Kiboko ya Jiwe
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 12,698
- 36,099
Habarini wakuu!
Leo ngoja niandike kitu ambacho huenda kitaamsha ari ya viongozi wetu.
Binafsi mimi ni mwenyeji wa mkoa wa Ruvuma(Myao) ila nimekulia na kuzaliwa Liwale (Lindi).
Ulinzi wa hifadhi ile hasa kipindi cha masika ulikuwa duni. Hii ilisababishwa na poor infrastructure (barabara). Hivyo wakazi wa vijiji vya Mlembwe, Barikiwa, Ndapata, Mpengere, Mkundi n.k walikuwa wakiingia bila hofu na kuwinda wanyama au kuvua Samaki.
Sema tu ufahamu wa wananchi juu ya utajiri wa madini ulikuwa duni , nakumbuka mwaka 2004 Mzee mmoja aliokota mawe ya thamani 3 kwenye kijito kidogo. Baadaye akayatupa 2 na kubakiwa na moja.
Aliporudi nalo kijijini ili ampe mtoto wake achezee mtu mmoja akamwambia kuwa ile ni Mali.
Wakaenda kuliuza Mtwara kwa walanguzi wakapata hela ya kujenga nyumba na kubadili mboga.
Wakarudi porini 2015 ili wakayaokote mengine wakajaza mfuko wa Rambo wakayaleta Dar , wakatapeliwa.
Imagine waliyaokota tu juu juu.
Mzee alipobembelezwa awapeleke mabrother wanaoijua pesa alikataa akikumbuka machungu ya matapeli wa Dar.
Jamaa wakaenda kwa kubahatisha mmoja aliokota jiwe ambalo aliliuza Tunduru zaidi ya milioni 100.
Sijajua siku hizi kukoje maana nilishahama huko kusini miaka zaidi ya kumi imepita.
Hizi fedha za kizamani za Wajerumani huko ukifika kwenye zile kota za Wajerumani za zamani huko porini utaziokota mpaka uchoke.
Ma skaveta yao baada ya kupigwa kwenye First World War wameyachimbia kwenye mahandaki huko.
Huenda na Dhahabu wamezichimbia huko pia.
Serikali kupitia shirika la madini ikachunguze deeply utajiri uliojichimbia ardhini huko.
Mjerumani anaipenda Selous kuliko sehemu yoyote ile duniani.