Hidden History: Baada ya Musa kukimbia Misri, aliishi kwanza Afrika akawa Mfalme kwa miaka 40.

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,510
28,416
Yoshua 10:13
Ndipo jua likasimama, na mwezi ukatulia, Hata hilo taifa lilipokuwa limekwisha jipatiliza juu ya adui zao.Hayo je hayakuandikwa katika kitabu cha Yashari?

2Samweli 1:17-18
Basi Daudi akamuombolezea Sauli na Mwanaye maombolezo haya, Kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Yashari.


Kulingana na Kitabu cha Yashari ambacho Biblia imekitaja kama moja ya Reference zake kuna Historia ambayo inafichwa sana na mara nyingi kwa makusudi haitakiwi ifahamike.

Historia inasema katika siku hizo utawala wa Ethiopia hapa Afrika ulikuwa umeimarika sana ukitawala sehemu kubwa sana ya Uarabuni.
Miaka iivyozidi kwenda ndipo katika utawala wa Mfalme Kikianus aliyekuwa Mwafrika, Waarabu waliasi na kutaka kuanza kujitawala wenyewe.
Mfalme Kikianus kuona hivyo akajipanga yeye na jeshi lake kwenda kuzima uasi ule na akapigana kwa siku nyingi mpaka akawatandika waarabu na kuzima uasi.

Baada ya kuwashinda akachukua mateka mengi sana ya watu na nyara za mifugo na mali za kila namna , pia akasimika utawala wake upya tena na kurudisha mfumo wa tozo ya kodi ya kila mwaka kutoka kwa waarabu kuja Ethiopia.
Hatimaye Waarabu wakarudishwa tena chini ya mkono wa Muethiopia.

Wakati Mfalme Kikianus anaondoka Ethiopia kwenda vitani, alimuachia Balaamu mwana wa Beori(yule anayefahamika kwenye Biblia) atawale kipindi yeye yuko vitani, mana vita zilikuwa zinapiganwa hata miaka minne mfuluizo na hakukua na mifumo ya mawasiliano kama zama hizi.

Kwa bahati mbaya sana Balaamu huyu alikuwa mtu wa akili nyingi sana na laghai kweli kweli lakini pia alikuwa mshirikina wa kiwango kilichotukuka.

Mara baada ya kuyaonja madaraka ya Kifalme na kuyaona matamu, akaandaa mpango wa kuyang'ang'ania, asiyaachie wala kuyarudisha hata kama mfame Kikianus atarudi na ushindi.

Ikumbukwe kwamba huyu Balaamu ndiye aliyekuwa mshauri wa mambo ya kiganga wa Farao mfalme wa Misri kipindi Musa amekwenda kudai uhuru wa watu wake, na ndiye aiyeongoza kikosi cha waganga wa kienyeji kum-challenge Musa pindi Musa na Haruni walipoleta ishara ya kutengeneza nyoka mbele ya Farao kwa kutumia fimbo ya Haruni.
Balaamu naye kwa ufundi wake akabwaga fimbo yake na za waganga wake, nazo zikawa nyoka mbele ya Farao, mpaka pae fimbo ya Haruni ilipozimeza fimbo zao.

Mfalme Kikianus aliporudi kutoka vitani baada ya miaka mingi alikuta mji umefungwa makomeo(ilikuwa ni ile miji ya ngome iliyokuwa imezungukwa na kuta pande zote), na hivyo kushindwa kuingia ndani.

Tayari Balaamu alikuwa amejitangazia Ufalme na watu walikuwa washamkubali kwa sababu ya akili zake nyingi na uganga wingi wake.

Balaamu aliongeza urefu wa ukuta wa ngome na kuhakikisha kuwa kila lango linafungwa(kulikuwa na malango manne ya kuingia mjini) akihakikisha kuwa anajenga mfereji mkubwa sana wa maji ambao mtu hawezi kupita katika mageti matatu ya mji, halafu geti la nne kwa kutumia ufundi wake wa kiganga akaweka bustani ya ukuta ya nyoka hatari sana wengi kuzunguka geti ambapo hapakuwa na mtu mwenye uwezo wa kuwasogelea, kila aliyesogea aliuawa.

