Heshima mbele Rais Kikwete, lakini Barack Obama road lazima iondoke

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,786
Watu wa USA huwa nawasikia wakisema mara nyingi hasa kwenye vyombo vya habari kwamba If you knew then what you know now, would you ...? Hivyo basi nina uhakika Rais wetu mstaafu Kikwete alikuwa na nia njema kabisa wakati tunabadilisha jina la Mtaa/Br. Kivukoni kwenda Barack Obama ambalo ndilo jina la Mtaa ilipo Ikulu yetu!

Lkn sasa muda umepita na mara nyingi muda hutoa majibu ya mambo mengi, ambapo hutupa pia mtazamo mwingine kabisa, hivyo basi nina uhakika kabisa Raisi Kikwete leo hii ana mtazamo tofauti na uamuzi wake sema tu hana uwezo wa kubadilisha chochote!

Hivyo Mkuu wa Mkoa Makonda wewe ndiyo mwenye huo uwezo tafadhali tuondolee hii dhihaka wakazi wa Dar kwa kuondoa hili jina, huyu mtu (Barack Obama) ni war criminal, hakuna Rais wa USA aliyeua moja kwa kwa moja Waafrika kama Rais Obama, hakuna Raisi wa USA aliyeipuuzia Afrika kama Rais Obama, hivyo tafadhali Mkuu Mkoa wa Dar, usitufanye Dunia ituone wajinga, Obama hastahili kupewa jina la Mtaa hapa Tanzania, angalau mngeita George Bush, angalau labda tungekuwa na hoja kwa kiasi fulani kwa maana hata kuna Kiwanda Arusha Kikubwa cha textile kimejengwa kwa sababu ya fedha za George Bush, Bush alileta TZ yetu, 500 million US Dollars, alikaa ndani ya TZ yetu siku 4 akaenda mpaka Arusha kuna Watz wengi wamejiriwa leo hii Arusha kwa sababu ya fedha alizoleta G.Bush!

Lakini Obama haithamini Afrika hata kidogo na kama ulikuwa haumini nitakupa mfano Obama anamaliza muda wake miezi michache ijayo na ameshazunguka Dunia nzima kuaga, amekwenda Ulaya, Marekani Kusini, Kanada, Asia nchi mbali mbali pmj na kuhudhuria ASEAN (Asia) summit na kuaga rasmi lkn hajakanyaga Afrika kuaga, kwa nini? Kwa nini hajaenda kwenye Kikao cha AU kuaga?

Jibu ni rahisi sisi siyo muhimu kwake, sasa ni kwa nini sisi tunamthamini kiasi hicho mpaka kumpa jina la Mtaa wetu muhimu? Hivyo tafadhali ondoa Barack Obama road na rudisha Kivukoni yetu au kama jina lazima tubadilishe basi tuchukuwe majina yetu na kama ni lazima liwe jina la kigeni basi liwe mtu ambaye amegusa maisha yetu moja kwa moja na wapo wengi sana Dunia hii lkn siyo Obama!

OBAMA3.jpg


hqdefault.jpg
 
Tofauti tu na war criminal ni ngumu na impossible kukuta mitaa ya Columbia province ina jina la yeyote asiye na asili typically ya marekani that's impossible sijui huyo bwana alipagawa na kipi kuupa first street jina la Obama homosexuality fighter and hero hii ni aibu kupindukia kama taifa hatukupaswa kabisa kuupa mtaa wa ikulu jina lolote kutoka nje ya founding fathers wa Tanzania.
 
Kinjeketile street, abushiri street, mkwawa street, majimaji street, nk...... tuna majina mengi sana yenye historia katika taifa hili ambayo tungeweza kuibatiza mitaa yetu na miji yetu. Hili taifa ni janga sana na nafikiri kunatatizo sehemu na hilo tatizo hapo mahala ndio ubishi wetu kila siku, CCM ndio tatizo kuu.......
 
anzisheni hata hapa kazi tu we dont care hakuna la maana kuwepo au kutokuwepo ..........
 
