Hifadhi ya Pori Selous imepata ufadhili wa Sh bilioni 47.124 kutoka Ujerumani

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,498
54,923
Hifadhi ya Pori la Akiba la Selous imepata ufadhili wa Sh bilioni 47.124 kutoka Ujerumani kwa ajili ya mradi wa miaka mitano wa Maendeleo ya Uhifadhi wa Ikolojia ya Pori la hifadhi hiyo (SECAD).

Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe kwa kushirikiana na Balozi wa Ujerumani hapa nchini, Egon Konchanke alizindua mradi huo ambao umefadhiliwa na Serikali ya Ujerumani kwa ushirikiano na Serikali ya Tanzania, mradi huo utatekelezwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania, WWF (World Wildlife Fund) na FZS (Frankfurt Zoological Society).

Akizungumza katika hafla iliyofanyika jana, Matembwe Selous Mkoani Morogoro, Maghembe amesema Serikali ya Ujerumani kupitia benki ya KFW ilichangia Euro milioni 18 (sawa na Sh bilioni 45.124) katika mradi huo wa miaka mitano huku mashirika ya WWF (World Wildlife Fund) na FZS (Frankfurt Zoological Society) kwa pamoja zikachangia Euro 400,000 (sawa na Sh bilioni 2).

Profesa Maghembe almesema,Mradi huu ni muhimu kwa kuwa utasaidia kuongeza nguvu kwenye jitihada za kuendeleza na kuimarisha hifadhi ya pori hili la Selous ikiwemo upatikanaji wa vitendea kazi pamoja na kutuongezea nguvu kwenye mapambano dhidi ya ujangili.

Alisema jitihada ambazo Serikali imeshazifanya katika pori hilo ni pamoja na kuimarisha doria za ndege zenye rubani na zisizo na rubani (drones), kutoa mafunzo ya jeshi usu kwa askari, kuongeza maaskari pamoja na vitendea kazi ambapo katika mwaka ujao wa fedha Serikali pia itatoa magari mengine 15 kusaidia pori hilo.

Akizungumzia changamoto ya ujangili katika pori hilo, alisema Serikali imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupambana na tatizo hilo ambapo majangili wengi wameshakamatwa katika maeneo ya Tunduru, Namtumbo na maeneo ya katikati ya Selous

Chanzo: Radio5
 
Afadhali watazisimamia wenyewe wazungu, maana wala rambi rambi wangefanya diversion ya ajabu ili tembo waendelee kupotezwa na yule mtu wao!!
 
sidhani kama hizo pesa zinatoka kiburebure, baadae mtakuja kutajana wanyama wakianza kuchukuliwa....... tutarudi kulekule kwenye mikataba feki
 
Frederick_Courteney_Selous_portrait.jpgFrederick Courteney Selous DSO (31 December 1851 – 4 January 1917) was a British explorer, officer, hunter, and conservationist, famous for his exploits in Southeast Africa. His real-life adventures inspired Sir H. Rider Haggard to create the fictional Allan Quatermain character. Selous was also a friend of Theodore Roosevelt, Cecil Rhodes and Frederick Russell Burnham. He was pre-eminent within a select group of big game hunters that included Abel Chapman and Arthur Henry Neumann. He was the older brother of ornithologist and writer Edmund Selous.

On 4 January 1917, Selous was fighting a bush war on the banks of the Rufiji River against German colonial Schutztruppen, outnumbered five-to-one. That morning, he was creeping forward in combat during a minor engagement when he raised his head and binoculars to locate the enemy. He was shot in the head by a German sniper and was killed instantly.

Upon getting the news, American president Theodore Roosevelt (his close friend) wrote:

He led a singularly adventurous and fascinating life, with just the right alternations between the wilderness and civilization. He helped spread the borders of his people's land. He added much to the sum of human knowledge and interest. He closed his life exactly as such a life ought to be closed, by dying in battle for his country while rendering her valiant and effective service. Who could wish a better life or a better death, or desire to leave a more honourable heritage to his family and his nation?

He was buried under a tamarind tree near the place of his death, in today's Selous Game Reserve, Tanzania, in a modest, flat stone grave with a simple bronze plaque reading: "CAPTAIN F.C. SELOUS D.S.O., 25TH ROYAL FUSILIERS, KILLED IN ACTION 4.1.17." Exactly a year later, on 4 January 1918, his son, Captain Frederick Hatherley Bruce MC, was killed. He was a pilot with Royal Flying Corps, in a flight over Menin Road, Belgium.
 
Am just thinking how much more billions of USD will be harvested from that project back to Germany. Neo colonialism
 
Halafu baadae wanaanza, Oooooh tunaibiwa wanyama! as if pesa ya mwanaume inaliwa bure!
 
Back
Top Bottom