Jitihada za kupambana kuingia ndani ya ukuta zilishindikana ndipo ikabidi itumie mbinu ya vita inayoitwa "kuuzingira mji", mbinu hii ni mbinu ya ku-block njia zote za kuingilia ndani ya mji kwa vikosi vya kijeshi, kwa hiyo mtakufa kwa njaa na itabidi mtoke tu njaa ikiwalemea.

Mfalme alikaa nje ya mji wake kwa miaka 9 mfululizo, huku askari waliotoka vitani wakishindwa kuwaona wake zao wala watoto wao wala ndugu, hili lilileta uchungu kweli kweli.

Ni wakati huo huo ambao jamaa walikuwa wako nje ya ukuta kwa miaka 9 ndipo Musa naye kule Misri alikuwa ameshaharibu mambo kwa kumuua Mmisiri mmoja na siri yake ilivyobumbuluka akakimbia, akimuogopa Farao.

Musa alipofika Ethiopia alikuta jamaa wako nje hawana la kufanya, akajiunga na jeshi la Mfalme Kikianus, maana lipokuwa Misri alipokea mafunzo ya kijeshi na elimu ya utawala kama mmoja wa wana wa mfalme wa Misri, alikulia Ikulu ya Farao kama kijana wa Binti Mfalme.

Musa kwa haiba alikuwa ni mtu mpole, mwenye maguvu kweli kweli, msomi wa mambo ya Utawala,aliyekuwa anapendwa sana na watu, mwenye hekima nyingi, mbabe wa kivita na kutokana na hekima nyingi aliyokuwa nayo Mfalme alimfanya awe mshauri wake.

Miwshoni mwa miaka 9 tangu warudi toka vitani, Mfalme Kikianus alifariki kwa ugonjwa uliokuwa unamsumbua kwa miezi miwili mfululizo.
Ethiopia ikakosa Mfalme.

Mara baada ya mazishi kuisha, kukazuka taharuki kubwa sana kwa vikosi vya Ethiopia, kwa kuwa kule Uarabuni ambako walitoka kupigana miaka ya nyuma taarifa zilikuwa zishaanza kuwafikia kuwa mbabe wa kivita Mfalme Kikianus wa Ethiopia amefariki dunia na kuna mgawanyiko ndani ya Dola ya Ethiopia.

Kwa hiyo Waarabu kwa kutumia mwanya huo wakajiandaa kuja kulipiza kisasi kipigo walichokula miaka ya nyuma kabla Mfalme wa Ethiopia hajafa.

Hapo ndipo ikabidi atafutwe kwa lazima mtu mwenye uwezo wa Kivita, anayejua mambo ya utawala, mwenye hekima na ambaye kila mtu atamkubali, maana tayari kulikuwa kumeshaanza kuwa na mgawanyiko.

Hapo ndipo Musa akaonekana ni mtu pekee ambaye anaweza kuchukua nafasi ile.

Musa alianza kutawala Ethiopia nje ya Ukuta akiwa na miaka 27 tu.
Na akakutana na jaribio la kwanza kama mfalme la kutafuta mbinu ya kuingia mjini, kitu ambacho kilikuwa kimemshinda mtawala wa kwanza kwa miaka 9 mfululizo.

Mara baada ya siku 7 Waethiopia walikusanyika wakimtaka alete mpango mkakati wa namna ya kuingia ndani ya ukuta wa mji wao, maana askari walikuwa wamechoka kukaa nje ya mji.

Ndipo hapo Musa akaja na mpango makini sana kwa kutumia mamlaka ya Kifalme aliyokuwa nayo.
Akatangaza kuwa kila askari aingie msituni na apande kwenye miti akatafute makinda ya ndege maarufu sana kwa wakati huo anayeitwa ndege mwarabu
Ndege huyu huwa ana mistari myeupe na myeusi na mdomo mrefu, na ni adui mkubwa sana wa nyoka.

Askari wakawa na jukumu moja tu la kila mtu kuamka asubuhi na kutafuta makinda ya ndege mwarabu na kuyafuga mpaka yakuwe kuwa ndege mkubwa.
Zoezi lilifanyika na kila askari akawa na ndege wake.

