HESLB kukata 15% ktk Mishahara ya wanufaika: Sheria haiwezi kutumika retrospectively

Sisi tulio soma miaka ya 1994 hakukuwa na mkopo
Ilikuwa unasoma bure enzi za Mzee Mwinyi
Mm hadi leo sijapata barua yao na wala jina halipo
Nasubiri kwa hamu sana hiyo barua yao ya kipuuzi
Kama wameshindwa kubuni vyanzo vipya vya mapato watuondokee madarakani
Hakukuwa na mkopo, mimi nilimaliza 2003 na sikuwahi kuambiwa kama nasomewshwa kwa mkopo. Wala sheria ya bodi ilikuwa bado kutungwa. na wala bodi ilikuwa haipo
 
Hakukuwa na mkopo, mimi nilimaliza 2003 na sikuwahi kuambiwa kama nasomewshwa kwa mkopo. Wala sheria ya bodi ilikuwa bado kutungwa. na wala bodi ilikuwa haipo
Sasa kutuletea barua kama tunadiwa sisi wa mwaka 1994 nguvu hiyo wanapata wapi?
Wanasheri home TZ wanasemaje?
 
Sasa kutuletea barua kama tunadiwa sisi wa mwaka 1994 nguvu hiyo wanapata wapi?
Wanasheri home TZ wanasemaje?

Naona wako kimya, labda wanasubiri bodi ianze kuwashitaki watu. Na katika mahakama hawawezi kusikiliza kesi kama hawana original documents yaani mkataba original oliosainiwa kati ya mdaiwa na bodi. Kama hawakuwahi kusign mkataba na watu wa miaka hiyo hawataweza kuwashitaki kwani hakukuwa na mkatataba baina ya watu hao na bodi.
 
Naona wako kimya, labda wanasubiri bodi ianze kuwashitaki watu. Na katika mahakama hawawezi kusikiliza kesi kama hawana original documents yaani mkataba original oliosainiwa kati ya mdaiwa na bodi. Kama hawakuwahi kusign mkataba na watu wa miaka hiyo hawataweza kuwashitaki kwani hakukuwa na mkatataba baina ya watu hao na bodi.
Hawana CONTRACT OF ADHESION hata moja
Nahisi msemo wao kama WOTE TUISHI KAMA SHETANI wanataka kuhamishia kwetu
Wakati wa Mzee Mwinyi nafasi za chuo hazikuwa nyingi kama leo
Kwenda UDSM au IFM au Mzumbe ilibidi form Six ufanye vyema
Walituchagua bila hata mkataba kama ipo siku tutalipa
Hatulipi ng'oo!
 
Tuchukulie mtu ana mkopo, mikopo mingine kabla ya hii sheria, na kuna sheria ya HR inayohusu kiwango ambacho mfanyakazi anaweza kukatwa mshahara wake kulipia mikopo, itakuwaje kama itazidi kiwango hicho?
Dah! Mi ntabaki na elfu40 kwa mwezi...
 
Wanasiasa wote wanafanana na tofauti Yao ni uwezo na umahiri wao kwny kudanganya tu.

Mkuu nafurahi sikuhizi michango yako mingi ina balance haipo kiukada sana kama zamani, yaani ingekuwa zamani hapo povu zito lingekutoka kwa Lowasa au kuhusu wadaiwa wa loan board.

Hongera sana!
 
Sheria ya Mikopo kwa wanafunzi ilitungwa 2005 lakini ilipiga reverse ( retrospective)mpaka 1994 na watu wakalipa Madeni.
'Atakaejaribu kutukwamisha tutambomoa'- Bosi wake Paul Makonda
Mkuu, kwa hilo naweza kuwaelewa Loan Board hasa kwa kuanzia miaka hiyo ya 1995. Sababu kubwa inayowalinda Loan Boaed hapo ni ile Sheria ya Education Cost Sharing ambayo ilipitishwa miaka hiyo na hivyo kufanya nao walipe tu. Issue ambayo inatia shaka ni kuongeza kutoka mikataba iliyoridhiwa na pande mbili na kuweka hadi 15%, wajuzi wa sheria watufafanulie hilo. Yaani mtu ulikopa benki kwa riba 20%, then kutoka kusikojulikana unaambiwa riba itakua 30% huo ndiyo mfano wa hicho kinachotaka kufanyika. Au Loan Board iuleze umma hiyo 15 % repayment ni kwa wanufaika wa kuanzia mwaka gani, na je wale ambao tayari wanakatwa 10% inawahusu nini hiyo 15%
 
Ulimwenguni popote pale hakuna sheria yoyote inayotungwa halafu ikawa applied retrospectively. Sheria zote mpya zinazotungwa zinakuwa applied prospectively.

