Heri ya Mwaka Mpya 2021

Leslie Mbena

Verified Member
Nov 24, 2019
172
1,000
HERI YA MWAKA MPYA

Leo 14:30hrs 01/01/2021

Yakobo alivuka kuelekea nchi ya ugenini akiwa na fimbo tu lakini Mungu alimbariki kwenye nchi ya ugeni.Nawe pia yawezekana unaingia mwaka 2021 ukiwa huna kila kitu,huna kazi huna mtaji wala huna chochote,nakuombea Mungu akubariki akakuinue,na kukupa Mwaka mpya kwa ajili yake.

Mungu akupe Mwaka mwingine wa Maendeleo,Mwaka mwingine wa kumuabudu,Mwaka mwingine wa kumsifu,Mwaka mwingine wa kuthibitisha Uwepo wa Mungu siku zote za maisha yetu,Mungu akupe Mwaka mwingine wa Rehema,Mwaka mwingine wa Neema,Mwaka mwingine wa furaha itiayo nuru katika nyuso zetu,

Isaac hakumpa mwanae Yakobo shamba wala mali bali alimpa neno la Baraka,Nami leo nakutamkia Baraka za Mungu zimiminike kwako mwaka 2021,Mungu akupe Mwaka mwingine wa kuwa Mwaminifu mbele zake, Mwaka mwingine wa kujifunza na kurekebisha tulipokosea,Mwaka mwingine wa kufanya kazi, Mwaka mwingine wa kushuhudia Uwepo wa Mungu na Upendo wake kwako.

Luka 18:27 "Akasema yasiyowezekana kwa wanadamu yawezekana kwa mungu." Tume ahidiwa moyo mpya na maisha mapya Imeandikwa Ezekieli 36:26 "Mimi nitawapa moyo mpya nami nitatia roho mpya ndani yenu nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama." Ametuahidi kutusamehe dhambi zetu. Imeandikwa katika 1Yohana 1:9 "Tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote."

-Yawezekana Corona ilikupa hofu na umasikini 2020,Nikutie moyo na historia ya Bingwa George Foreman na Mohammed Ali.

Pambano lao la mwaka 1974 lilikuwa pambano kubwa lililoangaliwa na watu bilioni moja kwenye tv likijaza uwanja mzima pale Congo,Kinshasa likiishia round ya nane,Round zote tano za mwanzo Mohammed Ali alipigwa hasirushe hata konde kwa Bingwa George Foreman,Mohammad Ali akivumilia hadi round ya saba,akipigwa huku akimkumbatia George Foreman alimkumbatia George Foreman ili hasiendelee kupigwa,alitumia wakati huo kumwambia George Foreman "Is that all you got?"

George Foreman anasema,baada ya kuambiwa "Is that all you got" alianza kumfikiria upya Mohammad Ali kama si mpinzani wa kumpiga kama ilivyokuwa kwa Wapinzani wake wengine,George Foreman ambaye sasa ni muhubiri injili anasema "I thought Mohammad Ali is the same knock out victim"

George Foreman anasema, kujiamini kwake kulikwisha baada ya kuambiwa hivi ndivyo vingumi vyako unavyopigaga watu? "Is that all you got" na round iliyofuatia ikiwa ni round ya nane,Mohammad Ali alianza kumpiga Bingwa George Foreman kutokea kila upande hata akaanguka chini na kushindwa kunyanyuka katika round hiyo ya nane,

Baada ya round saba za kupigwa na Shetani na corona iliyoleta umasikini,Nakuombea round ya nane ukampige Shetani akaanguke na kushindwa kuinuka katika jina la Yesu Kristo wa Nazareth, Nakuombea baraka katika mwaka 2021,Uwepo wa Mungu ukakufunike,Roho wa Mungu akaende nawe kila hatua,Roho wa Mungu akakanyage kabla haujakanyaga,ukawe mshindi kwa maana Bwana Yesu tayari ametushindia.

Mungu akakulinde na kukuokoa sawa sawa na neno lake katika Isaya 49:25, "... Kwa maana nitateta na yeye atetaye nawe, nami nitawaletea wana wako wokovu."Mungu akakutimizie mahitaji yako sawa sawa na ilivyoandikwa katika Wafilipi 4:19, "Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu." Hatatunyima lililo jema. Imeandikwa katika Zaburi 84:11 "Kwa kuwa BWANA, Mungu ni jua na ngao, BWANA atatoa neema na utukufu. Hatawanyima kitu chema hao waendao kwa ukamilifu."

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854
 

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
38,313
2,000
Mkuu bandiko lote hilo bila kumtaja jiwe? Umeanza kumchukulia poa nini?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom