Heri ya krimas na mwaka mpya familia ya Ukawa

Victor wa happy

JF-Expert Member
Apr 24, 2013
11,660
11,641
Heshima kwenu ndugu zangu katika mtazamo wa mabadiliko na mageuzi ya nchi yetu

Mchongo wetu nyuma ya keyboard ni mkubwa sana tumeweza kujenga hoja na kuwasambatarisha wapinzan wetu wa kifkra na mawazo ambao wao uhafidhina bado ni chaguo lao

Kizazi cha kina Lema, mnyika, Ben saanane, mdee, mtatiro, kafulila na wengine walishahamia kwenye majukwaa halisi ila naamini tunawawakilisha vema maana hatuwapi nafas watesi wetu kushikilia mjadala

Ushirikiano wetu, humu ndivyo ulivyo kwenye maisha halisi huko mtaani

Mwaka huu tuliwazidi kila kitu wapinzani wetu, pamoja na kuwa wanaingizo jipya pale magogoni, ambaye grafu yake ya kukubalika imepukutika sana kuanzia kipind cha bunge la bajeti

Mimi naamini vuguvugu letu la mitandaoni linachangia karibu nusu ya harakat za upinzani nchini

Niwapongeza pia viongozi wakuu wa chama wakiongozwa na freeman mbowe, maalimu seif, tundu lissu, mbatia, lowasa, vicent na viongozi wote wakuu wa vyama

Tuendelee pia kumuombea ndugu yetu, apatikane akiwa salama, yale tuyofikiria kichwani yasiwe ya kweli, God can save him
Pia tusimsahau brother Lema huko ndani kwasababu anawakilisha mitazamo harakat zetu za kila siku


Mao Zedong

Aliwahi kusema

POLITICS IS WAR WITHOUT BLOODSHED WHILE WAR IS POLITICS WITH bloodshed


Nawatakiwa heri. Ya kirismas na mwaka mpya nikiwa napaki vizur begi langu kwenda kijijin kumwona bibi yangu kipenzi

Nitarudi humu January panapo uzima

Mungu awabariki wote hata wapinzan wetu katika mabadiliko
 
Merry chriistmas too, happy new year too.
Karibu wengine tushfika kitambo tunaanda mbuzi huku tukifanya sala
ya
# Bring back Ben
 
UKAWA kuna mambo hamyaelewi mfano ni swala la Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ambao huwa mnasema hamuuelewi ulivyokaa huo wa serikali mbili uliomchanganya hata warioba na tume yake.

Muungano huo ulifanyika kwa Udongo ulichukuliwa pande mbili ukachanganywa kwenye chupa wazee wakala yamini ya kutouvunja huo muungano hivyo hivyo ulivyo milele,wakapiga madua na manuizo ya kiutawala kwenye hiyo chupa.Kwa hali ya kawaida ungetarajia ile chupa iliyochanganywa udongo iwe jumba la makumbusho kama kumbukumbu .Haipo.Ilifanyiwa mauchawi ya kitawala ikaenda kutupwa katikati ya vilindi vya bahari.Ukitaka kuuvunja hutakiwi kutumia porojo za kitoto za sijui rasmu ya kitoto ya warioba!!! Katafute ile chupa uibomoe.Huo UKAWA wenu haujui hili.

Ndio maana wapinga muungano huu kama ulivyo wote hakuna anayeweza kuwa Raisi awe wa Zanzibar au muungano wote waliojaribu hawajawahi fanikiwa kuwa maraisi akiwemo SEIF SHARIFF hamad,LOWASA,warioba,mbowe,SLAA nk Uwe CCM au nje ya CCM ukiupinga muungano huu wa serikali mbili hushiki uraisi popote Uraisi wa muungano wala wa Zanzibar.

HUO MUUNGANO NI KISIKI.Ukitaka kushika uraisi lazima utake usitake ukubaliane nao kama ulivyo.HUU UJUMBE WAFIKISHIE UKAWA wote wanaodhani huu muungano ulivyo ni wa kuuchezea.Ukitaka kuubomoa unakubomoa.Ndio maana safari hii LOWASA na SEIF walikubaliana SEIF ashike uraisi Zanzibar LOWASA ashike uraisi muungano halafu wabomoe muungano huu wa serikali mbili.Kilichomkuta SEIF zanzibar haji kisahau.Na lowasa hana hamu.

HUO UKAWA ni umoja wa watu mbumbumbu wasiojua uchawi wa utawala.HILO LA KUTAKA KUVUNJA MUUNGANO ni kigezo kiukuu cha UKAWA kutoshika dola HATA WAJIZATITI VIPI.Muungano sio wa kugusa ndio maana hata CCM Haiugusi sababu wanaujua mziki wake wakiugusa kutaka kuufumua.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom