HESLB Wanavyotafuna Mikopo na Uchunguzi wa Bodi 2011

Mikopo ya vyuo vya nje iangaliwe upya. Napendekeza serikali iweke nguvu zake kuboresha na kutanua vyuo vya ndani ili vichukue wanafunzi wengi zaidi..
 
Halafu kama hili la wanafunzi wa nje ilitakiwa sheria ya mikopo kwa elimu ya juu iwe clear kwa wale waliokuwa wanapelekwa nje ya nchi kwani kiasi cha fedha kinachotolewa kwa siku kilitakiwa kiendane na hali ya maisha ya nchi husika.Wakati mwingine unakuta hata fedha zinazotolewa kwa wanafunzi wa nje haziwatoshi kwani unakuta gharama za maisha kwa nchi fulani ni tofauti na Tanzania,aidha unakuta exchange rate kati ya dola na shilingi kuna risk flani na kati ya dola na sarafu ya nchi kama India ni tofauti kabisa.Lakini Bodi katika hali ya kushangaza haikuweza kutilia maanani jambo hili.
 
Hivi hakumshangaa kwanini wakati wanaleta mabadiliko ya sheria ya Bodi ya Mikopo hakuna kipengele hata kimoja kinachowahusu wanafunzi wa nje?
 
Mwanakijiji,
Hilo hapo nililifikiria mkuu ndiyo maana nikasema ile sheria ina mapungufu yake kwani hakuna kipengele kinachowahusu wanafunzi wa nje.Sasa sijui wanatumia kili kifungu kinachohusu wanafunzi wa huko nyumbani au vipi.Ndio maana hata ukiangalia fedha wanayotenga kiasi ni kile kile cha nyumbani ili hali gharama za maisha zinatofautiana
 
Ben.. ndio maana utaona maajabu ya serikali yetu... wakati wanawarudisha Watanzania wa Ukraine kwa kisingizio cha "gharama" serikali hiyo hiyo inawalipia wanafunzi nyumbani kwa kiwango kile kile cha Ukraine au zaidi!
 
Sasa huku hata ubalozi unasema hauwezi hata kuwakopesha wanafunzi pale bodi wanaposuasua kutuma fedha mapema.Unajua kuna hatua ambazo watu wakichukua zitalidhalilisha sana taifa?Zaidi ya miezi miwili ugenini watu wameshaanza masomo lakini bado hela hawajapewa sasa sijui kisingizio chao kitakua nini tena.Na ni kwa nini wadanganye wameshatuma?
 
Halafu wizara inadai kuhusu suala la kuongeza fedha ni mpaka mtu atakapotoka huko nyumbani aje aandike ripoti.Sasa hapa najiuliza kwanini wasitumie ubalozi kwani hawa ndio wwako huku mda mrefu na wana experience maisha ya kila siku ya huku kuliko kutuma mtu atakaekuja na kukaa wiki au mwezi mmoja na kutuma ripoti.

Je,hataandika ripoti isiyo sahihi?

Je,nini kazi za ubalozi kama haziwezi kushughulikia suala kama hilo ni yapi basi ambayo wanaweza?

Je,hakuna ubadhirifu au matumizi mabaya ya fedha pasipo ulazima wowote kwa kutuma mtu au watu kutoka huko ilihali huku kuna maofisa wa ubalozi ambao wako huku huku wangeweza kuifanya hiyo kazi kwa ukamilifu huku watanzania wengi wakiishi kwa dhiki?

Naomba kuuliza!

Tafadhali naomba mwenye kunielewesha hapa.
 
thanks MM, Nchi yetu ni ya uonevu kila kona, Mwisho wao waja!
 
Wenzenu hawajali wala nini, leo hii bado wana matatizo Bodi ya Mikopo na inashangaza kuwa bado Msolla na timu nzima iliyovurunda miaka mitano sasa bado wapo na wanatarajiwa kufanya vizuri
 
RAIS Jakaya Kikwete ameombwa achukue hatua za haraka zitakazowasaidia wanafunzi 300 wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), ambao wapo hatarini kufukuzwa kutokana na kukosa ada.
Wanafunzi hao wako kwenye uwezekano mkubwa wa kushindwa kuendelea na masomo na baadhi yao wamesharejea nyumbani baada ya kujulishwa kwamba Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB), haitawapatia mikopo ya kuwadhamini masomo yao.

Taarifa ambazo gazeti hili linazo, zinaeleza kuwa wanafunzi wa fani mbalimbali zikiwemo biashara, benki, uhasibu, ugavi, kodi na fedha wengi wao wakiwa ni wasichana waliopata daraja la tatu, walifika chuoni hapo baada ya kuomba na kutimiza vigezo vya kudahiliwa kujiunga na chuo hicho.

Baada ya kufanikiwa kufikia hatua hiyo, waliwasilisha maombi yao Bodi ya Mikopo na wakakubaliwa kupata udhamini kwa viwango mbalimbali kwa kadiri ya mahitaji yao.

Tangazo la kustahili kwao kupewa mikopo lilitolewa na bodi katika tovuti yake Septemba mwaka huu wiki chache baada ya kumalizika kwa kikao cha Bunge la Bajeti mjini Dodoma.

Hata hivyo, mpaka sasa wanafunzi hao hawajapewa mikopo yao na viongozi wao wamewaeleza kwamba bodi imewajulisha kuwa hawastahili kupatiwa mikopo hiyo.

