Heslb yatoa siku 90 waliokosa mikopo kukata rufaa

Bibi Mikopo

Senior Member
May 15, 2015
177
33
Wakuu,
Nimeona niwashirikishe hii:

HESLB yatoa siku 90 walikosa mikopo kukata rufaa


Na Mwandishi Wetu

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza siku 90 kuanzia leo (Jumatatu, Oktoba 31, 2016) kwa waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2016/2017 kukata rufaa kwa njia ya mtandao ikiwa hawajaridhsihwa na matokeo ya upangaji uliotangazwa hivi karibuni.

Serikali imetenga Tshs 483 bilioni kwa ajili ya kutoa mikopo kwa jumla wanafunzi 119,012 – kati yao, wanafunzi 93,295 ni wanaondelea na masomo na wanafunzi 25,717 ni wa mwaka wa kwanza. Hadi sasa, jumla ya wanafunzi 20,183 wa mwaka wa kwanza wameshapata mikopo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo (Jumatatu, Oktoba 31, 2016) na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul-Razaq Badru, Bodi imeanza kupokea rufaa hizo kwa njia ya mtandao (Online Loan Application and Management System) kuanzia leo (Oktoba 31, 2016) hadi Januari 31, 2017.

“Wanachotakiwa kufanya wanafunzi ni kulipa Tshs 10,000.00 kwa njia ya M-Pesa na kuingia katika mtandao wetu wa http://olas.heslb.go.tz na kujaza fomu, kuichapa na kuiwasilisha kwa Afisa Mikopo wa chuo chake ambaye atawasilisha kwetu fomu zote za chuo chake kwa barua kwa ajili ya sisi kuzifanyia kazi,” amesema Bw. Badru.

Bw. Badru, katika taarifa yake inayopatikana pia katika tovuti ya HESLB (www.heslb.go.tz) ameongeza kuwa Bodi haitapokea wala kuzifanyia kazi fomu za rufaa ambazo zitawasilishwa Bodi na wanafunzi bila kupitia kwa maaifsa mikopo wa vyuo vyao.
--------------
 

Attachments

  • HESLB STATEMENT - APPEAL AGAINST MEANS TESTING RESULTS 2016-17.pdf
    163.8 KB · Views: 212
Jamani hii sii namna ya kuvuna hela kweli? Kuna watu lukuki walilipa 30000 wakaambiwa hawana vigezo,hizo hela zinaenda wapi.!!Kwanini wanaonea wazazi lakini?Hivi kama wana nia ya dhati kwanini watu wasiombe kwanza afu wale waliofanikiwa ndio walipe hizo hela kama walivyokua wanafanya TCU huko nyuma.Jamani nani atasimama juu ya huu uonevu????
 
Kwa hiyo vyuo vitaturuhusu kusoma bila kulipa ada hadi rufaa itoe majibu?
 
Nimeamini mutegemea cha ndugu hufaa maskini ambao hatuna uwezo tuende tuu kitaani !!!! Kweriii siku 90 sikutufukuza kinamuna kweri. Yaaani MTU huna pesa ya ada harafu upo chuoni unambiwa ukate rufaaa wakati chuo wanataka ada yao
 
Wekeza Bima Ya Elimu ya watoto wako mapema tangu yuko secondary alifika Chuo we unaenda banks unalipa ada mtoto anasoma
f15e891a67e492afe28ea3146cf8e22b.jpg
 
Nimeamini mutegemea cha ndugu hufaa maskini ambao hatuna uwezo tuende tuu kitaani !!!! Kweriii siku 90 sikutufukuza kinamuna kweri. Yaaani MTU huna pesa ya ada harafu upo chuoni unambiwa ukate rufaaa wakati chuo wanataka ada yao
Sijui kwa nini Badru haulizwi maswali kama haya!
 
Huyu Badru sijui Albadir wamemwokota wapi huyu? Geez! Watoto wa masikini kutoka mikoani wanarudi nyumbani. Sasa wanawakamua tena 10,000 eti rufaa. Mungu Anawaona!
 
Back
Top Bottom