HESLB acheni kuzingua, kwanini hamtatui tatizo langu? mnasema mnalifanyia kazi zaidi ya masaa 4?

Vitamin K

Senior Member
Dec 2, 2017
158
168
Nimelipia Application fee halafu mfumo wenu unasema bado sijalipa na kuonesha control namba hiyo hiyo niliyoitumia kulipia.

Nimewasilisha tatizo langu kwenu mnasema mnalifanyia kazi tangu saa 7 mchana hadi muda huu bado hamjamaliza, kweli?

Kesho ndio mwisho wa kutuma maombi, kwa nini mnataka kunikwamisha kutokana na mfumo wenu? Mtanilipa hela yangu baada ya kufunga dirisha la maombi?

HESLB acheni ukanjanja...
 
Kama mumeshindwa kazi achieni wengine, nyie muendelee na siasa
Siasa ndio iliweka kitu kinaitwa HESLB,siasa ndio ikaamua nani apate Nani akose,siasa ndio ikaamua ukatwe 15% ya salary kulipa deni na siasa ndio ikamteua mkuu wa HESLB ambaye nae anaajiri wa chini yake unaowalalamikia.Kwa hiyo rafiki Kama Unafikiri maisha yako yako nje ya siasa nakushauri ujinyonge mapema usiwe ktk dunia hii
Lakini habari mbaya ni kwamba hata ukifa bado siasa haitakuacha, itaamua ikuite mtakatifu au dikteta,mzalendo au muasi nk
 
Mbona ulichelewa sana ulikuwa wapi. Mimi niliomba wiki ya kwanza kama sikosei.
Nilipata matatizo ya kiafya ambayo yalinifanya niweze kuchelewa.

Lakini tangu jana isingekuwa mfumo wao huu mbaya ningekuwa nishamaliza.

Nimewauliza wanirekebishie niweze kuendelea na application wanadai mtandao unasumbua.

Huo mtandao unatoa control namba papo hapo ila ukilipia, unaanza kutoa notification kuwa bado sijalipia na unaendelea kudisplay control namba hiyo hiyo niliyoitumia. Iweje mfumo utoe control namba haraka lakini ugome kuendelea baada ya kulipia?

Ole wao wanikwamishe, watanirudishia hela yangu maana nimelipia ndani ya muda ila kutokana na usumbufu wa ubovu wa mtandao wao, ndio inaleta matatizo kama haya.

Hadi muda huu mfumo wao bado unagoma, ngoja pakuche patachimbika huko kwenye ghorofa lao.
 
kuchelewa kwako sisi kama bodi hautuusu, tunaomba uwe mvumilivu na usubili kufanya application mwakani mapema, tunakutakia asubuhi njema, karibu kwa huduma nyingine
 
Bwana mdogo una hasira sana, sijui ni ugumu wa maisha au vipi. BTW, vumilia wataongeza muda.
Mmmh, kama dirisha hili linalofungwa leo ni la kuongeza mda unadhani wataingeza tena... Alafu vyuo vishaanza kufanya kuruhusu application.. Labda kutoa majina kwa waliokosea
 
Back
Top Bottom