Ukifika ofisi za Bodi ya Mkopo Elimu ya Juu unachokutana nacho ni foleni kubwa ya watu waliomaliza makato kusitisha mwezi mmoja au miwili na baada ya hapo ni kuanzia tena kukatwa kupitia mshahara. Ukifika kulalamika wanakupa fomu ujaze na baadae unapewa barua kwenda kwa mwajiri kusitisha. Maswali anayotakiwa Prof. Mkenda kuwauliza Hawa wapigaji. Kwanza, kwa nini tujaze formu na tupeleke barua ya kusitisha wakati Kila marejesho yanapofanyika kiasi Cha Salio la mkopo huonekana kwenye salary slip? Pili, Kwa nini hawatoi hundi ya kurejeshewa makato yaliyofanyika kimakosa papo hapo? Tatu, watarekebisha lini system yao ya kudai kurejeshewa malipo yaliyokatwa kimakosa?. Waziri wa Elimu , Mhe. Rais anaposema na hili nalo ukalitazame ulimuelewa anamaanisha nini? Hebu tembelea Bodi yako ya Mikopo Elimu ya Juu usiende kuishia kutazama tu.