Hifadhi ya Rubondo yageuka kitega uchumi kwa askari game

Von Bismarck

JF-Expert Member
Jul 11, 2018
3,073
6,251
Kwanza nianze kwa kuwapongeza askari wa hifadhi za wanyamapoli walio waadilifu, kwa kuendelea kusimamia kulinda urithi wa maliasili tulizo nazo ikiwemo hifadhi ya Taifa ya rubondo.

Kwa wasio ifahamu rubondo ni kisiwa kinachopatikana ndani ya ziwa Victoria. wilayani chato, Mkoani Geita.

Naweza kusema kwa ushahindi ni moja ya hifadhi ambayo imepoteza watanzania wengi sana kuanzia maeneo ya kasenda, muganza, kibehe, nyamilembe, Nkome na maeneo mengine ndani ya mwambao wa ziwa hasa mkoa wa geita.

Vija wengi wameuwa kwa mateso ya kupigwa risasi, kuangikwa kwenye miti, kufungwa mawe na kuzamishwa ziwani na hao wanaojiita askari gemu.

Familia nyingi zimewapoteza Baba zao, kaka zao , waume zao ( maeneo hayo niliyoyataja yanaongoza kwa wanawake waliopoteza waume zao)..kweli Magufuli Mungu anakuona huko uliko

Kwa kipindi hiki hali ipo hivi.

Unapokamatwa ndani ya ziwa maeneo ya rubondo hasa wavuvi unapewa mateso makali kama kuvunjwa miguu na badae wanaakupiga faini ya 500,000 -600,000 au zaidi ili uachiwe na mateso umepata.

Hali yaa ukaamataji imekuwa ni kero kipindi hichi cha mwezi wa December
Wavuvi wanafatwa uraini (nje kabisa ya mipaka ya hifadhi) wanachukuliwa kama majangili.

nimeshuhudia leo magemu wakiwakata watu waliokuwa wanaendelea na uvuvi nje ya mipaka ya hifadhi, majira ya asubhi nikiwa eneo la mwembeni- kasenda.

Rai yangu kwa mkuu wa hifadhi Rubondo.

Ukamataji wa majangili uzingatie taratibu naa sheria zinazohusika.

Waliokamatwa leo maeneo ya kasenda hao watu wachiwe, askari wako wamekuwa kero kuwavutia wavuvi ndani ya eneo ya hifadhi wakati wa doria
 
Mvuvi na akili zako unaenda kuvua samaki Lubondo kweli....sehemu ambako hata babu yako anapaogopa, unajilipua kisa kuna mazalia ya samaki unaenda kupiga full mtumbwi matokeo na wewe unapigwa full mtumbwi!

Ukitaka kuwa mhalifu/haramia tumia akili....wekeza pesa au teknolojia! Gemu nao wana njaa kama watanzaia wa kawaida na wanahongwa kirahisi tu, weka pesa upate pesa...bure bure utatenguliwa nyonga na hutakula tena tunda kimasikhara!
 
Hakuna mtu anaroho ngumu kama mvuvi.
Utamkamata leo kesho anarudi ile inzi kufia kwenye kidonda

Ila ukamataji wa aina hii sio sawa kabisa. Nje ya mipaka ya hifadhi mkuu.
 
Ni kwel kabisa kuna jamaa aliwah kuniambia kuwa kuna wenzake wamewahi kuuwawa kwenye hifadhi ya lubondo ila yey na mwenzake mwingine walipona baada ya kuzamia kwenye maji na kuibukia kwenye hifadh wakajificha game walivyoondoka nao wakaondoka kwa kutumia mitumbw ya wavuv wengine ambao walipotelea msitun
 
Hawa game wanaroho ngumu sana
 
Back
Top Bottom