Maana yake ni kwamba wale wafaidika wa bodi ya mikopo waliokopa mikopo wakati sheria inasema makato ni 8%. Basi wanatakiwa kuendelea kukatwa 8% katika mishahara yao.

Ila wanafunzi wapya ambao watakopa wakati sheria imebadilishwa na kuwa makato ni 15% ya mishahara yao, basi hao ndio wanatakiwa kukatwa 15% katika mishahara yao.

Nitashangaa sana WASOMI wetu waliosoma wakati sheria inasema kwamba makato ni 8% ya mshahara wao, kama watakubali kukatwa katika mishahara yao 15% (retrospectively). Nitawadharau sana na kuona nchi hii inafundisha UJINGA vyuoni.

For the food of thought. Nyerere aliwahi kuwakamata wahujumu uchumi. Baada ya kuwakamata akapeleka bungeni mswaada wa uhujumu uchumi ukapita na kuwa sheria. Watuhumiwa hao wakafungwa kwa sheria hiyo (retrospectively).

Lakini hao watuhumiwa wa uhujumu uchumi walikata rufaa, kwa misingi hiyo kwamba hawawezi kuhukumiwa kwa sheria ambayo haikuwepo wakati walipotenda kosa (retrospectively), walishinda wote kesi zao na kuachiwa huru.

Inaonekana tangu wakati wa Nyerere bado serikali haijajifunza kwamba sheria hazi apply retrospectively. Wasomi amkeni nendeni mka challenge huo uamuzi mahakamani, mtakuwa mme set good president kwa utawala wa sheria kama walivyofanya watuhumiwa wa uhujumu uchumi.

The ball is in your court WASOMI.
Wazo zuri sana,ila makato bado hayajaanza ina maana hata mtu akienda mahakaman leo hana vielelezo,
 
Kiukweli wanasheria inabidi wasimamie jambo hili vizuri maana hali itakuwa mbaya endapo serikali itamua chukua hiyo 15%
 
Hivi umeelewa alichoandika mtoa mada au umekurupika huko na ushabiki wako kuja kubisha tu.
Mtoa mada hakusema watu wasilipe, lakini wale ambao waliingia mkataba wa repayment ya 8% hawez kulipa 15% kwa sababu yeye hakukubaliana na makato ya asilimia hizo. Ila pia atatakiwa kulipa penalty ambazo alikubali kwa wakati anachukua mkopo kwa uzembe wa kutolipa deni kwa wakati.
Usihangaike na huyu jamaa na wenzake. Wameshikiwa akili zao na CCM kwa kiasi cha kuwa mataahira kabisa. Endelea kumsoma tu utaamini maneno yangu
 
Kama kungekuwa na room hiyo ambapo sheria ilisema kwamba mnufaika atakatwa kati ya 5-20 % basi serikali isingesumbuka tena kupeleka mswaada bungeni wa kubadilisha sheria kutoka 8% kwenda 15 %. Kama ingekuwa hivyo waziri mwenye dhamana angetangaza kwenye gazzetti la serikali na sheria ingebadilika na kuwa 15 %.

Lakini kwakuwa hakukuwa na room hiyo ndiyo maana serikali ilipeleka mswaada bungeni wa kubadilisha makato kutoka 8% kuwa 15%.


Na hapa ndipo hoja yangu inapokuja kwamba wale waliokopa wakati sheria ni 8% wanasitahili kisheria kuendelea kukatwa ktk mshahara yao 8%. Ila kwa wale wanafunzi wapya watakaokopa wakati sheria imebadilishwa na kuwa 15% ndio wanatakiwa kukatwa 15 %.

Kuwakata wakopaji wa zamani 15 % is null and void because sheria huwa hazifanyi kazi retrospectively. That's is the rule of the thumb and that decision can be challenged before the court of laws.
Inaonekana unaijua sheria MKUU,naomba nikuombe ....!!! Kama ni mwanasheria ( wakiri) pitisha mchango ili kesi ifunguliwe alafu wahanga tuchangie.
Huu ni ubabe na dhuruma kwa wafanya kazi, Increments zimesitishwa,watu hawapandi madaraja zaidi ya miaka 6/8 , makato kibao ....!!! Leo hii mtu anasaini sheria kandamizi kama hii kwa maslahi ya nani???? ,kama sio kuwakomoa watumishi.
Naichukia nchi yangu hadi kichefuchefu kwa sababu ya ubabe wa wachache usio na tija.
 
Sie wadaiwa sugu tunawasubiria watupeleke mahakamani kwanza tupige hela. Wengine hatujawahi hata jaza form ya mkopo halafu tunaambiwa tunadaiwa Na tupo kwenye list ya wadaiwa sugu.
 
