Heri ya kuzaliwa Dr. Martin Luther King

CWR2016

JF-Expert Member
Dec 14, 2017
2,760
6,294
Habari wana JF na Watanzania..

Siku kama ya leo mnamo tarehe 15 January 1929, alizaliwa mpambanaji wa haki za binadamu na mpinga ubaguzi wa rangi mmarekani mweusi Hayati Dr. Martin Luther King.

Alikufa tarehe 04 April 1968.

Ana historia ndefu na ni mmarekani mweusi aliyeacha "alama/legacy" kubwa sana ktk mapambano ya haki za binadamu.

Mimi namuona alikuwa na vipawa/vipaji vingi; mwanafalsa, mwanaharakati, n.k.

Nikushangaze kidogo....

Ukihesabu miaka hapo utaona aliishi kwa miaka 39 tu hadi kufariki.

Tuamini kwamba hakika tunayo nguvu na amini utafanikiwa ktk harakati zako na kufikia malengo.


Yeyote anayemjua zaidi au kwa lolote karibu useme hapa kumhusu huyu Legendary..
1. Elimu yake...
2. Ushupavu na uthubutu
3. Harakati...
4. U great thinker
5. Falsafa
6. Alianza lini harakati...
7. Vikwazo alivyowahi kukumbana navyo..
8. Na maisha yake mengine
...

Karibu..
 
Unamzungumzia Martin Luther muasisi wa kanisa la Lutheran almaarufu KKKT?
Huyu ambae alijipambanua kupigania haki za binadamu ni mwanae nafikiri.

Ndiye ninamzungumia hapa.
Unaweza kumuita Dr. Martin Luther King, Jr.
 
From Wikipedia...

Martin alizaliwa mjini Atlanta, Georgia,Marekani. Alikuwa mtoto wa mzee Martin Luther King Sr. ambaye pia alikuwa mchungaji na kiongozi wa kupigania haki za binadamu. Baba yake alimwita Martin Luther ili amheshimu huyu mtaalamu Mjerumani wa karne ya 16.

Aliwaongoza Waamerika Weusi kupingaubaguzi wa rangi uliokuwepo katika sehemu za USA mpaka miaka ya 1960. Katika mapambano hayo alifuata mapokeo ya Mt. Agostino katika Kanisa. Alieleza ya kuwa kila mtu amepewa naMungu heshima yake, hivyo sheria za nchi na serikali zinazovunja heshima hiyo si za haki. "Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu" (Mdo. 5:29).

Aliwaita watu kupinga ubaguzi hata dhidi ya serikali na polisi lakini bila kutumia mabavu. Watu waliongozwa na M. L. King waliandamana mahali pengi wakanyamaza wakipigwa na kukamatwa. Wakaingia katika hoteli,shule na vyombo vya usafirivilivyotengwa kisheria kwa watu weupe, wakasubiri mpaka polisi ilipoitwa na kuwakamata. Wakapokea adhabu na mapigo.

Baada ya miaka kadhaa mapambano kwa silaha hizo za amani yalishinda.Mahakama kuu ya Marekani na serikali kuu zilitangaza ya kuwa ubaguzi wa rangi katika mikoa mbalimbali hauruhusiwi kuendelea.

Mwaka 1964 alipokea Tuzo ya Nobel ya Amani kwa sababu ya kutetea haki bila ya kutumia mabavu.

Hata hivyo aliuawa kwa kupigwa risasi na mteteaji wa ubaguzi wa rangi mwaka 1968.

Baada ya hapo ujumbe wake ulizidi kukubalika na sheria mbalimbali zilibadilishwa.

Anahesabika kama mmoja wa watu wakubwa wa Mungu katika historia ya Kanisa.
 
Kila nikitizama Prophetic speech yake napata nguvu ya kusema kila binadamu ameletwa kwa kazi maalum na ni jukumu letu kutekeleza kabla ya kufariki
 
Kila nikitizama Prophetic speech yake napata nguvu ya kusema kila binadamu ameletwa kwa kazi maalum na ni jukumu letu kutekeleza kabla ya kufariki
Hivi alikuwa na ushawishi kiasi gani. Na bado alikuwa kijana kabisa. Aisee kweli Mungu katuumba kwa malengo kila mtu
 
Hivi alikuwa na ushawishi kiasi gani. Na bado alikuwa kijana kabisa. Aisee kweli Mungu katuumba kwa malengo kila mtu
Nadhani yote hayo ni kutokana na kujitoa kikamilifu nachokisikitikia ni kutokuungana na Malcom x

approach ya civil right movement ilikuwa tofauti na Nation of islam
 
Back
Top Bottom