Hesabu za gharama za usafiri kwa muajiriwa aliyeachishwa kazi.

Complicator

JF-Expert Member
Aug 23, 2013
2,198
3,566
wakuu naomba kuuliza kwa anayejua namna hesabu ya kumlipa mfanyakazi aliyeachishwa kazi gharama ya kumsafirisha.

na kila jambo linalohusu gharama za usafiri

muhimu sana.
 
wakuu naomba kuuliza kwa anayejua namna hesabu ya kumlipa mfanyakazi aliyeachishwa kazi gharama ya kumsafirisha.

na kila jambo linalohusu gharama za usafiri

muhimu sana.
Kwa mujibu wa sheria ya ajira na mahusiano kazini, kifungu cha 43 kinaeleza mazingira na namna ambayo muajiri anapaswa kulipa gharama hizo za usafiri kwa muajiriwa baada ya kumuachisha.

Moja ya jambo la msingi ama kanuni kuu ni kwamba muajiri atamlipa gharama za usafiri endapo tu mkataba wa kazi umesitishwa pahala tofauti na pale mfanyakazi alipoajiriwa mathalani, ukiajiriwa Dar es salaam na ukapelekwa kituo cha kazi Arusha, basi hapo ndo wapaswa kulipwa hizo gharama.

Vile vile, sheria imeweka utaratibu juu ya namna ya mwajili atalipa gharama za usafiri kwa kufanya kati ya yafuatayo:

i) Kumsafirisha mwajiriwa wake pamoja na mali zake mpaka mahala alipomuajiri.

ii) Kulipia gharama za kumsafirisha mpaka mahala alipomuajiri.

iii) Kumlipa mwajiriwa moja kwa moja, gharama za kumsafirisha yeye na familia pamoja gharama nyingine zinazohusiana na na usafiri kama zipo mpaka mahala alipoajiriwa 'place of recruitment'.

N.B Kiwango cha malipo kitategemea na nauli inayowezesha kumfikisha mpaka sehemu alipoajiriwa.
 
Back
Top Bottom