Heshima ya nchi yetu imeharibiwa na kundi dogo lisiloguswa na yeyote hapa Tanzania. Nini kifanyike? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Heshima ya nchi yetu imeharibiwa na kundi dogo lisiloguswa na yeyote hapa Tanzania. Nini kifanyike?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mlalila, Aug 16, 2012.

 1. M

  Mlalila Member

  #1
  Aug 16, 2012
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Baada ya kufikiria na kupima mwelekeo wa nchi yetu tulikotoka, tulipo, na tunakokwenda; tusipotafakari vyema nchi hii itakuwa na historia nzuri sana na mbaya sana. Nikakumbuka "heri mwisho wa jambo kuliko mwanzo wake".

  Tulianza vizuri ktk nchi yetu, tulikula na kulima pamoja, tukasoma pamoja, tukawa na maduka ya pamoja tukahifadhi mali ya umma pamoja.Leo hii chini ya chama kile kile (TANU/CCM) nchi na uzuri wake unaliwa na kikundi kidogo sana kisichoogopa chochote na kinafanya lolote ndani ya nchi hii. Baadhi ya wazalendo wakipiga kelele wanazimwa kwa namna moja au nyingine. Hakuna yeyote mwenye kusema tuache kuwaibia waTZ isipokuwa wale waliokuwa nje ya CCM nako wachache tu!!!!! kwa kuwa wengine ni mapandikizi.

  tufanye nini????.

  Dawa ni moja tu, hiyo ndiyo pekee itakayotupa nchi yenye neema kama tulivoanza mwanzo.Huduma zetu zitaboreshwa na pia watoto wetu watasoma.

  Kila mtu nayependa kuona nchi yetu inasonga mbele, basi ahakikishe mwaka 2015. CHADEMA inaingia magogoni na sio kwamba wakae pale milele. wakipoteza mwelekeo kama CCM, tunawapeleka NCCR-mgeuze.


  CHADEMA !!!!!!!!!!!>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>2015>>>>>>>>>>>>>2020>>>>>>2025.......?????????
   
 2. m

  majebere JF-Expert Member

  #2
  Aug 16, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,520
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 280
  CDM wapewe kwa sababu gani? Kwanini sio vyama vingine? Nyie bora mpambane na CCM tu wajirekebishe kwa sababu ndio wao ndio watachukua 2015. Kingine unacho weza kufanya ni kuhama nchi.wabeba mabox bado wanahitajika majuu.
   
 3. Hossam

  Hossam JF-Expert Member

  #3
  Aug 16, 2012
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 2,363
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mkuu Majebere,

  Nasikitika na napata tabu kuufahamu uzalendo wako. Mtoa mada kapapasa surface tu na simuungi mkono kiivyo kwa kuwa hajajadili mawazo yake kwa hoja maridhawa ama hajaweka ushahidi wowote. Katika siasa za Tanzania maneno kama ya mtoa mada yapo hata vijiweni na sio kila usemalo unaweza kulithibitisha pasipo shaka.

  Zamu yako sasa. Huwezi kuwa bubu wa akili ukaweza tu kuandika mawazo yako pasipo kuishirikisha akili kwa kuwa naamini mawazo pekee sio akili. Fungua macho mkuu ukatoe tongotongo la ushabiki na usimamie haki na ukweli, jitahidi kukwepa ukada na kamwe usitoe mchango kwa ufedhuli ili kupalilia hoja mfu kwa wenye msimamo kama mshumaa kwenye tufani.

  Nchi hii kumbuka inakuhitaji na wewe katika ukombozi wake na hasa ukombozi wa kifikra na kuepuka kuishi kwa historia. Ulaya na nchi nyingine kama hizo wataendelea kutawala wenye mawazo mgando na hata ukiamua kutimkia kwao utaishia kuwa mhamiaji haramu ma zaidi mlezi wa wazee ukizoa mavi na kuwanawisha wasiojiweza.

  Ila kama wewe sio Mtanzania, ima kama huguswi na ungumbalu wa nchi hii, futa yote uliyosoma hapa. Sio ishu.
   
 4. G

  Gwakisa Mwandule JF-Expert Member

  #4
  Aug 16, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 520
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Subiri utakapo mmeanza kunywea maji kwenye makarai ndo utajua kumbe m4c imeizima kambi yako ya wauza nchi!Mara utakapoona chukizo la uharibifu likisimama mahali pasipolisa ndipo walio katika uyahudi na wakimbilie milimani,aliyeshambani asirudi nyumbani waala aliye darini asishuke maana patakuwepo dhiki isiyopata kutokea na haitatokea tena....Ukiona Ccm wanaanza kuwa wapinzani.......Nadhani wewe husomi alama za nyakati utakumbwa na sunami ya m4c.Gamba wewe!Wanyaama wenyewe wanaelewa M4C inavyotisha sembuse wewe mlamba viatu vya magamba
   
 5. mito

  mito JF-Expert Member

  #5
  Aug 16, 2012
  Joined: Jun 20, 2011
  Messages: 7,613
  Likes Received: 1,993
  Trophy Points: 280
  Mkuu cha kufanya ni kutengeneza katiba nzuri kwanza! Hata hao chadema wakiingia katiba ikiwa mbovu ni madudu tupu! Katiba ndo inaongoza nchi, si maneno wasemayo wanasiasa majukwaani
   
 6. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #6
  Aug 16, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Alieweka utaratibu wa BAN ashukuriwe sana na baadhi ya watu!
   
 7. M

  Mlalila Member

  #7
  Aug 16, 2012
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tatitizo siyo katiba bali ni dhamira za watawala wetu. Unafikir ktk katiba kuna kipengele cha kuficha mabilion nje ya nchi?. Au ktk katiba kuna kipengele cha kuuza maliasili yetu Mfano Twiga!!!!!!?. Tusipobadilika na kuwapiga chini watauza mpaka kuku wetu majumbani mwet hawa jamaa si wema hata kidogo!!!!!!!.

  Navotambua bila CDM Tanzania tungekuwa wote waramba viatu vya mafisadi. CDM wakitinga Ikulu Katiba faster itatungwa, na wakisubr chadema wafike Ikuru ndo katiba itungwe basi kuna watu watakimbiria ughaibuni!!!!!!!
   
 8. d

  danizzo JF-Expert Member

  #8
  Aug 16, 2012
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 279
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mi nadhani ni tuwe na sheria kaki kwa viongozi kama vifungo vya maisha na kifo kwa mafisadi. Sio cdm sio cuf sio nccr watakao wezesha nchi yetu iludi ktk fom . Wabunge wanaweza kuleta mabadiliko makubwa ktk nchi hii ila nao wamepoteza dira. Ila habari ya chama flan sijui nini hapana tutabadiri sura tu michongo yao ile ile siasa
   
 9. mito

  mito JF-Expert Member

  #9
  Aug 16, 2012
  Joined: Jun 20, 2011
  Messages: 7,613
  Likes Received: 1,993
  Trophy Points: 280
  Mkuu dhamira ni namba mbili after katiba. Dhamira ya binadamu ni uovu tangu kuzaliwa kwake. Hali hii inathibitiwa na sheria tu (ambazo hutokana na sheria mama - katiba). Short of that tunacheza makida!

  Nakubaliana na wewe 100% kuwa katiba haina kipengele kinachoruhusu hayo mambo kwa red. Lakini kumbuka ni katiba hiyo hiyo ndo inamkingia kifua mtu atayefanya hivyo vitendo, na hapa ndipo hoja yangu ilipo. Hivi unajua tunapiga kelele tu lakini mtu kama BWM pamoja na madudu yote aliyofanya huwezi kufanya lo lote mbele ya sheria kwa sababu analindwa na katiba ya sasa?
   
 10. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #10
  Aug 16, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
Loading...