Hifadhini hii Kauli ipo siku huko usoni Mtakuja ihitajia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hifadhini hii Kauli ipo siku huko usoni Mtakuja ihitajia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Babylon, Jun 5, 2010.

 1. Babylon

  Babylon JF-Expert Member

  #1
  Jun 5, 2010
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 1,338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  CCM haiwezi kuanguka katika uchaguzi mkuu
  Saturday, 05 June 2010 08:58 0diggsdigg

  Festo Polea

  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Pius Msekwa amesema chama hicho hakiwezi kushindwa katika uchaguzi mkuu ujao kwa kuwa ni sawa na mto Rufiji ambao hauwezi kukauka.

  Alifafanua mto Rufiji, hauwezi kukauka kutokana na mtu au watu wachache kuchota maji yake kwa lengo la kuukausha.

  Msekwa alitoa kauli hiyo, kutokana na kuwepo taarifa za baadhi ya wabunge wachache wanaotishia kukihama chama hicho baada ya bunge kuvunjwa.

  Msekwa alisema hayo jana akijibu swali aliloulizwa na waandishi wa habari katika mkutano wake na waandishi uliofanyika ofisi ndogo za chama hicho kwa lengo la kutangaza rasmi tarehe ya kuchukua fomu kwa wanachama wa chama hicho wanaotaka kugombea kuteuliwa katika nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Zanzibar na kwamba shughuli hiyo, inatarajiwa kufanyika Juni 21 hadi Julai 1 mwaka huu.

  Msekwa alisema chama hicho, hakihofii vitisho hivyo na mbunge yeyote mwenye nia ya kukikimbia chama hicho baada ya bunge kuvunjwa hawezi kusababisha madhara yoyote kwa sababu CCM ina wanachama wa kutosha kukipa ushindi katika chaguzi ujao.

  “Chama chetu hakitetereki, kama kuna hayo mliyouliza ya kukimbiwa na viongozi wetu, hii ni kwa sababu mwaka 2005 waliondoka watu muhimu kama Njelu Kasaka, lakini hatukutetereka na alirudi kundini na chama kinaendelea kama kawaida,’’ alifafanua Msekwa.

  Alisema watu wengi maarufu waliondoka katika chama hicho akiwemo aliyekuwa Naibu Waziri Mkuu, Agustino Mrema na kujipatia maarufu na wanachama wengi, lakini chama hicho hakikuyumba.

  Akizungumzia kuhusu wagombea wa nafasi hiyo, Msekwa aliwataka kuwa na busara ya kujichunguza wenyewe kama wanakubalika ndipo waende kuchukua fomu za kugombea kuteuliwa nafasi hizo.

  Alisema gharama za fomu hizo ni Sh 1milioni kwa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano na kwamba zitatolewa na kurudishwa kwa katibu mkuu wa chama hicho makao makuu ya chama yaliyopo Dodoma na wale watakaochukua fomu kwa ajili ya nafasi ya Rais kwa Zanzibar wanatakiwa kuchukua na kuzirejesha fomu hizo kwa Naibu Katibu Mkuu, ofisi ya chama hicho zilizopo Kisiwa Ndui Zanzibar.

  Alisema baada ya kukamilika kwa kurejeshwa fomu hizo kuanzia Julai 2 hadi 8, mwaka huu, wagombea wa nafasi hiyo, wataanza kazi ya kutafuta wadhamini na upande wa muungano anatakiwa kuwa na wadhamini katika mikoa isiyopungua 10 na miwili kati ya hiyo inatakiwa iwe kutoka Unguja na mwingine Pemba.

  Msekwa alisema kwa mgombea wa Zanzibar atatakiwa kuwa na wadhamini katika mikoa isiyopungua mitatu, angalau mkoa mmoja kutoka Pemba, lakini hakuna kizuizi kwa wagombea hao, Bara na Visiwani katika kutafuta wagombea katika mikoa yote 26 ya Tanzania.

  Msekwa alisema shughuli hiyo ya kuteua jina la kukiwakilisha chama hicho kwa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itafanyika Julai 10 katika mkutano mkuu wa chama hicho na kwa upande wa Rais wa Zanzibar itatangazwa Julai 9, mwaka huu na Halmashauri Kuu yaTaifa.

  Alisema watakaogombea udiwani katika kata mpya zaidi ya 700 watachukua fomu kwa makatibu wakuu wa kata za zamani.
   
 2. Shagihilu

  Shagihilu Member

  #2
  Jun 5, 2010
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 61
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Babylon kwa uchaguzi mkuu ujao hili halina ubishi.
   
 3. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #3
  Jun 5, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Msekwa ananikumbusha kisa kimoja cha mwanasiasa, kada wa chama cha mapinduzi, shushushu na mkereketwa kiongozi wa maskani kaka ya CCM ya Mwembekisonge akiitwa, Borafia. Aliwahi kuitisha mkutano wa hadhara maeneo ya hapo hapo viwanja vya Michenzani-Kisonge, wakati akisubiri watu wajae mkutanoni kumsikiliza, alijikuta mpaka jua linakuchwa akiwa na wapiga matarumbeta tu, hakukuwa na mwenye haja ya kusikiliza matusi yake.

  Kuona hivyo alisimama jukwaani akanadi (kama alivyosema Msekwa), "...CCM haina shida ya kuwa na watu weengi kwenye mikutano...hata kupiga kura, kwa taarifa yenu...kura yangu mimi Borafia na Amani Karume, zinatosha kuitangazia ushindi CCM..."
  Unaweza kuona ni kauli ya mzaha, kumbe kilichokuja tokezea ni kweli...alimaanisha kuwa ni vyombo vya dola tu CCM inavitegemea kubaki madarakani na si kura ya mtu yoyote.
  Kwa kauli ya Msekwa wala tusishangae ni kweli tusije kusahau maneno yake.
   
 4. Spear

  Spear JF-Expert Member

  #4
  Jun 5, 2010
  Joined: Jun 21, 2008
  Messages: 510
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ni Borafia huyo huyo Ndie aliyewahi kutamka siku za nyuma kuwa Hata Mmungu hawezi kujenga Nchi kwa siku mia seuze CUF sitoisahau kauli yake hiyo ,Laana za Mmungu na adhabu zake zimshukie akiwa bado yupo hapa duniani na huko tuwendako ,na mfano mwengine ni ule wakati kambarage alipowambia watu kuwa uchaguzi ujao atauona tu lakini alisahau kuwa mwenye kutowa fursa ya kumfanya yeye auone alikuwa tayari amesha mtaarishia siku zake za kubaki hapa Duniani Mwisho (Usilo lijuwa Elewa ni sawa na usiku wa giza) na kama anajuwa kuwa watashinda sasa kinachowafanya kutapa tapa na hao wanaowaita wanaotaka kujimeguwa kutoka CCM nikipi ?
   
 5. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #5
  Jun 5, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Kama kweli CCM haina wasiwasi wa kushindwa/inapendwa na wananchi wengi,kwanini iwe na budget ya billion 50 kwa sababu ya uchaguzi? Kwa kigezo chochote kile,hizi ni hela nyingi sana kwa nchi ambayo wananchi wake kwa mamilioni hawana uhakika wa kupata mlo mmoja kwa siku!!!
   
 6. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #6
  Jun 5, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Bulesi,

  Hizi pesa CCM wanazokusanya si kwa uchaguzi mwaka huu, bali ni kujenga himaya yao na kuimarisha mizizi yake.
   
 7. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #7
  Jun 5, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  hapo umeongea
   
Loading...