Heshima ya Kinana imeshuka sana! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Heshima ya Kinana imeshuka sana!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Akiri, Sep 29, 2010.

 1. A

  Akiri JF-Expert Member

  #1
  Sep 29, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,447
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Najiuliza maswali sipati majibu wadau nisaidieni eti huyu Kinana ndiyo yule alikuwa mbunge wa Afrika mashariki pia akachaguliwa kuwa spika wa bunge hilo, hivi huyu ndiyo yule au huyu ni mdogo wake?

  najiuliza maswali hayo sababu kinana wa wakati ule alikuwa ni Mtu makini kabisa na pia alikuwa ni mtu mwenye heshima zake. huyu ninayemsikiliza na kumuona ananitia mashaka makubwa. Kwa mfano:

  • Kinana wa sasa hivi anatetea matumizi ya Salma na kuyaita ni matamizi ya kawaida eti huyu mama anakisaidia chama. kinana unaweza ukanifafanulia zaidi kwamba huyu mama ndiyo mwenye huo uwezo peke yake na hakuna mwanachama mwingine. na huyo mwingine angekuwepo angeruhusiwa kutumia 22,000,000 ndani ya masaa matano tu. na mtu mzima kama wewe ukawa unachekelea na kuita ni matumizi ya kawaida kabisa ?

  • Kinana wa sasa hivi anaghushi risiti na kuudanganya uma wa watanzania rejea gazeti la mwanahasili wiki iliyopita tarehe 22/09/2010 risiti alizotuonesha ni za vitabu vilivyotumika tayari mwaka 2006 na kwa sasa vimefungwa.
  kama sio kweli mbona sijakusikia ukikanusha wala waziri wako wa michezo sijui akidai atalifungia gazeti mbona kimya ? yaani mmegushi na bado mnataka tuwape madaraka???

  • Kinana wa sasa hivi amakuwa mtetezi wa ufisadi na kila baya linalotendwa na familia hii inayogombea kuingia ikulu kuendeleza sherehe zisizo na kikomo kinana ndiye mtetezi. haya na hizo helicopter mbili kati ya hizo tunasikia mmepewa na mafisadi kwa mujibu wa marando.
  Mzee Kinana leo umekuwa mtu wa kulishwa maneno na watu wanaokulisha hayo maneno ni ni akina yusuph nk

  Mzee Kinana tafuta busara za mzee warioba, Dr. Salim.

  Yaani mzee Kinana umeporomoka kutoka spika wa bunge la afrika mashariki mpaka kuwa mpiga porojo wa ccm.

  Nimesikia baada ya kampeni umeahidiwa kupewa ubalozi.

  Nakushauri jiuzulu huo umeneja kampeni, kaa tunza heshima yako ili nawe uje uheshimiwe. Siku hizi unaniudhi mpaka nahisi wewe ni msomali
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Sep 29, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  kwani lini amewahi kuwa na heshima huyu!!! toka zamani za kale hana heshima yoyote ndo maana sioni kilichoshuka kwake
   
 3. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #3
  Sep 29, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Hana uchungu na nchii hii kwanza kao Somalia sasa tukianza kuzipiga apa sijui atakimbilia wapi?
  Ajifunze kuwa mzalendo
   
 4. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #4
  Sep 29, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  inawezekana asiwe na Heshima tangu mwanzo kama Kigogo alivosema, ila jambo moja uelewe, kumtetea Kikwete na kumpigia Debe lazima uwe kichaa kidogo, mvuta Baghi, mnafiki ama malaya wa kisiasa.
  inataka moyo kumpigia kampeni huyu jamaa, kweli hauziki.
   
 5. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #5
  Sep 29, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Kinana hakuwahi kuwa na heshima yoyote ... sana sana watu walikuwa wanamuogopa kwa sababu ya stori zilizoko mtaani kuwa jamaa ni trained killer (nyoka aka usalama wa taifa la mafisadi wa tanzania). Baadhi ya watu walikuwa wanaogopa kuwa wakipingana naye, watajikuta wako kwenye meza moja na hayati kolimba.

  Sasa hivi watu hawaogopi tena, na akifanya makosa alete ughaidi na uharamia wake kwenye uchaguzi wa mwaka huu, atagundua kuwa watanzania wa leo sio wa miaka ya 90....
   
 6. pascaldaudi

  pascaldaudi JF-Expert Member

  #6
  Sep 29, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 534
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Duh!!!!!!!!!, Kumbe!,,,,,....................................
   
 7. Drifter

  Drifter JF-Expert Member

  #7
  Sep 29, 2010
  Joined: Jan 4, 2010
  Messages: 1,968
  Likes Received: 669
  Trophy Points: 280
  Si suala la heshima. Wala hakuna haja ya kuwa na hasira au jazba na mtu binafsi kama Kinana. Yeyote anayechukua mzigo wa kuwatetea watawala wa wakati huu (the establishment) lazima atafanya kama hivyo. Hakuna namna nyingine. Kama ni hasira basi zielekezwe kwenye mfumo mzima tulioulea miaka nenda miaka rudi ya kushabikia watu badala ya utendaji makini Serikalini na katika vyama vya siasa.
   
 8. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #8
  Sep 30, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Kutetea matumizi ya pesa kubwa kiasi hicho zinazoweza kujenga darasa 1 ni aibu saana. naipenda ccm lakini kwa matendo yake ya sasa sipo pamoja nao, Hata kama ni pesa ya chama pesa hii wanayochangia walala hoi! jk nani anakushauli na mabango makubwa ya gharama kubwa kwanini? kutumia ghalama kubwa kwaajili ya kampeni?? kwa nini msitumie nguvu hiyohiyo kwa ajili ya kupata pesa ya kujengea shule na hospital?? HV CCM UWEZO WETU UMEISHIA HAPO!?
   
 9. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #9
  Sep 30, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Wakuu Kinana hajawahi kuwa na heshima hata siku moja sana sana heshima anayo labda kwa waarabu wa Loliondo na wezi wenzake huko CCM.
   
 10. Mpambalyoto

  Mpambalyoto JF-Expert Member

  #10
  Sep 30, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kinana yupi? Heshima ishuke leo? Kwani alikuwa nayo lini?
   
 11. kipipili

  kipipili JF-Expert Member

  #11
  Sep 30, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 1,499
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Kinana ni kenge tu
   
 12. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #12
  Sep 30, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Haoni watu wazima wenziwe watu safi walivyotulia kama maji ya mtungi? Yeye kiherehere cha nini cha kujiingiza kwenye tope kichwakichwa?
   
 13. Kudadeki

  Kudadeki JF-Expert Member

  #13
  Sep 30, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiyo ngazi ya kushushia heshima ulimtengenezea wewe? :tonguez:
   
 14. MANI

  MANI Platinum Member

  #14
  Sep 30, 2010
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,862
  Trophy Points: 280
  Drifter mbona wako wengi wamekaa pembeni? Wapi Salim Ahmed Salim,Mzee Mwinyi, Mkapa na wengineo nafikiri ni wakati muafaka watu wakapima heshima zao kabla ya kutumikia watu.
   
 15. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #15
  Sep 30, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  mkapa nafasi yake imechukuliwa na mtoto, Mwinyi nafasi yake imechukuliwa na Salma! Tulijua mambo yatakuwa rahisi!
   
 16. MartinDavid

  MartinDavid JF-Expert Member

  #16
  Sep 30, 2010
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 876
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Tangu lini alikuwa na heshima huyo ni mwizi tangu zamani!!!

  unakumbuka kashfa ya Mama Mwinyi??? pia kwa taarifa yenu huyu ndiye mwenyekiti wa wasomali tanzania.. hivyo hana maslahi yoyote na tanzania...

  2005 Meneja Mkuu wa kampeni alikuwa Lowasa = akapewa Uwaziri Mkuu
  2010 Meneja Mkuu wa kampeni ni Kinana = Uwaziri Mkuu, Uwaziri, Ubalozi au ???? Slaa hatampa hata umeneja wa choo cha pale Ubungo.....

  Nia tunayo, Uwezo tunao
  Chagua Slaa Kwa maendeleo ya Taifa

  Tanzania bila ya Fisadi Jk na Jangili CCM inawezekana.
   
 17. Mpeni sifa Yesu

  Mpeni sifa Yesu JF-Expert Member

  #17
  Sep 30, 2010
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 649
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  kwahiyo kinana msomali, mwenyekiti wa wasomali ndiye anayeandaliwa kuwa waziri mkuu? dah, hii balaa.
   
 18. Kudadeki

  Kudadeki JF-Expert Member

  #18
  Sep 30, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bora ubaki kumsifia Yesu kanisani badala ya kuingia kwenye siasa. :A S 13:
   
 19. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #19
  Sep 30, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Umenena neno jema.... My encounter with kinana is bad, i just realised ana dharau and he cared less for ordinary people
   
 20. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #20
  Sep 30, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  mwafrika kapiga msumari aisee
   
Loading...