Baada ya makinda kukua na kufikia umri wa kutosha, akaagiza ndege hao wanyimwe chakula kwa siku tatu mfululizo mchana na usiku, tayari kwa maandalizi ya vita.

Siku ya tatu kila askari akabeba ndege wake na kuelekea kwenye lile lango lililokuwa limerundikwa nyoka wa Balaamu na kumuachilia ndege wake.

Ndege waliondoka mikononi mwao na kwa sababu ya njaa kali breki ya kwanza ilikuwa ni kudonoa macho ya nyoka, ikumbukwe kuwa ndege hawa wana uadui mkubwa sana na nyoka na hupenda sana kuwadonoa nyoka machoni wanapokutana nao na kuwala kama kitoweo.

Kizuizi cha nyoka kikawa kimeondoka na askari wakapata wasaa wa kupanda ukuta na kuingia ndani kwa ajii ya mapambano ya kuutwa mji.

Mapambano yalindelea na askari kama laki moja wa uasi wakauawa na Musa akawa ameshinda na kuurudisha mji chini ya himaya yake.

Mara baada ya Balaamu kuona utawala umenyang'anywa mikononi mwake , akatoroka na kukimbilia Misri kwa Farao, akapewa hifadhi ya kisiasa huko.
Na kwa kuwa Misri ilipenda sana ushirikina wakati huo na Balaamu aikuwa fundi sana wa anga hizo, akapewa wadhifa wa Mshauri wa Mfalme kwenye mambo ya ulimwengu wa roho, akimshauri Farao kwa miaka mingi mpaka pale walipokuja tena kukutana uso kwa uso na Musa aliporudi kuwakomboa watu wake.

Huku nyuma, Musa akapewa Ufalme rasmi na kukabidhiwa mke maana ilikuwa ni sheria kuwa mfalme lazima awe na mke, kwa hiyo akapewa mke wa Kiethiopia aliyekuwa anaitwa Adoniah ambaye alikuwa malkia, mke wa mfalme aliyefariki nje ya ukuta.

Musa kwa sababu za viapo vya kiyahudi alivyokuwa anavifahamu alikataa kata kata kumchukua mke yule, wayahudi walikuwa wanaoana wao kwa wao, hii waliitoa kwa Ibrahimu babu yao.
Lakini sheria zilimbana sana Musa, ikabidi akubali kuwa naye,lakini alikuwa ni mke jina, hakuwahi kuwa na mahusiano naye ya kindoa, kama ilivyo desturi ya wanandoa.

Musa mara baada ya kuingia madarakani alianza kuibadili Ethiopia taratibu ili ikae kwa kufuata dini ya Kiyahudi ambayo ilikuwa inaamini katika Mungu Yehova mmoja na taratibu Ethiopia ikajikuta imeshikilia dini ya Kiyahudi tofauti na dini zao za awali za kuwabudu kila mtu Mungu wake.

Mara baada ya Waarabu kupata taarifa kuwa mbabe waliyekuwa wanamuogopa amefariki na mfalme mpya ameingia, walitangaza uasi tena, na mara hii hawakutaka kusubiri Waethiopia wawafuate kuzima uasi kama mwanzo, waliwafuata huko huko kwao.

Waarabu wakiongozwa na Aram ambayo ndiyo Syria ya leo walikusanya kikosi kikubwa sana cha wapiganaji, huku Musa na Waethiopia wakichagua kikosi cha mashujaa tu wapatao elfu 30, kikiongozwa na Musa mwenyewe.

Ilipigwa ambush ya hatari na askari wa kiarabu wapatao laki tatu walifariki katika vita ile, kitu kilichiwafanya wakimbie uwanja wa mapigano na kurudi kwa aibu kwao.

Huku nyuma Musa akajipanga na kikosi chake wakawafukuzia mpaka katika nchi ya Aram au Syria, na akatembeza kichapo tena na huko na Syria nayo ikarudishwa chini ya mkono wa Muethiopia kama koloni lake na kuanza kutozwa kodi ya mwaka kwa mwaka kama ilivyokuwa kawaida ya makoloni ya wakati huo.

Mara baada ya vita zile, utawala wa Ethiopia uliimarika sana na kuwa na mafanikio makubwa sana ya kiuchumi na kisiasa.

