Hezbollah: Suala la Quds litapelekea kuangamizwa kikamilifu kwa utawala wa Israel

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,991
17,888
Nasrallah: Hujuma dhidi ya Quds ina maana ya vita vya kieneo na kuangamia Israel.

Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon ameuonya utawala wa Kizayuni wa Israel kuwa hujuma dhidi ya maeneo matukufu katika mji wa Quds (Jerusalem) inaweza kupelekea kuibuka vita vya kieneo na kuangamizwa utawala huo wa Kizayuni.

Sayyed Hassan Nasrallah ameyasema hayo katika hotuba kwa njia ya televisheni Jumanne usiku, ikiwa ni hotuba yake ya kwanza tokea harakati za Palestina zitangaze ushindi katika vita na utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Ghaza. Aidha ametoa hotuba hiyo kwa mnasaba wa Siku ya Kitaifa ya Mapambano na Ukombozi. Katika siku hii Walebanon huadhimisha ushindi wao dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel mwaka 2000.

Katika hotuba yake, Sayyid Nasrallah amesema, ushindi wa Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza umewashangaza marafiki na maadui. Ameongeza kuwa utawala wa Israel ulikosea katika mahesabu yake huku akipongeza harakati za mapambano ya Kiislamu au muqawama Palestina kwa kusimama kidete dhidi ya Wazayuni.

Kiongozi wa Hizbullah ameuonya vikali utawala wa Kizayuni wa Israel na kusema: “Mnapaswa kufahamu kuwa kuudhuru mji wa Quds, Msikiti wa Al Aqsa na matukufu ya mataifa ni tofautu na hujumba zingine mnazotekeleza.” Nasrallah ameonya kuwa, iwapo Israel itauhujumu Msikiti wa al Aqsa na maeneo matakatifu mjini Quds, jibu la jinai hiyo halitatoka tu katika mipaka ya Ghaza bali kutaibuka vita vya kieneo na hatimaye Israel itaangamizwa.

Amesema pale maeneo matakatifu ya Waislamu na Waktristo yanapokabiliwa na hatari, harakati za muqawama haziwezi kukaa kimya na kuwa watazamaji.

Aidha amesema “Oparesheni ya Upanga wa Quds” ya makundi ya muqawama ya Palestina hivi karibuni katika Ukanda wa Ghaza ilikuwa ni pigo kubwa kwa madola ya Kiarabu ambayo yanatekeleza mpango wa kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala bandia wa Israel katika fremu ya ‘Muamala wa Karne’.

Israel ilianzisha vita dhidi ya raia wa Palestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na huko Ghaza tangu tarehe 10 mwezi huu wa Mei; na kumalizika tarehe 21 kufuatia ombi la baraza la mawaziri la utawala wa Kizayuni na upatanishi wa baadhi ya pande ajinabi baada ya kushindwa jeshi la utawala huo kukabiliana na wanamuqawama wa Palestina.
 
Ushindi watu wako wamekufa 200+ na aliyeshindwa watu wake wamekufa 22 hii tafsiri ya wapi, kwani sahivi anayeruhusu watu waende kusali au wasiende si Israeli inaama yeye ndo mmiliki tatizo Arab wana akili ndogo sana
Yani akili zao wanazijua wenyewe kipindi cha vita walikua wanalalamika kwamba israel inaionea palestina mara wanalalamika palestina haina jeshi alafu israel inashambulia kijeshi kamili baada ya vita kuisha wanaanza kutangaza ushindi
 
Nasrallah: Hujuma dhidi ya Quds ina maana ya vita vya kieneo na kuangamia Israel.

Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon ameuonya utawala wa Kizayuni wa Israel kuwa hujuma dhidi ya maeneo matukufu katika mji wa Quds (Jerusalem) inaweza kupelekea kuibuka vita vya kieneo na kuangamizwa utawala huo wa Kizayuni.

Sayyed Hassan Nasrallah ameyasema hayo katika hotuba kwa njia ya televisheni Jumanne usiku, ikiwa ni hotuba yake ya kwanza tokea harakati za Palestina zitangaze ushindi katika vita na utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Ghaza. Aidha ametoa hotuba hiyo kwa mnasaba wa Siku ya Kitaifa ya Mapambano na Ukombozi. Katika siku hii Walebanon huadhimisha ushindi wao dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel mwaka 2000.

Katika hotuba yake, Sayyid Nasrallah amesema, ushindi wa Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza umewashangaza marafiki na maadui. Ameongeza kuwa utawala wa Israel ulikosea katika mahesabu yake huku akipongeza harakati za mapambano ya Kiislamu au muqawama Palestina kwa kusimama kidete dhidi ya Wazayuni.

Kiongozi wa Hizbullah ameuonya vikali utawala wa Kizayuni wa Israel na kusema: “Mnapaswa kufahamu kuwa kuudhuru mji wa Quds, Msikiti wa Al Aqsa na matukufu ya mataifa ni tofautu na hujumba zingine mnazotekeleza.” Nasrallah ameonya kuwa, iwapo Israel itauhujumu Msikiti wa al Aqsa na maeneo matakatifu mjini Quds, jibu la jinai hiyo halitatoka tu katika mipaka ya Ghaza bali kutaibuka vita vya kieneo na hatimaye Israel itaangamizwa.

Amesema pale maeneo matakatifu ya Waislamu na Waktristo yanapokabiliwa na hatari, harakati za muqawama haziwezi kukaa kimya na kuwa watazamaji.

Aidha amesema “Oparesheni ya Upanga wa Quds” ya makundi ya muqawama ya Palestina hivi karibuni katika Ukanda wa Ghaza ilikuwa ni pigo kubwa kwa madola ya Kiarabu ambayo yanatekeleza mpango wa kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala bandia wa Israel katika fremu ya ‘Muamala wa Karne’.

Israel ilianzisha vita dhidi ya raia wa Palestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na huko Ghaza tangu tarehe 10 mwezi huu wa Mei; na kumalizika tarehe 21 kufuatia ombi la baraza la mawaziri la utawala wa Kizayuni na upatanishi wa baadhi ya pande ajinabi baada ya kushindwa jeshi la utawala huo kukabiliana na wanamuqawama wa Palestina.
Fedha zinachangwa ili mji wa gaza ujengwe kutokana na Vita hii ya siku kadhaa hapo hapo unasema palestina kwenye hi Vita wao ndo wameshinda
 
Angalia matokeo operation ilivyokua
IMG_20210527_173438.jpg
 
Mbona kila siku ni mikwara tupu... Sera zao ni kuifuta Israel so wanasahau irani za vyama vyao? washashindwa kuiangamiza Israel wanaanza kusingizia Jerusalem... na Israel kamwe hatoiacha Jerusalem ndio fact... na viherehere vikizidi arabs wataondoshwa wote ndani ya nchi ya Israel wachague tu kutulia au genye
 
Mkuu upo mashariki ya kati nn,naona habari zako nyingi ni za Israel na majirani zake tu
 
Nilichogundua Iran wanaipenda sana Israel au sababu wameweza fanikiwa kuiba siri za silaha zao so now wanafyatua tu vifaa vinavyofanana kabisa na vya israel... Kila siku wao ni Kuitaja Israel kwa namna yeyote ile

1622149333044.png
 
Huyu gaidi wa Hezbollah anataka Lebanon ichezee mashambulizi ya anga zaidi ya Gaza nyumba nyingi wanazotumia kuficha silaha zao na wao zitageuzwa vifusi Israel imeapaa kujibu kwa nguvu kubwa shambulizi lolote la Hezbollah
 
Back
Top Bottom