Heri tisa shika ya Lowasa kuliko kumi nenda rudi ya mizengo pinda!

Munambefu

JF-Expert Member
Jun 24, 2012
2,608
6,503
Niweke kumbukumbu sahihi kwamba siungi wala sitetei ufisadi.Lkn kwa mizengwe ya Mizengo Pinda bora Lowasa alikuwa na ujasiri,uwezo,na kauli ya kimamlaka juu ya mambo mbalimbali ktk nchi.
 
Tehe!tehe!tehe! Aah!kwa na akili zenu zote wakuuu bado mnataka kumsifisha mamvi?
 
Munambefu umenena.Mh. Mizengo Pinda amepoa mnooooo! Anaonekana ni mtu wa kuogopa sana na kabla hajatoa tamko, huenda anaanza kuhisi hoja zake zitakataliwa, kuokosolewa ama hazina mashiko na hiyo humsononesha sana. Lakini najiuliza anabanwa na nani asiwe huru kifikra maana anaonekana kutojiamini? Nampenda sana na namheshimu Mh.Pinda ila ukweli ndio huo.
 
hili liko wazi kabisa wala halifichiki, Lowassa is a gentleman bana. Tena nafikiri hapa tanzania hatutapata kiongozi kama yeye mwenye uwezo, maamuzi, na muwajibikaji. Sikatai hata kama tutamtuhumu kwa ufisadi but si fisadi kuliko JK. Hivi mnayakumbuka maneno yake kwa muheshimiwa raisi kwamba 'hivi mh. rais ni kitu gani nilichokifanya ambacho wewe hukijui?'
Tusiunderestimate hii sentensi wakuu Lowassa alikuwa ma meseji kali mno kwa taifa hili kupitia hii kauli na magamba waliifukia kwa kuhofia watu kuendelea kuijadili zaid.

Pasi kuwa na itikadi yeyote ile still CCM wakimsimamisha EL lazima achukue hii nchi na mimi nitampa kura yangu. Fikiria yeye alizaliwa katika familia tajiri sana na elimu aliyopewa aliitumia vizuri sana hata kama anaiba not kwa extent ya wanayoibia akina JK na mwanae jamani. huyu tayari alikuwa na pesa so hakuhitaji kuchakachua sana kama wengine. Naamini angekuwa yy ndiye pm lazima suluhu ya madaktari ingekuwa imepita mkuu.

kumbuka EL alisimamia sera ya ujenzi wa shule za kata na ikafanikiwa huyu pinda yeye ni kama mtu aliyepewa bustani ambayo tayari imeshapandwa mboga amwagilie na kuvuna na kupata sifa wakati aliyeandaa shamba mwingine mbegu , mwingne na hata kupanda hadi yakazoea ardhi.
 
Naunga mkono hoja, Bora Lowassa anapiga dili za hela kuliko huyo mfipa mwanga wa sumbawanga anayewekeza kwenye damu za watu na kusema liwolo na liwe
 
Mizengo alikuwa TAMISEMI chini ya Lowasa so alijua kila kilichokuwa kinatokea, sasa yaliyompata EL Mizengo anakijua maana ni mmoja wa waliomkaanga ili wao wapone......na pia ni mwoga akimwaga unga hajui la kufanya.
 
Kwa mimi binafsi, pamoja na kwamba sipendi kujipendekeza, sijaona kiongozi CCM. Mamboa yanaenda kama gari iliyokata trearing tena haina hata lock. Wengine wezi, wengine hawajui wanachofanya, wengine wachawi tu, yaani basi tu. 2015.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom