HESLB na Serikali wawafutie madeni wapiganaji wote wa vyombo vya Ulinzi

MKEHA

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
713
1,136
Habari waungwana? Nimekuwa nikipita mitaani na kuongea na marafiki na jamaa zangu walioko serikalini, kwa kweli wanaumizwa sana na deni la HESLB.

Sheria inatoa mwanya kuchukuliwa kwa % 15 ya mishahara yao ghafi kulipia deni hilo la elimu ya juu. Sio mbaya sana kwani dawa ya deni ni kulipa. Lakini kwa wafanyakazi walioko kwenye vyombo vya ulinzi wangepata msamaha wa deni hilo. Nina sababu kadhaa za kwanini wasamehewe.

1. Deni la HESLB huwa linaleta stress kwa mtu akiwa analipa deni hilo. Mtu hukosa utulivu wa akili kila akiangalia salary slip yake hivyo kuwa na mawazo muda mwingi.

2. Vyombo vyetu vya ulinzi vina kazi ya ziada kuhalikisha tuko salama usiku na mchana, hivyo inakuwa kama zawadi kwa kazi hiyo mgumu sana ya kulinda raia, mali na mipaka ya nchi yetu.

3.Wanufaika wa HESLB waliopo kwenye vyombo hivyo sio wengi sana kiasi kwamba serikali itapoteza fedha nyingi.

4. Kama kwenye huduma zingine za umma huwa vyombo vyetu hupewa kipaumbele kama vile kwenye usafiri, mabenki kwanini hapa serikali isifumbe macho.

5. Kwa watumishi wengine kupanda cheo ni baada ya muda flani ukifika unapenda cheo kwa kujaza OPRAS, lakini kwa majeshi lazima uende kozi ya muda flani ndo upande cheo. Lazima uhenyeke.

6. Ukiwa kwenye majeshi unakuwa tayari kufa ili mwenzako wabaki salama. Hiki ki kiapo kikubwa kushinda vyote katika maisha, ni kutokana na kiapo hicho tunaweza kiwafikiria kuwafutia deni hilo la HESLB.
 
kama ishu ni kudaiwa mkopo,

Mbona wengi tu (hao watu wa Vyombo vya ulinzi na usalama) wana mikopo kwenye mabenki na wanalipwa tu kupitia makato kwenye mishahara yao?

Pia hiyo kazi si waliomba wenyewe na pia wanalipwa mishahara.

Kuna hoja nyingine ni za kipumbavu sana
 
Habari waungwana? Nimekuwa nikipita mitaani na kuongea na marafiki na jamaa zangu walioko serikalini, kwa kweli wanaumizwa sana na deni la HESLB.
Sheria inatoa mwanya kuchukuliwa kwa % 15 ya mishahara yao ghafi kulipia deni hilo la elimu ya juu...
Kwahio kwakuwa wewe ni poti au mjomba wako ni afande ndio unashauri utumbo huo! Lipa deni acha uzwazwa aisee,,,zile za kubrashia viatu mnazochukua kwa kutubambikia makosa barabarani mjue nasie zinatuuma kama hilo deni
 
Hawa jamaa wanapenda kitonga.

Kila kitu wanataka bure nguo mnapewa, mnapata posho ya chakula,mnalipwa hela ya nyumba,mabasi mnapanda bure bado mtaani mnakopa kopa na bia mnaomba omba.

Wapiganaji msipende bure bure,bure aghali. Ndiyo maana mkistaafu mnapata shida sana mtaani
 
Kila mtumishi/mnufaika wa mkopo wa Elimu ya Juu ana umuhimu kwenye Ujenzi wa Taifa hili. Ukitaka kujua hili angalia Waalimu, Madaktari, Wahandisi, Wanasheria, Marubani, Waongoza Meli n.k

Kwahiyo suala la Marejesho ya Mkopo wa Bodi linamtatiza kila Mtu, ndiyo maana wote waliosoma na kuhitimu kabla ya 1994 walisomeshwa bure. Ndiyo yaani Bure kabisa tena wakipata kila hitaji kwa gharama za Serikali.

Ajabu yake, baada ya wao kuhitimu na kuingia kwenye nafasi kadhaa za maamuzi na uongozi ndiyo waka impose hizo gharama eti kuwa ni mkopo na kila mnufaika wa baada ya 1994 anatakiwa kuanza kulipa.

Binfasi ningedhani bora hayo marejesho yangebaki 8% badala hii ya 15% waliyoimpose miaka 5 iliyopita
 
Mwisho wa nchi hii kupigana vita ilikuwa lini? Au wasamehewe kutokana na kufanya mazoezi huko vikosini?
Habari waungwana? Nimekuwa nikipita mitaani na kuongea na marafiki na jamaa zangu walioko serikalini, kwa kweli wanaumizwa sana na deni la HESLB.

Sheria inatoa mwanya kuchukuliwa kwa % 15 ya mishahara yao ghafi kulipia deni hilo la elimu ya juu. Sio mbaya sana kwani dawa ya deni ni kulipa. Lakini kwa wafanyakazi walioko kwenye vyombo vya ulinzi wangepata msamaha wa deni hilo. Nina sababu kadhaa za kwanini wasamehewe.

1. Deni la HESLB huwa linaleta stress kwa mtu akiwa analipa deni hilo. Mtu hukosa utulivu wa akili kila akiangalia salary slip yake hivyo kuwa na mawazo muda mwingi.

2. Vyombo vyetu vya ulinzi vina kazi ya ziada kuhalikisha tuko salama usiku na mchana, hivyo inakuwa kama zawadi kwa kazi hiyo mgumu sana ya kulinda raia, mali na mipaka ya nchi yetu.

3.Wanufaika wa HESLB waliopo kwenye vyombo hivyo sio wengi sana kiasi kwamba serikali itapoteza fedha nyingi.

4. Kama kwenye huduma zingine za umma huwa vyombo vyetu hupewa kipaumbele kama vile kwenye usafiri, mabenki kwanini hapa serikali isifumbe macho.

5. Kwa watumishi wengine kupanda cheo ni baada ya muda flani ukifika unapenda cheo kwa kujaza OPRAS, lakini kwa majeshi lazima uende kozi ya muda flani ndo upande cheo. Lazima uhenyeke.

6. Ukiwa kwenye majeshi unakuwa tayari kufa ili mwenzako wabaki salama. Hiki ki kiapo kikubwa kushinda vyote katika maisha, ni kutokana na kiapo hicho tunaweza kiwafikiria kuwafutia deni hilo la HESLB.
 
Dawa ya Deni ni kulipa tu acha ku create inequality kwa bodi ya mikopo vyombo vya ulinzi na wenyewe ni watanzania walipe tu

Upuuzi tu, ni sawa na hao wabunge, majaji, mawaziri yaani wao wanajiona hawatakiwi kulipa kodi, ila raia masikini ndio walipe kodi.
 
Wapuuzi hawa, ni sawa na hao wabunge, majaji, mawaziri yaani wao wanajiona hawatakiwi kulipa kodi, ila raia masikini ndio walipe kodi.
Eti vyombo vya ulinzi wasilipe wao ni nani kila mtanzania alipe Kodi I wonder ma judge, wabunge kwanini haiwalipi Kodi kwa kujiona wao ni exceptional huku wauza nyanya na vitunguu wenye uchumi mdogo usiofika 5000 kwa siku wakilipa
 
Kama umeona Mbunge aliyependekeza Wabunge walipe kodi walivyomrukia, huu mfumo wetu kodi ni wa kibaguzi. Halafu anakuja mtu anasema eti tulipe kodi ya kizalendo, wakati yeye halipi.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom