Hesabu za CHADEMA ktk kuichukua Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hesabu za CHADEMA ktk kuichukua Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Yakuza, May 23, 2011.

 1. Yakuza

  Yakuza Senior Member

  #1
  May 23, 2011
  Joined: May 22, 2011
  Messages: 112
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Wapendwa wana-JF

  Ukweli ninajiuliza maswali mengi ata sipati mtu wa kunipa majawabu.

  Leo hii:

  1. CDM wameishateka mikoa ya Kanda ya Ziwa kwa maana ya Mara, Mwanza, Shinyanga na Kagera
  2. CDM wameishamaliza kazi mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, hususani mikoa ya Iringa na Mbeya
  3. CDM walimaliza zamani homework yao mikoa ya Kanda ya Kaskazini hususani Arusha na Kilimanjaro
  4. Kanda ya Mashariki haina kazi, kwa sababu ni mchanganyiko wa watu mbalimbali wengi wakitokea kanda nilizotaja hapo juu. Kwa lugha nyingine, mikoa ya Dar, Pwani na Morogoro kwa CDM naona kazi kwisheni....
  5. Kanda ya Magharibi, kwa maana ya Kigoma, Tabora na Rukwa....nayo kazi almost kwisheni. Kigoma ni base ya Upinzani miaka nenda rudi. Kisiasa, kiuchumi, kijamii na kimaendeleo maeneo haya ndiyo Tanzania yetu.
  6. Kanda ya Kati kwa maana ya Dodoma na Singida kaachiwa Mh. Tundu Lisu na mama. Kasi kwisheni pia.
  7. CDM wamezama zaidi ktk shule za msingi, sekondari na vyuo. Katika vyuo vikuu walikuwa wamebakiza Mzumbe, huko moto unawaka tangu J'mosi wiki jana. Ninajua wanaelekea SUA....nako kwisheni.

  Kikubwa zaidi, CDM kwa kujitolea kugharimia mazishi ya wananchi waliouawa na Serikali, ni hesabu ya ajabu, ninasema hesabu ya ajabu ndiyo! Walifanya hivyo hivyo Arusha....Ujumbe wa chuki dhiki ya Serikali polepole unaingia akilini mwa watanzania ktk kila kona ya nchi hii. Hii inawapelekea wananchi kutaka mabadiliko.........tutake tusitake......Kibaya au kizuri zaidi CDM wanasema hukana kulala mpaka kieleweke....:mod:

  Haya yote yanishawishi kuendelea kujiuliza, hivi KWELI Mh. Rais ambaye pia ni M/Kiti wa CCM Taifa hayaoni haya. Mawaziri na washauri wake hawayaoni haya? Au wamekata tamaa?

  Jiulize, mfano leo hii uitishwe uchaguzi mkuu, Mh. Nyambale Nyangwine anaweza kuomba kura kwa wananchi wa Nyamongo? Ni nani ktk CCM anaweza kwenda Nyamongo kumnadi mgombea wake?

  Has CDM caused paralysis to Mr. President and the entire system? :smow:
  Nisamehe: Mimi sina itakadi ktk chama chochote cha siasa hapa Tanzania. Ni mdau tu.
   
 2. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #2
  May 23, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Haya mambo yaliyofanywa na CDM ni makubwa sana,CCM wanatakiwa wabuni mpanga mkakati ili kukabiliana na hali hii,vinginevyo itakula kwao mwaka 2015!!
   
 3. Don Alaba

  Don Alaba Senior Member

  #3
  May 23, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 158
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  CDM hakuna kulala lazima ifanye yale wananchi wanatarajia ili kuweza kuingia katika system, big up
   
 4. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #4
  May 23, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,644
  Likes Received: 1,436
  Trophy Points: 280
  :israel::israel::israel:
   
 5. T

  Tata JF-Expert Member

  #5
  May 23, 2011
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,737
  Likes Received: 657
  Trophy Points: 280
  Nyie ngojeni wamalize kuvua gamba mtawatambua. Watakuwa wepesi, wenye kasi na sumu kali zaidi. Afueni yenu ni labda hili gamba ling'ang'anie mwilini mwao.
   
