Heshima kwa walevi na wavuta sigara

bahati93

JF-Expert Member
Aug 6, 2015
1,049
1,906
Hapa kwetu bongo kuna vimbwanga vya kila aina ila mbali ya yote kumekuwa na tabia ya watu kuzarauliana kutokana na vipawa mbalimbali ambavyo watu wanavyo kama ulevi wa wastani na uliopindukia. Nasikitika jamii yetu imekuwa kipofu kuona mchango wa walevi kuwaona kama kwamba hawana akili na hawajui matumizi mazuri ya pesa. Wengine wanaenda mbali na kudiriki kuwaza kwamba eti bar zote zifunguliwe tu wikiendi.

Mbali na yote haya yatupasa tuwaombe walevi wanywe Zaidi kutokana na ukweli kuwa serikali inategemea kodi nyingi kutoka kwa bia na pombe sasa ukiwasumbua walevi wakagoma kunywa hio kodi uliopigia maesabu lukuki utaipata wapi au unafikiri madeski yatajijenga yenyewe.

Sasa endapo utamwona mlevi anayumba yumba usifikiri anayumba kwamba kilevi kimemkolea hapana anayumba Amani na faraja anapojua kwamba amechangia bila shurutu kodi ya taifa na hivyo kudhibitisha tz ndani ya bongo inaenda mbele kwa mbele.

Ata mimi mwenyewe nataka nianze kuwa mlevi nichangie pato la taifa haswa.
 
Mkuu naona tayari umelewa wakati unaandika hii article.

Naomba kuuliza ni magonjwa mangapi yanasababishwa na uvutaji sigara pamoja na ulevi ulio kithiri?

Je tunapotenza billioni ngapi kwenye mahospitali kila mwaka kutibu hao watu mfano watu wenye lung cancer?

In top of that ni familia ngapi zimeathirika ajili ya ulevi siongelei financial peke yake aina zote za abuse.

Mkuu everything in moderation. Kwa jinsi we unavyohalallisha ni hatari.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom