Hi ndiyo ilikuwa tofauti kubwa aliyoigundua Nyerere kati ya Mkapa na Kikwete mwaka 1995 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hi ndiyo ilikuwa tofauti kubwa aliyoigundua Nyerere kati ya Mkapa na Kikwete mwaka 1995

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MAGAMBA MATATU, Dec 9, 2011.

 1. MAGAMBA MATATU

  MAGAMBA MATATU JF-Expert Member

  #1
  Dec 9, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 617
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 60
  Hakuna ubishi kuwa Nyerere alijgundua tofauti kubwa sana kati ya Mkapa na Kikwete mnamo mwaka 1995 kipindi cha kumpitisha kwenye halmashauri kuu ya ccm(NEC) kwa ajili ya kugombeaa urais,

  Nyerere aligundua kuwa KIKWETE ni mwanasiasa na MKAPA ni mtendaji.

  JE KUNA TOFAUTI GANI KATI YA MWANASIASA NA MTENDAJI??
  jibulake ni rahisi pale tuu utakapoulinganisha utndaji kazi kati ya MAGUFULI na NGEREJA, ni pale tu utakapoulinganisha utendaji kazi wa Prof. TIBAIJUKA na MKULO. ni pale tu utakapoulinganisha utendaji kazi kati ya aliyekuwa mbunge wa Karatu kipindi hicho Dr SLAA na ZITTO bungeni, ni pale utakapoulinganisha utendaji wa aliyekuwa waziri mkuukipindi hicho EDWAD LOWASA na PINDA hivi sasa, ni pale utakapoulinganisha utendaji kazi kati ya aliyekuwa spika wa bunge enzi hizo Mh SITTA na ANNA MAKINDA.

  Maana yake ni kuwa
  Mkapa alikuwa ni rais wa vitendo zaidi kuliko maneno na Kikwete amekuwa ni rais wa maneno zaidi kuliko vitendo,

  Mafanikio ya Mkapa haya hapa:

  - kaacha chuo kikuu cha Dodoma kikijengwa hadi kukamilika na kutumika kwenye utawala wa kiwete,
  - kaacha uwanja wa kisasa ukijengwa hadi sasa unatumika kwenye utawala wa kikwete,
  - kaacha barabara ya mwanza hadi Dar inajengwa na hadi leo inatumika kwenye utawala wa kikwete,
  - kaacha supermarket ya kimataifa ya mlimani city najengwa hadi sasa inatumika utawala wa kikwete,
  - kaacha uchumi umeimalika japo sasa umeyumba kwenye utawala wa kikwete,
  - Kaacha elimu ikiwa na usawa wa maskini na tajiri japo sasa kama huna pesa husomi utawala wa Kikwete
  - kaacha shilingi ya Tanzania ikiwa imara japo kwa sasa imeyumba na kushuka utawala wa kikwete,
  - kaacha plan ya kuongeza barabara Dar kupunguza foleni japo sasa mpango huo umepotezwa na utawala wa JK
  - Kaacha maji kahama na shinyanga kutoka mwanza japo sasa jk kashindwa kuyafikisha Singida na Dodoma

  HUYO NDO ALIKUWA MKAPA.

  Mafanikio ya Kikwete:
  - kawaunganisha polisi na mahakama kuhakikisha kuwa hakuna mwananchi yeyote anayepinga utawala wake
  - kaunda bunge lenye kuamua chochote kile kwa maslahi ya chama tawala CCM hata kama kinapingwa na watz
  - kaunda baraza la mawaziri wanaosema uongo ili kumfurahisha japo ni chanzo cha umaskini kwa watz,
  - kasababisha chama tawala kiwe na makundi ndani kwa ndani maslahi yao binafsi,
  - kaunda jeshi pilisi la kuhakikisha kuwa pale wanafunzi au wananchi wanapodai haki zao wauawe hata kama kuna uhalali wa kudai haki.

  HUYO NDO KIKWETE


  Baada ya Nyerere kugundua hivyo, hapo ndo aliamua kusema kwa ,maneno yake kuwa "KAMA NEC MKIAMUA KUMPITISHA JK KAMA MGOMBEA URAIS BASI NIKO TAYARI KUWASHAWISHI WATANZANIA KUWAPIGIA KURA WAPINZANI NA SI KUWAPA KIONGOZI WA AINA HII"

  hapo ndo naamini kuna umhimu wa kuwa na rais aliye serious kwa kutotanguliza maneno badala ya vitendo.

