Hesabu ya maisha, vipi kwa maamuzi haya nimebugi au iko poa?

Busara Kali

Member
Jan 7, 2021
59
77
Nina miaka 34, Mke na watoto 2,Mwaka Jana nilikua na shauku ya ujenzi kiwanja nilisha nunua kina tofali kama 4000,Kokoto mende 3, mchanga mende 3, Tank za maji lita 4000. Nikatafuta mtaalam akanichorea ramani na kunifanyia tathmini ya ujenzi ni nyumba ya vyumba 3 master moja chini na kigorofa kina chumba kimoja master.

BOQ inahitaji 10m ya msingi tu nje ya material zilizoko site. Total garama ni kama 90m ujenzi kuisha. Kodi nilikua nalipa laki 4 na nusu nyumba ya room tatu. Ambayo ilikuwa kama 30km kutoka eneo langu la ofisi. Ikizingatiwa wife ni graduate kwa sasa hana kipato.

Mafuta ya gari almost laki 2na nusu kwa mwezi. Ikabidi nifanye màamuzi nitumie kama 7m kupata nyumba ya NHC ina vyumba 2, sebule jiko na public toilet, ambayo ipo 5km kutoka ofisini kwangu, na kodi ni laki 2 ambayo nailipa kila tareh 15 ya mwezi unaofuata.

Hii nilifanya ili niweze kushusha garama zangu za maisha ili kuweza kufanikisha dream house yangu. Wife alishauri kujenga servant house tuhamie ambayo ingegharimu kama 20 - 25m na site ipo 25km kutoka ofisini wazo Lake sikulipokea nikaamua on NHC apartments. Ambayo wife hana furaha nayo.

Ila mm natazama mbali kidogo na mwaka huu 2022 nataka nichukue ka mkopo wa miaka 3 angalau 40m ili nianze ujenzi na baada ya miaka 2 nifanye top up nichukue tena mkopo so nimejipa miaka 5 niwe nimekamilisha ujenzi. Tukumbuke hao watoto 2 nasomesha kama ada 4m kwa mwaka.
Haya maamuzi ni sahihi ??
 
Kuna namna ungeweza kujenga kwa awamu na kuhamia wakati ujenzi kamili wa ujenzi haujakamilika, huku mdogo mdogo ukiendelea. Kwa nyumba ya thamani ya 90milioni, ukiwa na 20milioni unaweza kufanya ujenzi wa awamu ili uhamie.

Upande wa pili pia ni sahihi, kama kupangisha ni laki mbili kwa mwezi na kujenga ni milioni 90 ni bora kuendelea kupangisha huku ukijenga taratibu.

Yote kwa yote, kwenye maisha kuna msemo maarufu kuwa, ukitaka kuwa na maisha yenye furaha basi jitahidi kuheshimu na kutii uchaguzi wa mke wao.
 
Nina miaka 34, Mke na watoto 2,Mwaka Jana nilikua na shauku ya ujenzi kiwanja nilisha nunua kina tofali kama 4000,Kokoto mende 3, mchanga mende 3, Tank za maji lita 4000. Nikatafuta mtaalam akanichorea ramani na kunifanyia tathmini ya ujenzi ni nyumba ya vyumba 3 master moja chini na kigorofa kina chumba kimoja master. BOQ inahitaji 10m ya msingi tu nje ya material zilizoko site. Total garama ni kama 90m ujenzi kuisha. Kodi nilikua nalipa laki 4 na nusu nyumba ya room tatu. Ambayo ilikuwa kama 30km kutoka eneo langu la ofisi. Ikizingatiwa wife ni graduate kwa sasa hana kipato. Mafuta ya gari almost laki 2na nusu kwa mwezi. Ikabidi nifanye màamuzi nitumie kama 7m kupata nyumba ya NHC ina vyumba 2, sebule jiko na public toilet, ambayo ipo 5km kutoka ofisini kwangu, na kodi ni laki 2 ambayo nailipa kila tareh 15 ya mwezi unaofuata. Hii nilifanya ili niweze kushusha garama zangu za maisha ili kuweza kufanikisha dream house yangu. Wife alishauri kujenga servant house tuhamie ambayo ingegharimu kama 20 - 25m na site ipo 25km kutoka ofisini wazo Lake sikulipokea nikaamua on NHC apartments. Ambayo wife hana furaha nayo. Ila mm natazama mbali kidogo na mwaka huu 2022 nataka nichukue ka mkopo wa miaka 3 angalau 40m ili nianze ujenzi na baada ya miaka 2 nifanye top up nichukue tena mkopo so nimejipa miaka 5 niwe nimekamilisha ujenzi. Tukumbuke hao watoto 2 nasomesha kama ada 4m kwa mwaka.
Haya maamuzi ni sahihi ??
Why ukope 40m kwajili ya kujenga nyumba?
Niko kwenye situation kama yako (wife hana kipato na ninaishi nyumba ya kupanga) nilinunua kiwanja nikajenga msingi wa nyumba ninayotaka. Nikachunguza gharama zilizotumika ni around 20m (kiwanja na msingi)nimezika
Nikaona kukopa hela nikazike wakati wife ataendelea kukaa nyumbani ilihali nimeongeza mzigo wa deni na kupunguza kipato,
Nikaamua kufungua biashara (kwa hela niliokuwa nimebaki nayo as hata ningejenga nisingemaliza kwa kuhamia)
Now, wife ana kazi (kijibiashara) na ujenzi utaendelea pole pole
 
