Heri ya CHADEMA wanachukua uamuzi mgumu

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,840
Ikiwa imebaki miaka miwili kufanyika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015, vyama vya siasa vimeanza kujiandaa ili kuhakikisha vinashinda uchaguzi huo na kushika dola.

Miongoni mwa vyama vinavyojiandaa, ni Chadema ambacho kimeanza kujitazama na kuwajibishana ili kujiweka sawa, kisha kuunda timu madhubuti ya ushindi mwaka 2015.

Kamati Kuu ya Chadema, hivi karibuni iliwavua nyadhifa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe na Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk Kitila Mkumbo kwa tuhuma za kuendesha mambo yanayodaiwa kutaka kukisambaratisha.

Kuchukua uamuzi kama huo kwa Chadema si mara ya kwanza. Itakumbukwa kwamba shoka kama hilo liliwahi kumwangukia aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wake, marehemu Chacha Wangwe aliyevuliwa wadhifa wake na mauti kumkuta siku chache baadaye.

Rungu kama hilo liliwahi kumwangukia aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Amani Kaborou ambaye sasa ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma. Pia David Kafulila alivuliwa cheo akatimkia NCCR-Mageuzi.

Mapema mwaka huu, Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema (Bavicha), Juliana Shonza na wenzake akiwemo Mtela Mwampamba na Habib Mchange walifukuzwa uanachama katika chama hicho kutokana na kutuhumiwa kukisaliti.

Inaweza kuelezwa kuwa hiyo ni migogoro, lakini pia ni uamuzi mgumu wa kujisafisha na kujiweka sawa ili kuingia katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 bila vikwazo.

Hata hivyo, kwa baadhi ya vyama vya siasa suala la kuchukua uamuzi mgumu wa kujisafisha limekuwa jambo gumu na uamuzi huu wa Chadema unapingwa kwa sababu mbalimbali, ikiwamo ya kukiuka misingi ya demokrasia.

Mathalan, Chama Cha Mapinduzi (CCM), tangu kilipotangaza kaulimbiu yake ya kujivua gamba mwaka 2011 mpaka sasa hakijafanya lolote, badala yake kimebaki tu kulalamika jukwaani na kushutumiana wao kwa wao.

Ukiacha Mwakilishi wa Kiembesamaki, Mansour Yussuf Himid aliyetimuliwa kwa madai ya kushindwa kutekeleza wajibu kwa wanachama na kutokutekeleza ilani ya chama hicho ya mwaka 2010/2015, hakuna kumbukumbu nyingine ya chama hicho kujivua gamba.

Ningetarajia kuona CCM kwa nafasi yake kama chama tawala ikionyesha mfano kwa kuchukua hatua dhidi ya wanachama na viongozi wasiotimiza wajibu wao, badala ya kutuonyesha sinema za bure za kulalamikia watendaji wake kwenye mikutano ya hadhara.

Mathalan, malumbano yanayoendelea baina ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye na baadhi ya mawaziri kwa kuwaita kuwa ni mzigo na kupendekeza wang’olewe ni sawa na kujikausha maji ukiwa ndani ya bahari ukioga. Mbona ilikuwa ni rahisi kwa CCM kumaliza suala hilo kwenye vikao vya ndani ambavyo mwenyekiti, Rais Jakaya Kikwete ndiye aliyewateua mawaziri hao?
 
Maamuzi magumu hata jambazi anafanya kuvamia kwenda kuiba.
 
Back
Top Bottom