Ikumbukwe pia wakati wa Dola za Kiethiopia na Kimisri zilizokuwa Afrika, pia kulikuwa na Dola iliyokuwa inafahamika kama "Dola ya Afrika" ambayo wakati huo ilikuwa chini ya mfalme Angeas.
Angeas huyu naye alikuwa mbabe sana wa kivita akitawala Afrika ya wakati huo na kumiliki mpaka maeneo ya Chittim au marufu kama visiwa vya Cyprus kwa dunia ya leo huku akihamisha utawaa wake mpaka kuhamia Dinhabah ambayo ndio nchi ya Jordan ya leo.

Mara baada ya miaka ya unabii wa Israel kukaa Misri kutimia yaani miaka 400 ambayo Mungu alimueleza Ibrahimu kuwa uzao wake utakaa utumwani, kuna watu kama elfu 30 mashujaa wa Kiisrael wakaamua kwa utashi wao wenyewe kuvaa silaha za kivita kujikomboa.

Kikosi hiki cha mashujaa kikavuka usiku usiku Misri na kuingia mpaka nchi ya Wafilisti kibabe maeneo ya Gathi, maeneo ambayo yalikuwa maarufu kwa ufugaji wa kondoo wakati ule, wakiwa na silaha wakitaka kuvuka kienyeji enyeji.

Wenyeji wa Ufilisti kuona vile wakatafsiri kama ni uvamizi wa kivita kutaka kuwapokonya mifugo yao wakajipanga kijeshi na vita ikapiganwa.

Katika pambano la kwanza Israeli wale walishinda lakini vikapangwa vita tena mara ya pili Israel wakapigwa vibaya wakapigwa sana na Wafilisti, na wengi wa askari wao wakafa huku wachache tu wakibahatika kutoroka na kukimbia uwanja wa mapigano kurudi Misri kwa aibu.

Mashujaa hawa waliotaka kujikomboa walikuwa kutoka kabila la Efrahimu, wana wa Yusuph

Huku nyuma Musa aiendelea kutawala Ethiopia kwa miaka 40 mfululizo, na kwa kuwa alikuwa mtu wa haki na hekima na anayemcha Mungu, watu walimpenda sana.

Ila taratibu mbegu ya tamaa ya madaraka kwa baadhi ya wazawa wa Ethiopia na Malkia Adoniah alianza kumea.
Na jambo hili lilikuwa limetoka kwa Mungu, ili Musa atoke Ethiopia aendelee na safari yake ya ukimbizi.

Hoja zikaanza kuibuliwa kumbana ni kwa nini hataki kuwa na mahusiano ya kindoa na Malkia Adoniah ili kuandaa mrithi wa Ufalme wao, jamaa akajitetea lakini Waethiopia hawakumuelewa.

Mwanzoni mambo yalikuwa yanapelekwa kimya kimya ndani ya familia ya Kifalme, lakini baadaye yakageuka na kuwa public issue.

Siku moja kikao kilikaa Ikulu yao huku Musa akiwa juu ya kiti chake cha kifalme na malkia akatamka mbele ya kadamnasi kuwa Mfalme Musa hajawahi kushiriki naye tendo la ndoa kitu kilichozua taharuki.

Musa alipohojiwa ikabidi atamke wazi kuwa hawezi kuvunja tamaduni za kiyahudi na yuko tayari kuachia Ufalme hata kama itabidi, lakini sio kulazimishwa kuoa mtu ambaye si Myahudi wa kwao.

Wenye uchu wa madaraka wakakomaa na hoja hiyo ikabidi Musa kiroho safi aachie Ufalme kwa wazawa, na Menacrus kijana mkubwa wa Malkia akatawazwa kuwa mfalme rasmi.

Ilifanyika sherehe kubwa ya kubadili ufalme kwa amani na Musa akakabidhi ufalme wao huku wakimpa zawadi na kila aina ya shukrani kwa kuwa katika wakati wake aliwatawala vizuri sana na walifanikiwa kweli kweli kisiasa, kijeshi na kiuchumi, na Dola yao ilikuwa kubwa sana ikiogopwa na Misri na Waarabu na Watu wa Edomu na watu Dola ya Afrika.