Ujenzi wa Pole Pole unagarama tusiyoiona hii Jan nimeweza kumfungulia duka, kukopa ni expensive lakini ni rahisi, uwezo wangu kusavu pesa ni mdogo siwezi kujikontrol matumizi nikiwa na pesa hivyo bora mkopo ambapo utalipwa na mshahara then nitajua napiganaje kuishi.
 
Unaweza kutoa ushauri mbadala nitaupokea pia
 
Njia niliotumia mimi, sikai na pesa. Kila ninapopata fedha ile bajeti ya ujenzi naenda kulipia material mfano tofari, nondo, cement etc. Siku narudi site ninakuwa na material yote yanayohitajika. Fundi anapiga kazi yote kwa hatua niliopanga.
 
Unaweza kutoa ushauri mbadala nitaupokea pia
Mkuu, inategemeana na mtazamo wa mtu. Unapokopa hela ukaingiza kwenye kitu ambacho hakizalishi faida ujue unajiingiza kwenye mtego wa madeni ambayo yasababisha usumbufu kwa muda utakaokuwa unalipa.

Kwa mtazamo wangu, kwakuwa upo kwenye nyumba ya bei himilivu (kutoka 400k hadi 200k) tafuta namna ya mkeo kujishughulisha either kwa biashara au namna nyingine ili mpanue wigo wa kipato katika familia.

Ni hatari sana kuwa na single source of income katika familia. Haijalishi unaishi kwako au umepanga
 
Asante hili nimelifanikisha Jan hii.
 
Njia niliotumia mimi, sikai na pesa. Kila ninapopata fedha ile bajeti ya ujenzi naenda kulipia material mfano tofari, nondo, cement etc. Siku narudi site ninakuwa na material yote yanayohitajika. Fundi anapiga kazi yote kwa hatua niliopanga.
Nilishakusanya material site.
 
Mkeo yupo sahihi...wanawake huwa wanawaza hivi..' ukifa yeye ataenda wap? Itakuaje' wanawake wanatuwazia kifo maana mara nyingi wanaona sisi ndio hutangulia..
Pili, mwanamke akiwa kwake anajisikia raha kweli ndio maana wanawake wengi wanakua wa kwanza kuhamia hata kama nyumba haijaisha.
Kwa material uliyonayo, 40m unajenga nyumba nzuri na unahamia, alafu ukianza hizo top up zako ndio ujenge ghorofa lako
 
Ulifanya wazo la maana kuhamia karibu na ofisi Ili pia usichoke na kupunguza gharama, huyo mkeo mwambie aache ujinga na kukupa unnessary pressure zisizo na kichwa wala miguu maisha ni michakato ya taratibu, akiendeleza gumu mpuuze ufanye kimya kimya
 
Ujinga ni kuhonga 7m ili tu upate nyumba NHC ambayo utailipia kodi 200k kila mwezi, hapo umeokoa nini…. hiyo 7m ingelipa kodi miaka mingapi mtaani jirani na hapo NHC?
Kwa kodi ya laki tatu ni miaka miwili tu. Nadhani kodi za mtaani kwa hapo alipo ni kubwa sana...!
 
Kwa kodi ya laki tatu ni miaka miwili tu. Nadhani kodi za mtaani kwa hapo alipo ni kubwa sana...!
Kodi ya chini kabisa ya hapa mtaani jirani na nhc ni laki 6 ukipinga kwa mwaka ni milioni 7na laki 2. Hapo bado ishu za ulinzi,usafi ambazo kwa NHC ni ndani ya hyo lak 2... kimsingi kwa hesabu niyoipigaga ya miezi 24 nimeweza kusevu big time. Hapo bado hujaweka ishu ya muda
 
Back
Top Bottom