HESLB kutoa muda mrefu wa siku 90 kukata rufaa, Inawatakia wanafunzi mema kweli?

msuya4real

Member
Oct 14, 2016
76
27
Kuna jambo najiuliza tu hivi bodi ya mikopo iko sahihi inapotangaza siku 90 za kukata rufaa kwa wanafunzi wote waliokosa mikopo, hivi kwa hali ya kawaida tu hizo siku 90 mwanafunz ataishije chuoni, huku pia hajui kuwa atafanikiwa kupata au laaaa!

Bora wawaambie watu watafute means nyingine maana cha kupata hapo ni ndoto kwa kweli, vijana wengi naona wanarudi nyumbani baada ya kuona hali sio nzuri kabisa ya kiuchumi ni hayo tyuuuuuuuuu wapendwa wa JF
 
Dili kubeti tuu hakikisha Simu yako Ina app ya meridian, m -bet na unasave bookmark mkekabet.com hawa jamaa wapo vizuri sana pesa haichelewi, haina masharti, haina dodoso wala priority
 
Ila mi najiulza nakosa jibu wamesema bajeti yao ndipo ilipo fikia kimono sasa mtu aki appeal hizo hela za kumpa zitatoka wapi? Mi nazan tunaongozwa na v!ongzi v!laza
 
Siku 90 ni semester nzima-kama kweli huna njia nyengine ya kulipa ada na kujikimu-utakuwa umefutwa chuo hakuna senate itakayo kuruhusu kuendelea kuwa mwanafunzi labda uahirishe masomo hadi mwakani. La pili kipi kimebadilika hadi uwe na tegemeo ya kupata mkopo kama umekosa hadi sasa. Sana sana kama serikali haikuongeza dau-si zaidi ya vijana takribani 4500 kati ya 30000 ambao wanaweza kupewa huo mkopo awamu hii. Ceiling imewekwa 25000 kama sikosei. Wale wenye kauwezo itabidi kufunga mkanda na kugharamia vijana (miradi mingine isimame).
 
Ni sawa na daktari kumpangia appointment mgonjwa aje baada ya miezi mitatu huku akijua kuwa kwa hali yake hawezi kufikisha hata mwezi mmoja!
 
Back
Top Bottom