Sasa kutuletea barua kama tunadiwa sisi wa mwaka 1994 nguvu hiyo wanapata wapi?
Wanasheri home TZ wanasemaje?
Mkuu, nyinyi munaingia katika ile sheria ya mwaka 1995 kama sikosei ya Cost Sharing. Hapo sheria hiyo inawahusu. Ila utata ni kwa wale waliosommeshwa na Loan Board kwa kusaini repayment ya 8 au %, dhidi ya maboresho ya sasa na kufika 15%, hapo wataalam wa sheria ndiyo wasaidie kufafanua kisheria, inawezekana mkopaji wakati yuko analipa deni kuongezewa riba, sheria inasemaje, inaruhusu au ni Null and Void? Lakini tukichukulia nyie wa zamani ambao hamkukopa kabisa japo munabanwa na Cost Sharing, mutalipa kwa kiwango cha asilimia ngapi? 8,10 au 15%Je kwa nini iwe ni 15 au iwe 10 au 8%,vigezo gani vitatumika kufikia Win Win Situation?

Yote kwa yote, beneficiaries wa kusomeahwa LAZIMA walipe deni, lakini Asilimia iangaliwe upya kwani wananchi wana maisha magumu sana. Ikiwa 15% kuna watu watabakiwa na chini ya 100,000 kama take home.
 
Nikiangalia kwa mtazamo mpana shida sio kulipa haya madeni kwa hawa wahitimu, SHIDA NI NGUVU INAYOTUMIKA NA USAWA KATIKA KUSHUGHILIKIA MATATIZO, IKUMBUKWE HAWA VIJANA WALIKOPA NA HAWAKUIIBIA SERIKALI NA BADO ZAIDI YA 40% UTAKUTA WANALIPA KODI. NGUVU HII PIA SERIKALI INGETUMIA KWA WEZI WA MALI ZA UMMA NA WATU WALIOFILISI SERIKALI NA WANAOENDELEA KUIFILISI mfano EPA, ESCROW, RADAR, NDEGE YA RAIS, MEREMETA,DEEP GREET, WIZI BOT, WIZI KWENYE HALMASHAURI ZETU, WIZARANI HUKO NK..
 
Hivi umeelewa alichoandika mtoa mada au umekurupika huko na ushabiki wako kuja kubisha tu.
Mtoa mada hakusema watu wasilipe, lakini wale ambao waliingia mkataba wa repayment ya 8% hawez kulipa 15% kwa sababu yeye hakukubaliana na makato ya asilimia hizo. Ila pia atatakiwa kulipa penalty ambazo alikubali kwa wakati anachukua mkopo kwa uzembe wa kutolipa deni kwa wakati.
Achana nae huyo anachojuaa ni kusifia hta vitu visivyosifikaaaa. Tunachoangalia hapo ni mkataba wa mkopo mtu aliosign na kuingia makubaliano. Kama ni 8% kwann akatwe 15%?
Shda wanahaha coz wanaorudisha mikopo ni walim na wengi wanaopewa mikopo n wanaosomea ualim. Soo zaid ya wahitim laki 4 wa mwaka jana na mwaka huu wote wapo kitaa na kati ya hao laki mbil na nusu ni walim ambao wangeajiliwa wangekua ndo wanarudish mikopo waliyosomea. So ili kukompasate loss ya hao inabid wapandish % ya makato ili iwe balanced na sheria ya 8% inabadilishwa jan ili iwe15%
 
nawashangaa akina ben saa nane kwa kutafta kick kwa kujiteka wakati kuna mambo ya msingi kama haya... hii kesi ilipaswa kuwa mahakamani kitambo.

haya ndio mambo ya msingi kuyaweka sawa....
 
Tuchukulie mtu ana mkopo, mikopo mingine kabla ya hii sheria, na kuna sheria ya HR inayohusu kiwango ambacho mfanyakazi anaweza kukatwa mshahara wake kulipia mikopo, itakuwaje kama itazidi kiwango hicho?

Wenzetu serikalini hawana sheria za hr na kwao hr does not exist nna nina wahurumia sana hr serikalini - maana huku kutumbuliwa kungefata hr procedures wote mgeshangaa ambayo yangetokea. Wao wanajua wenyewe wanachofanya ila watu wa labor wakienda private wanakomaa kuangalia km sheria za kazi znafatwa ila kwao ni bure kabisa,hakuna anayesimama kutoa mwongozo wala kukemea haki za wafanyakazi wa umma kuvunjwa - eti katumbuliwa sijui anapangiwa kazi nyingine,sijui mishahara inapunguzwa cjui kasimamishwa - yaani ni shida
 
Back
Top Bottom