Musa akakabidhi madaraka kwa amani akiwa na umri wa miaka sitini na sita, na kwa kuwa alikuwa ameshaharibu Misri akiwindwa, mara baada ya kutoka Ethiopia hakuweza kurudi Misri, ilimbidi anyooke moja kwa moja nchi ya Midiani.
Huko ndiko alipokutana na Yethro au maarufu kama Reuel.

Mara baada ya kufika Midian Yethro alikuwa mtu mkuubwa sana maeneo hayo na hakuwa na kijana wa kiume, Musa akamsaidia kama kijana wake wa kiume.

Lakini Yethro alikuwa mtu wa haki sana, akapata uwalakini kwa Musa akimdhani kuwa ni mtu aiyetoroka Ethiopia kwa hiyo alimuweka jela kwa miaka mingi akimshikilia kama mfungwa wake akimnyima chakula na maji mpaka atakapijiridhisha kuwa Musa hakuwa mtu aliyetoroka kutokea Ethiopia.

Binti wa Yethro aliyekuwa anajulikana kwa jina la Sipora alimpenda Musa kimya kimyaakawa anampa chakula na maji kisiri siri bila baba yake kujua.

Jambo lililomsumbua kichwa Yethro ni kwa nini mfungwa wake hafi kwa njaa wala kukonda siku zote hizo, ndipo alipoamua kumfungua baada ya kujadiliana kwa siku nyingi na binti zake.

Hatimaye Musa akaachiwa kwa kifungo cha nje cha kuchunga kondoo.

Kulikuwa na fimbo ambayo Adam alitoka nayo kutoka Bustani ya Edeni akaenda nayo, fimbo hiyo ilirithishwa vizazi kwa vizazi mpaka ikamfikia Nuhu na Nuhu akampa mwanawe Shemu mpaka ikaangukia mikononi mwa Ibrahimu, baadaye Isaka, baadaye Yakobo akaiiba kipindi anaondoka kumkimbia Esau kuelekea kwa mjomba wake Labani.

Na kwa kuwa Esau alikuwa ameshauza haki yake ya uzaliwa wa kwanza hakuona thamani yake hivyo hakuhangaika kuifuatilia.

Fimbo ile Yakobo alipokwenda Misri na wanawe siku za Yusuph, alimpa Yusuph, mara baada ya Yusuph kufa watawala wa Misri kwa kujua maana yake kiroho wakaiiba fimbo ile nyumbani mwa Yusuph wakaificha Ikulu ya Farao wakimkabidhi Yethro kama mmiliki wake.
(Ikumbukwe kuwa Yethro alikuwa mshauri wa Farao, yeye na Balaamu, na aliondoka Misri mara baada kuzinguana na Farao, alimpa ushauri wa kutowatesa Israel maana hata akiwatesa watastawi tu kwa kuwa Mungu alikuwa amemwapia Babu yao Ibahimu juu ya hilo, Farao akaona amedhalilishwa akamnyang'anya nyadhifa zake zote, badala yake akafuata ushauri wa Balaamu wa kuwaua wazaliwa wote wa kwanza, hicho ndicho kipindi alichozaliwa Musa)

Kipindi Yethro anaondoka Misri akabeba na fimbo ile akaondoka nayo mpaka Midiani, alipofika akaichomeka kwenye udongo , fimbo ile ikaanza kuota majani.

Yethro kwa kujua maana yake kiroho akawaamuru watu waliokuwa wanamzunguka kuwa ikiwa mtu anataka kumuoa binti yake Sipora, basi aje aing'oe fimbo ile na aishike mkononi mwake.
Kila aliyejaribu alishindwa.

Mara baada ya Musa kutoka gerezani siku moja bila kujua akaing'oa fimbo ile iliyokuwa ina majani majani, Yethro akashangaa sana na kujua maana yake, kuwa mtu huyu ana nyota ya Kifalme na ndiye atakayewaokoa Israel na kuijenga tena Israel kutokea Misri.

Akampa binti yake Sipora awe mkewe, bila kujua siku nyingi binti alikuwa ashamzimikia Musa kimya kimya.

