WANYONGE CHINI YA MTUKUFU SANA MPIGA-NIA WANYONGE.