HESLB mnataka tufe kwa pressure?

Serikali inabidi iangalie upya utaratibu wa kulipa Deni la HESLB kwani linawaumiza watumishi asilimia ni kubwa Sana toka 7% mpka 15% ni kubwa na ukiangalia viwango vya Mishahara na riba ambazo watu wanawekewa na HESLB.ni kubwa Sana.
 
Ukifika pale unajibiwa mavi,mtu kaegemea kwenye kiti kama yupo chumbani kwake,hela imeenda na unajibiwa upupu.
Wahitaji maskini na yatima wananyimwa na wanaoingia vyuoni wanaendesha mashangingi wamekopeshwa. Hao hawaajiriwi wengi wanajiajiri. Wakiona makusanyo ni kidogo wanaanza kupagawa wanapandisha asilimia.
Anayewadhulumu na kuwanyanyasa yatima,maskini na wanyonge huyo atapambana na nguvu ya Mungu. Tena akizidi ubishi Mungu anamtuliza kwa kuchukuatu Oxygen yake
Bodi yenyewe ni Chaka la unyonyaji tu...
 
Mimi ni mnufaika wa Bodi ya mikopo ya Elimu ya juu (HESLB). Nilianza kulipa deni langu la shilingi milioni 6.5 mwaka wangu wa pili tu baada ya kuajiliwa.

Nililipa deni langu katika kipindi cha miaka nane. Nimeshtushwa na barua niliyoandikiwa ofisini kwamba nina deni HESLB.

Nimemaliza deni langu na huu ni mwaka wa pili sasa. Naomba kujua Bodi ya mikopo hili deni wamelitoa wapi wakati katika salary slip zangu zinaonyesha ushahidi wa kukatwa pesa kuanzia mara ya kwanza mpaka nalimaliza miaka miwili imepita sasa.

Hivi kwa mshahara kweli ( take home) nitaweza kuendesha Maisha au ndio utakuwa mwanzo wa depression na hata kupoteza Maisha? SERIKALI NAOMBA MULIANGALIE HILI NAJUA SIO KWANGU HATA KWA WENGINE WAMEKUTANA NALO. SISI NI WANYONGE .

View attachment 1766800
Nimewapenda sanaaaa hawa CWT
Screenshot_20210501-125530.jpg
 
Usichojua kuhusu hao loan board wao wanaile 6% rentation fee kila mwaka inaongeza kutoka kwenye Deni liliobaki kwa kila mwaka.

hivyo Kama ulimaliza Deni kuanzia siku uliyomaliza Deni ulitakiwa kuwafata hao loan board wakupe statement kuonyesha Hali ya mkopo wako kwakua lazima bado utakua tu na Deni kwani hiyo rentation fee itakuepo tu.

Kwani ilipoanza kuonekana kwenye salary slip yako lilikua Deni lililokuwako wakati ule unaanza- kulipa maana yake rentation fee iliendeleza kujizalisha kila mwaka.

Anyway tukiwaambia hili Deni halilipiki muwe munaelewa
Kwa maana hiyo 6% ambayo ndio retention fee, imefutwa rasimi kuanzia leo baada ya hotuba ya Mhe. Rais? Na itafanyika recalculation upya ??
 
Back
Top Bottom