HESLB: Wanafunzi 47,305 wapata mikopo Awamu ya Kwanza

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu (HESLB) imetangaza orodha ya wanafunzi 47,305 watakaopata mikopo ya awamu ya kwanza.

Imesema inatarajia kutumia Sh150.03 bilioni kutoa mikopo hiyo kwa mwaka wa masomo 2020/2021.

Orodha hiyo imetajwa leo Jumatano Novemba 11, 2020 na mkurugenzi mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru takribani wiki moja kabla ya vyuo kufunguliwa.

Amesema kati ya wanafunzi 47,305, wanaume ni 26,964 sawa na asilimia 57.37 na wanawake 20,341 sawa na asilimia 42.63.

Badru amesema tayari fedha zimeanza kupelekwa katika vyuo mbalimbali na kuwataka wanafunzi kupata taarifa za kina katika akaunti walizotumia kuomba mkopo maarufu SIPA na kujiandaa kwenda vyuoni kwa ajili ya kujisajili.

“Serikali imeshatupatia fedha na tumeanza kuzipeleka vyuoni lengo letu ni kuhakikisha wanafunzi wenye sifa wanazikuta fedha vyuoni ambako watajisajili na kupokea ili watimize ndoto zao,” amesema.

Kuhusu kutangazwa kwa orodha ya Awamu ya Pili, Badru amesema imepangwa kutolewa Novemba 14, 2020 baada ya kukamilisha uchambuzi wa maombi unaoendelea na kuwataka waombaji wa mikopo kutembelea akaunti zao za SIPA kupata taarifa kuhusu maombi yao.

Hata hivyo amesema upangaji wa mikopo kwa wanafunzi wa mwaka wa pili unaendelea.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom