Heshima na hadhi ya Sheikh Ponda katika nyoyo za Waislam

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,913
30,255
FAHAMU HESHIMA NA HADHI YA SHEIKH PONDA KATIKA NYOYO ZA WAISLAM

''Allah ni Mjuzi Allah na ni Mbora wa kulipa.

Sheikh Ponda utayakuta malipo yako kwa Allah yakiwa makubwa kwa subra na ustahamilivu kwa ajili ya dini yake. Hukuwa tayari kuuza uhuru wako kwa matakwa ya wenye kudhulumu. Muda wote ulitutia moyo mawakili wako kila tulipokutana na vitimbi. Mara nyingi sisi mawakili tulikuwa kama wateja na wewe ndiye wakili.

Hakika wewe ni kiongozi. Umma huu wa Waislam wa Tanzania utaishi kwa mfano wako. Alhamdulilah leo uko huru baada ya miaka miwili na miezi mitatu jela ukiwa na jeraha kubwa la risasi. Allah anayo siri kubwa katika maisha yako Sheikh Ponda. Allah akuhifadhi kiongozi wetu. Amin.''

Wakili Juma Nassoro

Ilikuwa katika semina ya Vijana wa Kiislam Tanzania mwaka wa 1988 ndipo kwa mara ya kwanza nilipofahamiana na Sheikh Issa Ponda. Ninachokumbuka kwa Sheikh Ponda ni kuwa alitusalisha sala moja na niliusikia usomaji wake mzuri wa Qur'an. Nilimpenda Ponda kutoka siku hiyo. Semina hii ilikuja baada ya mambo mengi dhidi ya Uislam kutokea nchini.

Kulikuwa na sakata la Sophia Kawawa kutaka Qur'an ibadilishwe. Hii ilitokea mwezi Mei 1988. Baada ya kauli hiyo palifanyika maandamano makubwa Zanzibar kumpinga Sophia Kawawa na Waislam walishambuliwa, baadhi wakauliwa na wengine wakapata ulemavu wa maisha.

Sheikh Said Gwiji mshtakiwa namba moja na wenzake walishitakiwa na wakafungwa jela miezi 18. (Mwaka wa 2012 nilifanya mahojiano na Sheikh Gwiji na akaniambia hajuti kuwa katika historia ya maisha yake alipatwa kufungwa jela). Kosa lao likiwa ni kuihami Qur'an ya Allah isichezewe.

Kulikuwa na vita vikipigwa dhidi ya vazi la hijab na kesi maarufu ilikuwa ya Fikira Omari mfanyakazi wa Kiltex. Kulikuwa na kesi ya Sheikh Kurwa Shauri aliyeshitakiwa kwa ''uchochezi'' na mambo mengine. Sheikh Kurwa Shauri aliwekwa rumande na akiletwa mahakamani yuko nusu uchi. Alishinda kesi lakini alifukuzwa Zanzibar na kupelekwa "kwao," Zanzibar.

Katika hayo kulikuwa na tatizo la Mchungaji Christopher Mtikila aliyekuwa akimbughudhi Rais Mwinyi na kuwashambulia Waislam hasa wenye asili ya Kiasia na Kiarabu bila woga na magazeti yakimtoa katika picha na sura ya kuzidi kumjaza jeuri na ukaidi.

Kulikuwa pia na ''Christian Lobby,'' mtandao wa siri katika vyombo vya habari vilivyokuwa vikiwapiga vita Waislam waliokuwa katika serikali ya Rais Mwinyi achilia mbali kuupiga vita Uislam wenyewe wakitumia nafasi zao katika vyombo hivyo. Ulikuwapo mtandao wa chini kwa chini wa vijana wa Kiislam kupambana na fitna hizi. Mwaka wa 1988 wakakutana Dodoma na hapa ndipo nilipojuana na Sheikh Ponda Issa Ponda.