 6. m

  m.o.d.y Member

  #6
  May 23, 2011
  Joined: May 22, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Remember one thing every dark night there is a bright day after that, so no mater hard it get ccm lazima iondoke madarakani by any means.
   
 7. U

  UMMATI Member

  #7
  May 23, 2011
  Joined: May 18, 2011
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CDM ni vema kuanza na uchaguzi wa serikali za mitaa 2014 kwani hicho ndio kipimo cha KUCHUKUA NCHI 21015.
   
 8. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #8
  May 23, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,422
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  hAPO KWENYE RED MKUU SIO CHUKI DHIDI YA SEREKALI BALI KUONYESHA UBORONGAJI WA SEREKALI

  HAPO KWENYE PINK HAWAWEZI KUZUIA KITU MKUU...VYAMA VYA SIASA VIMEUNDWA KWA SHERIA NA HILI NI JUKUMU LAKE....ZAIDI ZAIDI WANATEKELEZA WITO WA KIKWETE KUKATAA KUWA CHAMA CHA MUSIMU!!!!!

  NDIO KAZI YA RUZUKU BABA...KWANI HUKO KWA WANAMAGAMBA WANATUMIAJE RUZUKU ZAO?
   
 9. Elungata

  Elungata JF-Expert Member

  #9
  May 23, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 28,045
  Likes Received: 8,533
  Trophy Points: 280
  Hey.we mwenye thread watakaje kwani?kama we chadema pressure ya nini SI USHEREHEKE AU HUJIAMINI.

  Kumbuka huu ni mwaka wa kwanza katika ile mitano SO ANYTHING CAN HAPPEN.kumbuka hao ccm wanaweza kujirekebisha ndani ya miezi tu na wanazo resourse za kufanya hivo so usijipe matumainiya haraka WAWEZA KUJA LIA.
   
 10. Yakuza

  Yakuza Senior Member

  #10
  May 23, 2011
  Joined: May 22, 2011
  Messages: 112
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Of course, CCM bado ni moto wa kuotea mbali japo wamekabwa koo kwa kiasi fulani. Lakini mbona wako kimya, kana kwamba hakuna chochote kinachoendelea?
   
 11. Ernesto Che

  Ernesto Che JF-Expert Member

  #11
  May 23, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,117
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Si kama CCM wako kimya kwa kuamua bali hawana mbinu za kupambana na makombora ya kisiasa ya cdm. Alianza Makamba then Tambwe baadae Mukama wote wamechemsha. Kibaya zaidi wana mwenyekiti wa taifa dhaifu kupita yoyote katika historia ya chama chao, kwa upande wa pili cdm wana safu kali ya mashambulizi kuliko chama chochote. Kwa haraka huwezi kufananisha uwezo wa kiongozi yeyote nchi hii (ukiwatoa hayati Nyerere na Sokoine) mwenye uwezo na haiba kama dk Slaa.
  CCM kimepoteza dira kama alivyosema marehemu Kolimba (katibu mkuu wa zamani CCM) hilo halina ubishi tena
   
 12. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #12
  May 23, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kama ni kwa kubadilika na kuleta maendeleo basi hiyo
  itakua credit kubwa sana kwa chadema ambao wanapiga kelele kila siku
  kuhusu ufisadi na wananchi wanasikia!
   
 13. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #13
  May 23, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Yeah tunaimega hii taratibu muhimu majimbo ya chadema yanatakiwa yaonyeshe mfano kimaendeleo hata wa kupanda miti na usafi wa mazingira!
   
 14. Nyami2010

  Nyami2010 JF-Expert Member

  #14
  May 23, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Yeah, lets hope wabunge wa CDM wanalitambua hilo na kulifanyia kazi :dance:
   
Loading...