robbinhood
JF-Expert Member
- Apr 19, 2020
- 524
- 1,521
HESLB YATOA SIKU TANO (05) ZAIDI KUOMBA MKOPO
Ni kuanzia Oktoba 1 hadi 5, 2020
Lengo ni kuwapa fursa vijana waliokuwa JKT kuomba
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inawajulisha wanafunzi waliomaliza mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) hivi karibuni kuwa mfumo wa kuomba mkopo kwa njia ya mtandao utafunguliwa kwa siku tano (05)kuanzia kesho, Ijumaa, Oktoba 1, 2020 ili kuwawezesha kuomba mkopo.
Uamuzi huu unatokana na maombi ya wanafunzi, wazazi na walezi wa wanafunzi wahitaji ambao hawakuweza kuomba au kukamilisha maombi yao kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kujiunga na mafunzo katika kambi mbalimbali za JKT kwa mujibu wa sheria.
Aidha, katika muda huo wa siku tano, mfumo pia utakuwa wazi ili kuwawezesha waombaji ambao maombi yao yana upungufu kurekebisha kwa kuweka nyaraka sahihi ili kuiwezesha HESLB kuendelea na hatua nyingine.
“Kwa wanaorekebisha taarifa, wanapaswa kuingia katika akaunti zao walizofungua kuombea mkopo na watapata ujumbe kuhusu maeneo ya kurekebisha. Tunawasihi watumie muda huu wa siku tano kurekebisha na kukamilisha maombi yao ili kutuwezesha kuendelea na hatua inayofuata ili hatimaye wenye sifa wawezeshwe kutimiza ndoto zao,” amesema Mkurugenzai Mtendaji wa HESLB Abdul-Razaq Badru.