Mmoja wa viongiozi wa wanafunzi hao aliyezungumza na gazeti hili, alisema wanashangazwa na hatua ya Bodi ya Mikopo kuwaachia jukumu hilo wao (viongozi).

"Walitutaka sisi ndio tuwaeleze wanafunzi wenzetu kuwa hatustahili kupatiwa mikopo, hili ni jambio la ajabu kidogo kwa sababu iwapo wanafunzi watatutaka tutoe maelezo kwa nini wamenyimwa mikopo, hatujui tutawaeleza nini," alisema.

Wanafunzi hao wameamua kumlilia Rais Kikwete kwani Februari mwaka huu, katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam, aliahidi kuwa atawasiliana na chama chake (CCM) kutafuta ufumbuzi wa suala hili na kwamba taarifa zingetolewa baada ya mwezi mmoja kuhusu hatua ambayo ingefikiwa.

"Rais alisisitiza wakati ule, na amekuwa akirudia kila mara kuwa hakuna mwanafunzi atakayeshindwa kuendelea na masomo kwa kushindwa ku
 
I am so mad... people can't just imagine.. Kwanini Msolla bado ni Waziri wa Elimu ya Juu, hivi hadi mtu aboronge kiasi gani ndipo Rais Kikwete atajua huyo mtu hamfai?
 
Sasa hii nchi kila kitu anapelekewe JK ina maana wengine hawafanyi kazi au namna gani? Ataweza yote haya?

JK inabidi atoe picha kwamba the government is more than him, ili watu wakiwa na matatizo wajue pakwenda!
 
NASIKITISHWA NA UTENDAJI KAZI WA HAPO LOAN BOARD.KWA MFANO HAPO LOAN BOAARD KUNA MAMA MMOJA ANAITWA ANNA SIJUI JINA LAKE LA PILI ANAHUSIKA NA KUPROCESS MAJINA YA WANAFUNZI ILI WAPATE FEDHA ZAO TATIZO NI KWAMBA MAMA HUYU AMEKUWA FISADI SANA KIASI KWAMBA FEDHA ZINAZOTAKIWA KUKOPESHWA MWANAFUNZI NI KAMA ZAKE VILE KWA MAJIBU YAKE MABOVU.
MFANO UNAOONYESHA MAMA HUYU ALIVYOSIMUWAJIBIKAJI KWA KAZI YAKE NI PALE ANAPOJIBU "FORM YAKO YA KUOMBA MKOPO IMEFIKA LAKINI SINA MUDA WA KUITAFUTA ILI NIJAZE BAADHI YA DATA NA KWASABABU SINA MUDA HUTAPATA MKOPO",AU ANAPOSEMA"FORM ZIMEPOKELEWA HAPA LOAN BOARD LAKINI FORM HAIONEKANI HIVYO HATUWEZI KUKUPA MKOPO"
HESLB WAMEKUWA WAKIPOTEZA FORMS NYINGI ZA WANAFUNZI NA WAKIFIKA HAPO KUZIFUATILIA WAMEKUWA WAKIPEWA MAJIBU YA KUKATISHA TAMAA KAMA DADA ANNA WA HAPO HESLB ANAVYOJIBU HAPO JUU.JE HAPO HESLB HAKUNA UONGOZI? NA UNAWAJIBIKA KWA NANI?
SAA ZINGINE TUNAWEZA KUWALAUMU KINA MSOLA KUMBE WABOVU NI WAFANYAKAZI HAPO HAPO LOANS BOARD HASA HASA HUYU DADA ANNA.
TAFADHARI WAHUSIKA WASHUGHULIKIENI WABOVU HAWA HESLB
GIVE ME FREEDOM OR KILL ME
 
Mnyari I will choose ur second option to KILL U.

MMh hoja tumeiona ila hapa kuna mambo machache nasema.

1. Jamani nadhani tunahitaji definition ya ufisadi maana sijaelewa inakuwa je.

2. Naona kwa wewe tatizo kubwa sio HESLB bali ni huyo Anna. Nadhani tatizo ni uongozi mzima kuanzia Msola. Msola kama mkuu wa kazi kama hawajibiki usitegemee watumishi watawajibika. Yeye anauwezo wa kuwawajibisha hao wengine.

Tatizo la hii Bodi ni kubwa sana. Kuna vijana wako Arusha huko Chuo cha uhasibu wanamaliza semister bado hawajapata pesa. Tatizo ni bodo nzima na mimi hakika ningependekeza hii bodi ivunjwe na ipitiwe upya.
 
Lakini tujiulize! kwani tukibadili mfumo na hii kazi ya kukopesha wanafunzi ikafanywa na mabenki kama NMB na CRDB itakuwa na madhara gani!! mbona mamalishe wanakopeshwa mabilioni ya kikwete through bank, nadhani afrika ya kusini kuna mabenki kama standard bank of sauth africa hukopesha wanafunzi yanafanyaje?

Pia kuhusu ukusanyaji wa madeni haya kwanini isifanywe na TRA kwa kushirikiana na bank husika, kwani kupitia list ya PAYE wanaweza kuwapata wadaiwa kwa ufanisi mkubwa, wadaiwa sugu TRA ikatafuta agents au court brokers wakahangaika nao!

Nadhani HELSB wanapaswa kuwa co-ordinators na kushughulika na rufaa za wanafunzi au wadaiwa tu, sasa hivi HELSB ni kama benki bubu.
 
Back
Top Bottom