Musa akamuoa yule binti, na cha ajabu kwa wakati huu akasahau kile kiapo cha kutokuoa watu wa makabila mengine, na akasahau pia kumtahiri kijana wake mkubwa aliyezaliwa hapo hapo Midiani.
Jambo hili lilikuwa makusudi kutoka kwa Mungu.

Na ile fimbo ikawa fimbo yake ya kutembelea tu kama fimbo ya mchunga kondoo, yeye hakujua maana yake, ila Yethro alijua kila kitu maana alikuwa kule ikulu ya Farao.

Ikatokea siku moja katika chunga chunga zake za kondoo, katoto ka mbuzi kakaponyoka kwenye kundi la mbuzi wengine kakaanza kuingia huko milimani.
Musa akaanza kukafuatilia ili akarudishe kundini.

Katoto ka mbuzi kakanyoosha kuelekea karibu na kichaka kimoja kilichokuwa kinawaka moto.

Musa kukiangaia vizuri anashangaa kichaka hakiteketei, aliposogea ashangae jambo hilo, ndipo akapokea wito wake wa kwenda kuwaokoa Israel kule Misri, ambapo wakati huo walikuwa chini ya Farao aliyejulikana kwa jina la Melol.

Farao huyu kwa wasifu alikuwa mtu mfupi mnene, katili, mwenye akili nyingi sana na ndiye aliyeionja joto ya jiwe ya Musa kipindi amerudi kuwaokoa Israel.

Mwisho.

NB:
Simulizi hii imenukuliwa kutoka vyanzo mbali mbali lakini kikubwa kikiwa ni Kitabu cha Yashari au "The Book of Jasher", kitabu ambacho Biblia takatifu inakitaja katika vitabu vya Yoshua na Samweli wa pili.

Yoshua 10:13
Ndipo jua likasimama, na mwezi ukatulia, Hata hilo taifa lilipokuwa limekwisha jipatiliza juu ya adui zao. Hayo je hayakuandikwa katika kitabu cha Yashari?

2Samweli 1:17-18
Basi Daudi akamuombolezea Sauli na Mwanaye maombolezo haya, Kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Yashari.
 
Salute B Asigwa...
Hivi hii habari umeandika wewe au ume copy somewhere?
Nijibu nataka nikuulize.

Nachofahamu mimi Musa alizaliwa misri na kukulia misri baadae ndio akakimbilia midiani. Sasa nashangaa kua alikimbilia misrii.

Lakini swala la yeye kua kiongozi (Mfalme?) Mimi naweza kukubaliana nalo kwani Musa amelelewa na Princess mwana wa Pharaoh na alikua kama Prince Heir kwa pharaoh (Mjukuu wa mfalme Huitwa Prince Heir)
 
Ngumu kumesa....
Lakini kwa kuwa tafiti inapingwa kwa tafiti kitu amvacho mimi sijakifanyia tafiti ngoja nikae kimya
 
Salute B Asigwa...
Hivi hii habari umeandika wewe au ume copy somewhere?
Nijibu nataka nikuulize.

Nachofahamu mimi Musa alizaliwa misri na kukulia misri baadae ndio akakimbilia midiani. Sasa nashangaa kua alikimbilia misrii.

Lakini swala la yeye kua kiongozi (Mfalme?) Mimi naweza kukubaliana nalo kwani Musa amelelewa na Princess mwana wa Pharaoh na alikua kama Prince Heir kwa pharaoh (Mjukuu wa mfalme Huitwa Prince Heir)
Nimeandika mimi mkuu sijaikopi mahali.

Baada ya kukimbia Misri alikwenda Ethiopia kwanza ndipo akakaa kwa miaka 40.
Safari ya kwenda Midiani ilikuwa alipofikisha miaka 66, akakaa kule miaka 14.
 
Daah hii bible kumbe ni summary tu aisee
Biblia ni kitabu cha kiroho mkuu, kila kilichoandikwa mule kina maana kiroho.
Hata nukta ina maana kiroho, ndio maana unaweza kuiona kama summary.

Ila kwa uungwana wa mwandishi wa Biblia ame quote vitabu ambavyo kuna habari kama hio hio.
Mfano kitabu cha Jasher, Kitabu cha Henoko, Kitabu cha Kumbukumbu za Wafalme na vinginevyo ambavyo havipo kwenye Bible.
 
Nimeandika mimi mkuu sijaikopi mahali.

Baada ya kukimbia Misri alikwenda Ethiopia kwanza ndipo akakaa kwa miaka 40.
Safari ya kwenda Midiani ilikuwa alipofikisha miaka 66, akakaa kule miaka 12.
Wee jamaa wewee mbona kama fix vilee. Nashindwa kugain kabisa though nimepata challenge ya kuchimba zaid. Kuna uzi naandaa nitakuita
 
Mkuu mbona Musa alipotoka misiri na wana wa Israel bado alikuwa na mke mkushi(Ethiopia) na sio mmidiani.

Hesabu 12:1
Kisha Miriamu na Haruni wakamnenea Musa kwa sababu ya mwanamke Mkushi aliyekuwa amemwoa; maana, alikuwa amemwoa mwanamke Mkushi.

Inaonyesha Musa alikuwa ameoa mwanamke kutoka Ethiopia na alikaa nae hata alipowatoa watu misiri.


Na kuhusu mkeni ambaye ni shemeji yake Musa vipi?


Waamuzi 1:16
[16]Hao wana wa Mkeni, huyo shemeji yake Musa, wakakwea juu kutoka katika huo mji wa mitende, pamoja na wana wa Yuda, na kuingia hiyo nyika ya Yuda, iliyo upande wa kusini wa Aradi; nao wakaenda na kukaa pamoja na watu hao.
 
Umejitahd Lakn Pia Umedanganya Meng,kabla Wana Wa Yakobo Kurud Ya Ahad Hawakuwa Na Jeshi,bal Walikuwa Watumwa,ivo Hawakuwa Na Nafas Ya Kujikusanya Kama Jesh Na Kwenda Vitan,pia Musa Wakati Huo Alioa Mwanamke Mweusi Asiye Muisrael Ambae Miriam Dadake Musa Alimnung'unikia Kiubaguz Na Mungu Akampga Kwa Ukoma Miriam Kw Sabab Ya Manung'uniko.
Mbona Ujipa Sifa Za Uongo!Kwa Nn Usikop Kama Hukuish Wakati Wa Matukio Hayo?Acha Uongo Uliyaona Hayo!
 
uo
Umejitahd Lakn Pia Umedanganya Meng,kabla Wana Wa Yakobo Kurud Ya Ahad Hawakuwa Na Jeshi,bal Walikuwa Watumwa,ivo Hawakuwa Na Nafas Ya Kujikusanya Kama Jesh Na Kwenda Vitan,pia Musa Wakati Huo Alioa Mwanamke Mweusi Asiye Muisrael Ambae Miriam Dadake Musa Alimnung'unikia Kiubaguz Na Mungu Akampga Kwa Ukoma Miriam Kw Sabab Ya Manung'uniko.
Mbona Ujipa Sifa Za Uongo!Kwa Nn Usikop Kama Hukuish Wakati Wa Matukio Hayo?Acha Uongo Uliyaona Hayo!

uongo wa jamaa upo wapi?
kutokufuatilia kwako ndio uite watu waongo.
Wamidiani ni watu wapi kama si watu weusi kwa rangi?
Ukijua ukweli utakuweka huru
 
Ahsante mkuu kwa Makala nzuri ya kihistoria tutazidi kufuatilia kujua mengi kuhusu Mussa, Wakuu msimpinge kwa kile alichoandika unatakiwa kuongezea yale unayoyajua wewe kuhusu Mussa ili tuunganishe Dots
 
Akili za utumwa nazo ni shida tu. Hao waliowatungia hivyo vitabu wako bize kugundua Advanced technologies nyinyi mmekazana na mihadhara, ubishi, kutoka mishipa tu pimbi kabisa hili ngozi JEUSI.Umaskin shida sana
[/QUOTE]

Sio tatizo lako bali ni ujinga wako. Bakia hivyo hivyo kisha tuone wewe utavumbua nini zaidi ya kutumia vya hao unaowasifia.

Hapa hatubishani bali tunajdili kwa hoja. Maarifa yamehifadhiwa kwenye vitabu. So kusoma vitabu kunatufanya kujua mengi na kuyatumia kwa faida.
 
Back
Top Bottom