Watu wa USA huwa nawasikia wakisema mara nyingi hasa kwenye vyombo vya habari kwamba If you knew then what you know now, would you ...? Hivyo basi nina uhakika Raisi wetu mstaafu Kikwete alikuwa na nia njema kabisa wakati tunabadilisha jina la Mtaa/Br. Kivukoni kwenda Barack Obama ambalo ndilo jina la Mtaa ilipo Ikulu yetu!
Lkn sasa muda umepita na mara nyingi muda hutoa majibu ya mambo mengi, ambapo hutupa pia mtazamo mwingine kabisa, hivyo basi nina uhakika kabisa Raisi Kikwete leo hii ana mtazamo tofauti na uamuzi wake sema tu hana uwezo wa kubadilisha chochote!

Hivyo Mkuu wa Mkoa Makonda wewe ndiyo mwenye huo uwezo tafadhali tuondolee hii dhihaka wakazi wa Dar kwa kuondoa hili jina, huyu mtu (Barack Obama) ni war criminal, hakuna Raisi wa USA aliyeua moja kwa kwa moja Waafrika kama Raisi Obama, hakuna Raisi wa USA aliyeipuuzia Afrika kama Raisi Obama, hivyo tafadhali Mkuu Mkoa wa Dar, usitufanye Dunia ituone wajinga, Obama hastahili kupewa jina la Mtaa hapa Tanzania, angalau mngeita George Bush, angalau labda tungekuwa na hoja kwa kiasi fulani kwa maana hata kuna Kiwanda Arusha Kikubwa cha textile kimejengwa kwa sababu ya fedha za George Bush, Bush alileta TZ yetu, 500 million US Dollars, alikaa ndani ya TZ yetu siku 4 akaenda mpaka Arusha kuna Watz wengi wamejiriwa leo hii Arusha kwa sababu ya fedha alizoleta G.Bush, lkn Obama haitahmini Afrika hata kidogo na kama ulikuwa haumini nitakupa mfano Obama anamaliza muda wake miezi michache iliyopita ameshazunguka Dunia nzima kuaga, amekwenda Ulaya, Marekani Kusini, Kanada, Asia nchi mbali mbali pmj na kuhudhuria ASEAN (Asia) summit na kuaga rasmi lkn hajakanyaga Afrika kuaga kwa nini? Kwa nini hajaenda kwenye Kikao cha AU kuaga? Jibu ni rahisi sisi siyo muhimu kwake, sasa ni kwa nini sisi tunamthamini kiasi hicho mpaka kumpa jina la Mtaa wetu muhimu? Hivyo tafadhali ondoa Barack Obama road na rudisha Kivukoni yetu au kama jina lazima tubadilishe basi tuchukuwe majina yetu na kama ni lazima liwe jina la kigeni basi liwe mtu ambaye megusa maisha yetu moja kwa moja na wapo wengi sana Dunia hii lkn siyo Obama!
Obama mlivyokuwa mnampa heshima ya barabara kuitwa jina lake hamkusumbua ubongo wenu (kama upo) kuyatambua haya??

na huyo kwenye blue mnayemfagilia sasa akija baadae kuwatia vidole....mtakuwa na lipi la kutuambia tena??

kwa akili hii, no wonder nchi hii imeendelea kuwa shamba la bibi 50 years post-independence.
 
Hakuna nchi ambayo USA inaifagilia kama UK. Kuna muingereza aliiitwa Winston Churchill Wamarekani wanampenda kuliko mtume wao, Jesus Christ. Lakini hakuna hata mtaa mmoja Marekani utakuta unaitwa Winston Churchill street. Sisi Waafrika, Watanzania, ni mambwiga tusiojithamini. Huwezi kukuta Marekani mtaa unaitwa kiongozi wa Afrika. Hususan mtaa ambao ndio una Ikulu yao. Neeever! Ever! Never, Never, Never!

Nimewahi kusema ni bora angepewa hata Ronald Reagan, alileta mahindi ya kulishia ng'ombe wa marekani tukala kala hapa wakati wa njaa tulipotoka vita vya Kagera.

Au JF Kennedy au Jimmy Carter, hawa nao walitujali jali, walimuheshimu Nyerere, walimuita Marekani kwa ziara maalum wakamfanyia dhifa ya kitaifa Whitehouse.

Barack Obama hana mtaa kwao Marekani! Hata yeye alishangaa sana. Alituona hawa third world people wanashoboka kunipa mtaa wa Ikulu yao, vichwa panzi wakubwa hawa watu.
 
Obama mlivyokuwa mnampa heshima ya barabara kuitwa jina lake hamkusumbua ubongo wenu (kama upo) kuyatambua haya??

na huyo kwenye blue mnayemfagilia sasa akija baadae kuwatia vidole....mtakuwa na lipi la kutuambia tena??

kwa akili hii, no wonder nchi hii imeendelea kuwa shamba la bibi 50 years post-independence.


Jaribu kuelewa nilichoandika kama ukipenda, nimesema kama ilikuwa ni lazima kufanya hivyo basi angalau G.Bush alistahili zaidi ya Obama, isitoshe Obama ndiyo atayekayetutia vidole kama bado hajaanza kututia vidole kwani kila siku unasikia kuna NGO hapa kwetu zinafungiwa ambazo zinaeneza USHOGA, sasa hv zimesambaa TZ nzima, kwa maana yeye (Obama) ndiyo anataka mambo ya homosexuality wakati G.Bush alipinga, Bush ni conservative na Serikali yake ilipinga kutoa mimba, ushoga na mambo mengine mengi lkn hiyo ni mada nyingine hata hivyo!
 
Huwezi kukuta Marekani mtaa unaitwa kiongozi wa Afrika. Hususan mtaa ambao ndio una Ikulu yao. Neeever! Ever! Never, Never, Never!

No facts,No right to speak.....
According to the Nelson Mandela Centre for Memory, no fewer than 120 streets, roads, boulevards, avenues, bridges, and highways have been named after the first democratically elected president of South Africa, who turns 95 today. A thorough search turned up more than 140, including 50 in South Africa and 10 in the United States. Click on any icon for the full name and location of a Mandela-inspired roadway; zoom in to see the a street map.
source:
Map: Streets Named After Nelson Mandela,

Barack Obama hana mtaa kwao Marekani! Hata yeye alishangaa sana. Alituona hawa third world people wanashoboka kunipa mtaa wa Ikulu yao, vichwa panzi wakubwa hawa watu.
Kwa nini usitetee hoja yako na Facts...???
List of things named after Barack Obama -
 
Jaribu kuelewa nilichoandika kama ukipenda, nimesema kama ilikuwa ni lazima kufanya hivyo basi angalau G.Bush alistahili zaidi ya Obama, isitoshe Obama ndiyo atayekayetutia vidole kama bado hajaanza kututia vidole kwani kila siku unasikia kuna NGO hapa kwetu zinafungiwa ambazo zinaeneza USHOGA, sasa hv zimesambaa TZ nzima, kwa maana yeye (Obama) ndiyo anataka mambo ya homosexuality wakati G.Bush alipinga, Bush ni conservative na Serikali yake ilipinga kutoa mimba, ushoga na mambo mengine mengi lkn hiyo ni mada nyingine hata hivyo!
cut the bull....US wame-pull the plug kwenye MCC cash - that's why!

sijui ushoga, nk ni visingizio tu - mbona miongoni mwenu wanaoshabikia haya mambo wapo kibao na wanajulikana!
 
cut the bull....US wame-pull the plug kwenye MCC cash - that's why!

sijui ushoga, nk ni visingizio tu - mbona miongoni mwenu wanaoshabikia haya mambo wapo kibao na wanajulikana!


Kuna uhusiano gani wa nilichoandika na MCC?
 
hahaha mlifagia na kudeki barabara na polisi wenu walipekuliwa hadi makufuli yao aisee baraka noma
 
Hauoni kama ktk wote hao ambao wameita jina ya Barack Obama sisi ndiyo tumempa heshima ya juu kuliko wote? Huko Malaysia Bakteria ambaye anashambulia mapafu na kusababisha ugonjwa ndiyo amepewa jina la Barack Obama! Soma wote hao halafu linganisha na kwetu, uone kama sisi wajinga!
kufaa au kutofaa ni maoni yako...Mimi nilikuwa namjibu huyu anayepinga kwa kuleta hoja za uwongo.....
 
Hata hivyo Obama sijyi Osama. Anabaki kuwa rais wa Marekani kwahiyo kujipendekeza kwake,ni kujilisha upupu na upepo tuu.Turudi tu kwenye misingi ya jamii yetu.
 
Back
Top Bottom