  JE TUTAFIKA.
   
 2. Ng`wanakidiku

  Ng`wanakidiku JF-Expert Member

  #2
  Dec 9, 2011
  Joined: Apr 18, 2009
  Messages: 1,196
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hongera uchambuzi mzuri, sema tatizo watanzania ni mazuzu! wakipewa sh10,000 na kuambiwa CCM oye basi mpaka gego la mwisho utaliona, na baada ya hapo huyo huyo mtanzania anaanza kulalamika eti serikali haitujali, eti mara ufisadi! Safari ni ndefu, Tanzania bado wajinga ni wengi!!!
   
 3. nickname

  nickname JF-Expert Member

  #3
  Dec 9, 2011
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 516
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Nimeipenda post hii hakika ni uchambuzi mzuri na wa ukweli.Thanks
   
 4. only83

  only83 JF-Expert Member

  #4
  Dec 9, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  JK atakumbukwa kwa siasa uchwara na ulegelege wake...na mtu asiyejali maneno na vilio vya watu masikini,sijui ni mtu wa namna gani huyu jamaa...ati wakuu!!
   
 5. Atubela

  Atubela JF-Expert Member

  #5
  Dec 9, 2011
  Joined: Aug 15, 2011
  Messages: 637
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 180
  Sio uzuzu tu, Kikwete ni bingwa wa kuchakachua kura, akiitumia NEC pamoja na usalama wa taifa.
   
 6. MAGAMBA MATATU

  MAGAMBA MATATU JF-Expert Member

  #6
  Dec 9, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 617
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 60
  Hata mimi mkuu bado sijamuelewa kabisa kuwani mtu wa aina gani!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 7. Alwatan

  Alwatan JF-Expert Member

  #7
  Dec 9, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 409
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Kajipange tena halafu ndio urudi na huu ushuzi wako wa kusadikika.

  Mwalimu hakuwahi kutamka maneno hayo kama unavyomnukuu. Sababu kuu ni tatu,
  • Mgombea Urais wa CCM anachaguliwa na MKUTANO MKUU WA CCM na sio NEC ya CCM.
  • Wagombea walikua WATATU KIKWETE, MKAPA na MSUYA
  • MWALIMU asingeweza kufanya such a fragrant VIOLATION ya demokrasia mbele ya mkutano wa chama. Inaelekea humjui Mwalimu na wala huna haja ya kumjua alikua ni mtu wa aina gani wakati wa uongozi wake.
  Jambo moja alilotamka lakini hukuliandika ni swali alilomuuliza LOWASSA: "Je umepata wapi mali nyingi kiasi hiki, kwa umri ulionao, wakati toka umalize chuo kikuu umekua ni mtumishi wa UMMA? Wakati hata mimi niliyekuwa rais wenu kwa miaka 24 sinazo?"

  Majibu ya hapo, fuatilia simulizi za Mzee Kasori, Katibu Mstaafu wa Mwalimu. Zimo humu JF.
   
 8. T

  Topical JF-Expert Member

  #8
  Dec 9, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Eti mkapa kajenga chuo kikuu udom ..siyo kweli

  Acha ushabiki dogo, mkapa anasifika kwa kuuza mali za umma kuanzia nyumba hadi madini
   
 9. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #9
  Dec 9, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Nimependa sana uchambuzi huu. Hongera sana mtoa mada. Na ulivyoeleza ni ukweli mtupu na kwa sasa hakuna atakaye tokea kama baba wa taifa, ambaye anaweza sema fulani hafai waliopo wote sasa ni wasanii na maslahi binafsi.
   
 10. kingxvi

  kingxvi JF-Expert Member

  #10
  Dec 9, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wewe jamaa mvivu wa kufikiri sana inaonekana ulikuwa tu na hamu yakuanzisha post
   
 11. Papa D

  Papa D JF-Expert Member

  #11
  Dec 9, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nakubaliana na wewe kuwa Mkapa alikuwa Mtendaji si mwanasiasa. ndiyo sababu alisimamia alichoamini kuwa sahihi hata kama baadaye kikaonekana si sahihi. a leader has to make a decision not follow a decision!!. Tukio moja ambalo mpaka hii leo nampa heshma mzee mkapa ni pale alipokataa kupandisha mishahara ya watumishi wa umma kwa hoja za msingi ambazo wafanayakazi waliridhika nazo alisema hivi:-

  Ninatakapopandisha mishahara mfumuko wa bei utaongezeka na hiyo mishahara itaonekana haina msaada. Jamba ninalofanya ni kudhibiti mfumuko wa bei hili hiyo mishahara kidogo ninayotoa iweze kukidhi mahitaji yenu. Hapo alisema alichoamini ni sahihi na baada ya miaka kadhaa kilidhihirika kuwa ni cha msingi.

  That's what a leader s made of!! JK alipoambiwa aongeze mishahara kwanza akadanya idadi ya watumishi wa umma, pili akadanganya mapato yanayohitajika kuwalipa watumishi. mambo haya yote si ya kiongozi mtendaji!!
   
 12. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #12
  Dec 9, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  si mkwer.e jamani cha kujiuliza ni lini mk.were akawa kiongozi wa serikali? Kwakweli tujilaumu wenyewe kwa kumchagua awamu ya kwanza 2005
   
 13. L

  Leonard Akaro JF Gold Member

  #13
  Dec 9, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Brother safi sana kwa uchambuzi murua.
   
 14. MAGAMBA MATATU

  MAGAMBA MATATU JF-Expert Member

  #14
  Dec 9, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 617
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 60
  unaweza ukauza mali lakini ukawa na akili ya kuwakumbuka waliokuweka madarakani, ni tofauti na yule anayesema hana haja na kura za watu kwa kujua ana mbinu zake mbadala za kumuweka madarakani.
   
 15. R

  Rugemeleza Verified User

  #15
  Dec 9, 2011
  Joined: Oct 26, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  MAONI YANGU:

  Kulinganisha Mkapa na Kikwete ni kama kupima mafuta katika Kitumbua na Andazi. Wote wamepikwa kwa mafuta. Mkapa aluza rasilimali zetu, karuhusu kuuawa wachimbaji wadogo Bulyanhulu, uzembe na vifo vya MV.Bukoba, kaua Tanesco na kuikabidhi kwa kampuni uchwara ya Net Solutions Group(ya kwake), kagawa bure NBC. Kauza nyumba za serikali. Ubabe wa polisi, mauaji ya Mwembechai na Pemba.

  Kizuri chake, kujenga uwanja mpya wa taifa, na kuruhusu wasitaafu wa serikali kupokea mafao kufa kwao.
  Kikwete kuchakachua uchaguzi, kuchekelea kuporwa rasilimali zetu, ufisadi mtindo mmoja, mauaji na mabavu dhidi ya wapinzani, kukataa kupambana na ufisadi wa Deep Green, Meremeta, EPA na Kagoda (isipokuwa wachache wa kafara),ufisadi mkubwa mawizarani, halimashauri za wilaya. Kujenga misingi ya udini na ukabila na mgawanyiko wa ajabu.Zanzibar kuamua kujitenga kwa kutunga sheria mpya huku akiona hilo si tatizo. Safari za nje mtindo mmoja.

  Mazuri: Chuo cha Udom na ujenzi wa barabara.

  Mwisho wa siku ni bora kupanga mikakati mipya ya kupata uongozi wenye uono, upeo na mapenzi makubwa kwa nchi yetu na watu wake na mikakati ya namna ya kuitoa nchi yetu katika lindi la umasikini, maradhi, ujinga, ufisadi na utengano wa kikabila, kikanda na kidini.
   
 16. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #16
  Dec 9, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mkuu nakushukuru na kukupongeza kwa fact zako japo hapo kwa lowasa sitokuunga mkono, Pia Jk anayajua yote hayo ila katia pamba masikioni hataki kusikiliza wala kuyakataa maovu na mabaya yote
   
 17. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #17
  Dec 9, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Elfu kumi nyingi hivyo ni Tshirt na kofia au kanga basi umemaliza kuteka haki zao zote
   
 18. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #18
  Dec 9, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Ukizipata fanya kuzi attach humu ili mwongo ajulikane now
   
 19. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #19
  Dec 9, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Bora yeye alikuwa anajua kula na kipofu sasa huyu mwenzetu akila na kipofu anamlamba mikono na kuiburuza kwenye vumbi, nikiwa na maana kwamba Jk anaiba zaidi kuliko utaendaji na kuwajibika huku mkapa akijitahidi kuimarisha uchumi
   
 20. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #20
  Dec 9, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Na Kikwete je? Aliyesaini mikataba ya madini na Barrick ni nani? Chuo kikuu cha UDOM kimeanza kujengwa under Mkapa's rule.
   
Loading...