MKEHA
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 713
- 1,136
Habari waungwana? Nimekuwa nikipita mitaani na kuongea na marafiki na jamaa zangu walioko serikalini, kwa kweli wanaumizwa sana na deni la HESLB.
Sheria inatoa mwanya kuchukuliwa kwa % 15 ya mishahara yao ghafi kulipia deni hilo la elimu ya juu. Sio mbaya sana kwani dawa ya deni ni kulipa. Lakini kwa wafanyakazi walioko kwenye vyombo vya ulinzi wangepata msamaha wa deni hilo. Nina sababu kadhaa za kwanini wasamehewe.
1. Deni la HESLB huwa linaleta stress kwa mtu akiwa analipa deni hilo. Mtu hukosa utulivu wa akili kila akiangalia salary slip yake hivyo kuwa na mawazo muda mwingi.
2. Vyombo vyetu vya ulinzi vina kazi ya ziada kuhalikisha tuko salama usiku na mchana, hivyo inakuwa kama zawadi kwa kazi hiyo mgumu sana ya kulinda raia, mali na mipaka ya nchi yetu.
3.Wanufaika wa HESLB waliopo kwenye vyombo hivyo sio wengi sana kiasi kwamba serikali itapoteza fedha nyingi.
4. Kama kwenye huduma zingine za umma huwa vyombo vyetu hupewa kipaumbele kama vile kwenye usafiri, mabenki kwanini hapa serikali isifumbe macho.
5. Kwa watumishi wengine kupanda cheo ni baada ya muda flani ukifika unapenda cheo kwa kujaza OPRAS, lakini kwa majeshi lazima uende kozi ya muda flani ndo upande cheo. Lazima uhenyeke.
6. Ukiwa kwenye majeshi unakuwa tayari kufa ili mwenzako wabaki salama. Hiki ki kiapo kikubwa kushinda vyote katika maisha, ni kutokana na kiapo hicho tunaweza kiwafikiria kuwafutia deni hilo la HESLB.