Heritage financing company limited inavyouza mali za watu walioshindwa kurudisha fedha za mikopo

Jamani heritage financing company limited iliyoko hapa Arusha Tanzania ni shida. Wanapenda riba kubwa, wanapenda kuuza mali za watu,wanapenda makesi mahakamani la kushangaza kupita kiasi mkurugenzi wa kampuni hii ni mlokole. ova
iv kuna aliewah shikiwa bunduki kwenda kukopa hapo....???

mbna kuna makampuni meng tu yanatoa mkopo si muende huko .....????
 
utakuta mkataba wa milioni kumi unajumlishwa na hiyo riba 6m mkataba unasoma umekopeshwa 16m unasainiwa hakimu akijua kinachoendelea, tena wana mahakimu wao kule wilayani,wakikatiwa laki 5 hazina risiti, wanagonga na mihuri ua jamhuri kabisa, wanajitia wanatoa huduma, hii si sawa (kwa sauti ya Nape)
Mwenye Loan agreement ya heritage financing company limited ,aiweke hapa. Mikataba yao huwa ni siri na serikali sidhani kama iliwahi kupitia hiyo mikataba yao ili kuiona uhalali wake. He Hakuna taasisi ya kuangalia hii mikstaba jamani. Heritage ni shida hapa Arusha
 
hivi wanalazimisha watu kwenda kukopa kwao kwa viboko
Heritage Finance limited ya hapa arusha wauza nyumba ya baba wa watu na kuibomoa iliyoko bomangombe wilaya ya Hai mkoa wa kilimanjaro. Baba huyo alikuwa hajakopa mkopo Heritage bali alikopa jirani yake wakati wa kuuza nyumba wakauza nyumba ya mtu mwingine. Huku arusha hii kampuni imekuwa kituko. Kungine inachukua hati ya nyumba inampa mke Wa mtu mkopo kupitia hiyo nyumba bila ridhaa ya mume na hati imeandikwa jina la mume. Tunaomba uchunguzi ufanyike kuhusu hujuma zinazofanywa na hii taasisi.
 
Jamani heritage financing company limited iliyoko hapa Arusha Tanzania ni shida. Wanapenda riba kubwa, wanapenda kuuza mali za watu,wanapenda makesi mahakamani la kushangaza kupita kiasi mkurugenzi wa kampuni hii ni mlokole. ova
Sasa kama hujalipa mkopo ulitaka wafannyaje? Wakati unachukua mkopo unakuwa umeshajua yote hayo..kwanini uje kulalamika baadae?
 
Pole walikuuzia nini mkuu, naona umedhamiria anguko lao.
 
Duh.. Yaani akope mwingine afu nyumba ya jirani iuzwe??! Hio haiwezekani, maana kama kweli hajakopa hao Heritage hawana document za nyumba yake, na huwezi uza nyumba bila documents za umiliki. Huyo nyumba yake ipo saalama, afuatilie tu
 
kama ndo hvi itafungwa kwakukosa wateja maana wamejiharbia soko
Itakosa Wateja vipi na Wateja ndio hao unasikia wanalia, wanaenda tu wanapigwa wanatoka wanalia...Wabongo unawajua unawasikia?
 
Itakosa Wateja vipi na Wateja ndio hao unasikia wanalia, wanaenda tu wanapigwa wanatoka wanalia...Wabongo unawajua unawasikia?
Hii ya zamani sana May 2018
Waziri wa Fedha juzi Disemba 2019 alikataza hizi Taasisi kujichukulia fedha kwa wananchi kwa Riba wazitakazo
Hata watu Binafsi sasa ni marufuku kukopesha bila leseni na kibali, Waraka upo huko Mahakamani kuanzia Mahakama za mwanzo, ni marufuku kutoza Riba bila ya Kodi
pia km km ni Mtumishi ni KUFUKUZWA KAZI
Kwa hiyo hivi vitaasisi vya mitandaoni, km niwezeshe nk ni Marufuku
Hao Heritage hawajakutana na mbogo, mm niliwafukuza Brack ana nikawalipa kupitia Mahakama ya mwanzo Principal tu hakuna cha Riba wala mama yake Saccos
 
nyumba inauzwa kwa amri ya mahakama, mahakama zetu huwa zinabariki mikataba hii haramu kwa nini?Nilisoma mahala ili mkataba uwe na nguvu ni lazima uwe halali. Riba 100% bot na tra wanajua hii!

TRA wanahusikaje na riba za mikopo?
 
Ukwaju,
Wamekataza tu, au pia wamekuja na ushauri wa Wananchi wafanye nini?

Maana hawa wote mpaka kwenda huko ku risk ni kwa sababu hakuna njia mbadala.

Sasa sioni ushujaa wowote kwa kukataza, ushujaa ungekuwa sasa msiende huku nendeni kule.

Sanasana hao Mawaziri wasiojua kiundani wanachopitia Wananchi wao wataishia kushauri "nendeni benki"
 
Ndumbayeye,
Ukikopa laxima ulipe ila Kwa riba ya 100% utalipaje? Heritage financing company limited ni tatizo.wachunguzwe
Unakubali vipi kuingia kwa mkopo wa riba ya 100% ??

Inakuaje unalikubali hili kwa hiyari yako mwenyewe na kusaini makubaliano hayo,

Kabla ya kumchunguza Heritage Financing!!

Inabidi tumchunguze kwanza huyu aliyekubali kuwa mteja wa huko kwa riba ya 100%

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom