Hesabu kibantu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hesabu kibantu

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by TWANJUGUNA, Jun 17, 2010.

 1. T

  TWANJUGUNA Member

  #1
  Jun 17, 2010
  Joined: Jun 6, 2010
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  unapojifunza lugha nyingi, msamiati wa kwanza huwa tarakimu moja hadi kumi. lakini wajua kuwa neno la herufi 3 ni karibu sawa katika asilimia 70 ya lugha za ki-bantu?
  wajua kuwa lugha nyingi huwa base 10- yaani ni mafungu ya kumi kumi. ishirini ni mafungu ya kumi mara mbili, mia ni makumi kumi.....lakini kunayo lugha moja ya ki-bantu ya base 5.kwa mfano 6 ni isano na imo (5+1), 7 is isano na ibere.
   
 2. Kipala

  Kipala JF-Expert Member

  #2
  Jun 17, 2010
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 3,535
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 145
  Asante kwa mfano mzuri ulionipa motisha ya kuangalia jambo jili. Kwa kweli inaonekana ya kwamba katika lugha nyingi (zote?) za Kibantu namba za kimsingi ni za 1-5 pekee halafu 10. Yaani majina ya namba ya kimsingi ni yale yenye neno la pekee kwa namba na baadaye kuna majina yaliyounganishwa.
  Mfano kwa Kiingereza (kama lugha zote za Kigermanik) kuna majina ya kimsingi kwa namba kuanzia 1 hadi 12 (ten-eleven-twelve, kama Kijerumani zehn-elf-zwoelf); kuanzia 13 majina yameunganishwa three-ten (=thirteen), four-ten na kadhalika. Kumbe wewe umekuta lugha ile (ni lugha gani?) inayohesabu "isano na imo (5+1), 7 is isano na ibere". Kamusi yangu inasema ya kwamba lugha nyingi za Kibantu zimechukua majina ya 6-9 kutoka lugha nyingine, kama Kiswahili sita, saba, tisa (Kiarabu) na nane ni labda nne-nne. Kumbe.

  Nimekuta pia hoja ya kwamba msingi wa muundo wa majina ya namba katika lugha mbalimbali ni ama mfumo wa 5 (kama Kibantu - vidole vya mkono 1), 10 (vidole vya mikono miwili), 20 (vidole vya mikono na miguu). Ila tu mfumo wa 12 namna gani? Wengine husema ukihesabu viungo vya vidole vya mkono 1 bila dole gumba unafikia 12.
   
 3. T

  TWANJUGUNA Member

  #3
  Jun 17, 2010
  Joined: Jun 6, 2010
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Asante, post lako hili limeniangazia upya kuwa kweli herufi 1 hadi 5 kwa kibantu zina shina moja.
  1. imo, imwe, ........
  2. ibiri, shibiri, igiri,
  3. isato, ithatu, itatu...
  4. inei, inya, ina....
  5. isano, ithano, itano....
   
 4. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #4
  Jun 17, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,365
  Likes Received: 6,992
  Trophy Points: 280
  ni kweli katika kibantu namba moja mpaka tano almost zinafanana, lakini kuanzia sita mpaka Tisa kunakuwa na tofauti kubwa, lakini ukija kwenye kumi kibantu kinakuwa na almost same name, na format ya kuanzia kumi kwenda mbele pia ni kama inafanana, hebutujaribu kuangalia mfano wa Bantu ya Southern part ya africa
  SHONA
  1. Motsi
  2. Piri
  3. Tatu
  4. China
  5. Chanu
  6. Tanhatu
  7. Nomwe
  9. Pfumbamwe
  10. Gumi
  11 Gumi na Imwe
  .
  .20 Makumi Maviri
   
 5. T

  TWANJUGUNA Member

  #5
  Jun 17, 2010
  Joined: Jun 6, 2010
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  GIKUYU EMBU KAMBA
  MERU (eastern kenya bantus)
  1. imwe
  2. iiri, igiri,eri
  3. itatu, ithatu
  4. ina, inya
  5. itano, ithano
  6. itandatu, ithanthatu, ithathatu
  7. muanza, mugwanja.
  8. inana, inyanya
  9. kenda
  10. ikumi
  11. ikumi na imwe...
  30. miongo-itatu

  XLINGALA
  1. moko
  2. mibale
  3. misato
  4. minei
  5. misano
  6. motoba
  7. sambo
  8. lisa
  9. libwa
  10. zomi
  11. zomi na moko...
  30. tuku-misato

  kweli 1 hadi 5 ni sawa. kuanzia sita ndiko kunahitaji wanachuo waangazie.
   
 6. Kipala

  Kipala JF-Expert Member

  #6
  Jun 18, 2010
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 3,535
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 145
  Inaonekana wale wazeee Wanbatu asilia walipoanza matembezi walihesabu hadi tano yaani waliona vitu vitano vya kwanza kuwa muhimu hasa ili vinastahili jina la pekee; vingine waliridhika kuvitaja kwa maeneno ya kuunganika kama ule mfano wa juu "6= isano na imo (5+1), 7 = isano na ibere." Ila tu baadaye wengine waliona faida kuwa na majina ya ziada wakaopa kwa lugha nyingine. Katika Kiswahili tunatambua majina ya Kiarabu (sita, saba, tisa), na wataalamu watatambua labda pia athira ya lugha nyingine zilizokopesha majina yao kwa namba kufuatana na mazingira.
  Hapo ndipo asili ya 1-5 kufanana kote lakini 6-9 kuwa tofauti; mara majina ya kuunganishwa mara majina yenye asili ya kigeni.

  Kwa hiyo hata iile "kenda=9" ("miji - kenda) si neno la kibantu asilia bali kutoka wapi?
   
 7. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #7
  Jun 18, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,365
  Likes Received: 6,992
  Trophy Points: 280


  kweli nadhani kuna maana kubwa sana na hizo ndizo elimu ambazo wababntu Tunazimisi, ipo logic na labda ungeweza kuwa msingi mkubwa wa maendeleo yetu, kwa nini wababntu almost wote walikuwa na almost common names kwa namba moja mpaka tano?
   
 8. Kipala

  Kipala JF-Expert Member

  #8
  Jun 18, 2010
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 3,535
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 145
  Sina uhakika juu ya maendeleo.
  # Maana angalia yale mataifa yenye lugha za Kigermanik kama vile Kiingereza, Kijerumani, Waskandinavia na kadhalika. Wote wana muundo wa namba 12-12 za msingi. Waliiacha kwa sababu kwa hesabu ya kawaida na kuandika namba muundo wa kumi-kumi ilionekana afadhali. Lugha ya kituruki tangu kale ilikuwa na muundo wa 10-10 - ila tu haukuwasaidia sana kuwa mbele kimandeleo (namba zao 1 bir, 2 iki, 3 uch.... 10 on, 11 on-bi, 12 on-iki na kadhalika)

  #Tena tazama sku hizi kompyuta ambazo zote zinafanya hesabu wa namba 1 tu - maana yote tunayopata hapa kwenye skreeni ni mfululizo wa 1=Moja na 0=Sifuri inayobadilishwa na kompyua kuwa herufi, rangi, picha au nini.

  Lakini kwa utamaduni ni vema kuijua ya kwamba wazee Wabantu walikuwa na mtindo wa 5-5
   
Loading...