Historia ya Waislam wa Tanzania itakapokuja kuandikwa jina la Sheikh Ponda Issa Ponda litaunganishwa na jina la Mufti Sheikh Hassan bin Amir kwa kitu kimoja nacho ni ardhi ya Chang'ombe Dar es Salaam ambako Waislam chini ya uongozi wa East African Muslim Welfare Society (EAMWS) walikusudia kujenga Chuo Kikuu mwaka wa 1968.

Katika uwanja huu ndipo Rais wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere akishuhudiwa na Tewa Said Tewa na Mufti Sheikh Hassan bin Amir aliweka jiwe la msingi la chuo hicho.

Chuo hakikujengwa na EAMWS ikapigwa marufuku na serikali. Mambo hayakuishia hapo. Sheikh Hassan bin Amir akakamatwa na kufukuzwa nchini akarudishwa ''kwao'' Zanzibar. Serikali ikaunda BAKWATA na Chuo Kikuu cha Waislam hakikujengwa.

Nini kilisababisha nakma hii?

Leo si tabu kujua sababu yake. Kulikuwa na viongozi ndani ya serikali ambao hawakupendezewa kuona Waislam wanaelimika.

Waliokuwa karibu na Sheikh Hassan bin Amir wanasema katika siku zake za mwisho kila alipotajiwa ule mradi wa chuo kikuu alikuwa akilia na kusema ilikuwa hamu yake kujenga chuo Kikuu kama Azhar ya Misri na akifika hapo alikuwa akibubujikwa na machozi.

Wakati ule Sheikh Hassan bin alikuwa na miaka zaidi ya 90 na aliishi na simanzi hizi hadi alipokufa mwaka 1979.

Sasa msomaji wangu fikiria na jiulize kwa historia kama hii Waislam wanawatazamaje masheikh wa BAKWATA wanapokusanyika na kumshambulia Sheikh Ponda?

Ponda aliyeongoza maandamano ya Waislam dhidi ya Baraza la Mitihani Tanzania lililokuwa likishutumiwa kuhujumu wanafunzi katika shule za Kiislam.

Sheikh Ponda ana historia ya kutukuka katika kupigania haki bila hofu hawa masheikh wa BAKWATA hawataishi kuifikia.

Picha: Picha ya kwanza Sheikh Ponda na Wakili Juma Nassoro Mahakamani Morogoro. Picha ya pili Sheikh Ponda akiwa kafungwa pingu na picha ya tatu Sheikh Ponda ameelekea Kibla Msikiti wa Kichangani anaomba dua kabla hajaongoza maandamano dhidi ya Baraza la Mitihani mwaka wa 2012.
 
Sheikh Ponda Issa Ponda
Screenshot_20201022-063259.jpg
 
Sheikh Ponda ana historia ya kutukuka katika kupigania haki bila hofu hawa masheikh wa BAKWATA hawataishi kuifikia.
 
Nyakati hazidumu Mzee wangu

Mimi nimefahamu huyu ponda miaka ishirini nyuma, si huyu aliyeamua kukumbatia mambo machafua ya Chadema ili apate anachostahili
Bia...
Kweli sisi ni watu masikini sana lakini nakulia yamini Ponda si wa kuuza heshima yake.
Zilipata kutoka fedha kwa wengi yeye alipopelekewa alizikataa lau kama ana shida.
 
..Sheikh Ponda angekuwa anataka pesa angekwenda kwenye majukwa ya CCM.

..Mtu muoga, mwenye tamaa ya fedha, mwenye kupenda starehe, hawezi kuwa karibu na Tundu Lissu katika mazingira ya siasa za miaka hii.

..Tundu Lissu amekuwa mtetezi wa HAKI ktk nchi yetu kwa zaidi ya miaka 20, na hicho ndicho kilichomsukuma Sheikh Ponda kumuunga mkono.
 
FAHAMU HESHIMA NA HADHI YA SHEIKH PONDA KATIKA NYOYO ZA WAISLAM

''Allah ni Mjuzi Allah na ni Mbora wa kulipa.

Sheikh Ponda utayakuta malipo yako kwa Allah yakiwa makubwa kwa subra na ustahamilivu kwa ajili ya dini yake. Hukuwa tayari kuuza uhuru wako kwa matakwa ya wenye kudhulumu. Muda wote ulitutia moyo mawakili wako kila tulipokutana na vitimbi. Mara nyingi sisi mawakili tulikuwa kama wateja na wewe ndiye wakili.

Hakika wewe ni kiongozi. Umma huu wa Waislam wa Tanzania utaishi kwa mfano wako. Alhamdulilah leo uko huru baada ya miaka miwili na miezi mitatu jela ukiwa na jeraha kubwa la risasi. Allah anayo siri kubwa katika maisha yako Sheikh Ponda. Allah akuhifadhi kiongozi wetu. Amin.''

Wakili Juma Nassoro

Ilikuwa katika semina ya Vijana wa Kiislam Tanzania mwaka wa 1988 ndipo kwa mara ya kwanza nilipofahamiana na Sheikh Issa Ponda. Ninachokumbuka kwa Sheikh Ponda ni kuwa alitusalisha sala moja na niliusikia usomaji wake mzuri wa Qur'an. Nilimpenda Ponda kutoka siku hiyo. Semina hii ilikuja baada ya mambo mengi dhidi ya Uislam kutokea nchini.

Kulikuwa na sakata la Sophia Kawawa kutaka Qur'an ibadilishwe. Hii ilitokea mwezi Mei 1988. Baada ya kauli hiyo palifanyika maandamano makubwa Zanzibar kumpinga Sophia Kawawa na Waislam walishambuliwa, baadhi wakauliwa na wengine wakapata ulemavu wa maisha.

Sheikh Said Gwiji mshtakiwa namba moja na wenzake walishitakiwa na wakafungwa jela miezi 18. (Mwaka wa 2012 nilifanya mahojiano na Sheikh Gwiji na akaniambia hajuti kuwa katika historia ya maisha yake alipatwa kufungwa jela). Kosa lao likiwa ni kuihami Qur'an ya Allah isichezewe.

Kulikuwa na vita vikipigwa dhidi ya vazi la hijab na kesi maarufu ilikuwa ya Fikira Omari mfanyakazi wa Kiltex. Kulikuwa na kesi ya Sheikh Kurwa Shauri aliyeshitakiwa kwa ''uchochezi'' na mambo mengine. Sheikh Kurwa Shauri aliwekwa rumande na akiletwa mahakamani yuko nusu uchi. Alishinda kesi lakini alifukuzwa Zanzibar na kupelekwa "kwao," Zanzibar.

Katika hayo kulikuwa na tatizo la Mchungaji Christopher Mtikila aliyekuwa akimbughudhi Rais Mwinyi na kuwashambulia Waislam hasa wenye asili ya Kiasia na Kiarabu bila woga na magazeti yakimtoa katika picha na sura ya kuzidi kumjaza jeuri na ukaidi.

Kulikuwa pia na ''Christian Lobby,'' mtandao wa siri katika vyombo vya habari vilivyokuwa vikiwapiga vita Waislam waliokuwa katika serikali ya Rais Mwinyi achilia mbali kuupiga vita Uislam wenyewe wakitumia nafasi zao katika vyombo hivyo. Ulikuwapo mtandao wa chini kwa chini wa vijana wa Kiislam kupambana na fitna hizi. Mwaka wa 1988 wakakutana Dodoma na hapa ndipo nilipojuana na Sheikh Ponda Issa Ponda.

Historia ya Waislam wa Tanzania itakapokuja kuandikwa jina la Sheikh Ponda Issa Ponda litaunganishwa na jina la Mufti Sheikh Hassan bin Amir kwa kitu kimoja nacho ni ardhi ya Chang'ombe Dar es Salaam ambako Waislam chini ya uongozi wa East African Muslim Welfare Society (EAMWS) walikusudia kujenga Chuo Kikuu mwaka wa 1968.

Katika uwanja huu ndipo Rais wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere akishuhudiwa na Tewa Said Tewa na Mufti Sheikh Hassan bin Amir aliweka jiwe la msingi la chuo hicho.

Chuo hakikujengwa na EAMWS ikapigwa marufuku na serikali. Mambo hayakuishia hapo. Sheikh Hassan bin Amir akakamatwa na kufukuzwa nchini akarudishwa ''kwao'' Zanzibar. Serikali ikaunda BAKWATA na Chuo Kikuu cha Waislam hakikujengwa.

Nini kilisababisha nakma hii?

Leo si tabu kujua sababu yake. Kulikuwa na viongozi ndani ya serikali ambao hawakuoendezewa kuona Waislam wanaelimika.

Waliokuwa karibu na Sheikh Hassan bin Amir wanasema katika siku zake za mwisho kila alipotajiwa ule mradi wa chuo kikuu alikuwa akilia na kusema ilikuwa hamu yake kujenga chuo Kikuu kama Azhar ya Misri na akifika hapo alikuwa akibubujikwa na machozi.

Wakati ule Sheikh Hassan bin alikuwa na miaka zaidi ya 90 na aliishi na simanzi hizi hadi alipokufa mwaka 1979.

Sasa msomaji wangu fikiria na jiulize kwa historia kama hii Waislam wanawatazamaje masheikh wa BAKWATA wanapokusanyika na kumshambulia Sheikh Ponda?

Ponda aliyeongoza maandamano ya Waislam dhidi ya Baraza la Mitihani Tanzania lililokuwa likishutumiwa kuhujumu wanafunzi katika shule za Kiislam.

Sheikh Ponda ana historia ya kutukuka katika kupigania haki bila hofu hawa masheikh wa BAKWATA hawataishi kuifikia.

Picha: Picha ya kwanza Sheikh Ponda na Wakili Juma Nassoro Mahakamani Morogoro. Picha ya pili Sheikh Ponda akiwa kafungwa pingu na picha ya tatu Sheikh Ponda ameelekea Kibla Msikiti wa Kichangani anaomba dua kabla hajaongoza maandamano dhidi ya Baraza la Mitihani mwaka wa 2012.

Muda ni mwalimu mzuri. Toka 1961 mpaka leo bado mnaonewa? Nani anawaonea? Kuna mambo sina shaka hayatakaa kutokea, kama hili la kutaka dini moja iwe ndio mmliki wa Tanzania nzima.
We all have equal space. Tusipojua hilo tutakonda kwa kujisengenya na kuwaza mambo ambayo ni ya kufikirika. Naam, tukapige kura ili kuondoa hawa wanaojipa matumaini hewa
 
Nikiri nimekuwa mgumu kumuelewa Sheikh Ponda na harakati za waislamu hapa nchini. Nimekuwa nikijiuliza kwann waislamu wanalalamika halafu hawaachi kuichagua ccm? Labda vyama vya upinzan vilikosa mtu wa kuaminika wa kariba ya Tundu Lissu. Hii ya Sheikh Ponda kumuunga mkono Lissu ni game changer, ashinde au asishinde..

Hoja yangu ni kwamba, ktk kudai maslahi ya waislamu, adui sio mkristo. Ni mfumo. Bahati mbaya sana harakati hiz kuna wakat zilitugawa. Tuendelee kuelimishana, leo wote tunaona unafiki wa TEC, hawana mboyoyo kama wakat wa JK. Akija rais muislamu tutawamulika!
 
Bia...
Kweli sisi ni watu masikini sana lakini nakulia yamini Ponda si wa kuuza heshima yake.

Zilipata kutoka fedha kwa wengi yeye alipopelekewa alizikataa lau kama ana shida.
Nilitamani usingeijibu hii hoja maana huyu kuna upande ameegama bila ya hoja wala sababu ya msingi!
Zipo hoja za kujibu au kuzitolea ufafanuzi lakini kama itakupendeza wengine ni kuziba masikio to na mibwatuko yao.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom