Heri nisiwe DIWANI kuliko kuwa GAMBA... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Heri nisiwe DIWANI kuliko kuwa GAMBA...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by VUTA-NKUVUTE, Jun 4, 2012.

 1. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #1
  Jun 4, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,868
  Likes Received: 6,566
  Trophy Points: 280
  Mwishoni mwa juma nilikuwa nyumbani nilikozaliwa-Visiga,Kibaha.Nikiwa sina hili wala lile,nikapata ugeni nyumbani kwetu.Wakaja jamaa watatu wakidai kuwa na ujumbe wangu.Nikawakaribisha.Salamu zikafuata halafu mazungumzo.

  Wakaniarifu kuwa,wao wameagizwa na wazee na vijana wa kata yangu waje kuniambia uamuzi wa wanakata juu ya nani anatakiwa kuwa Diwani wa Kata yetu hapo 2015.Wanataka kumandaa kabisa.Wanadai wamemchoka Diwani aliyepo kwakuwa hakufanya lolote kwa miaka yake 12 aliyokuwa madarakani.Pia,kwakuwa ni Darasa la saba.Wanamtaka msomi na mwenye uchungu na maendeleo ya Kata.Wameniona mimi nafaa.

  Wageni wangu wakanieleza mchakato mzima uliwafikisha katika uamuzi wao huo.Mwishoni nikawauliza: kwa chama gani? Wakanijibu: CCM.Mwili wangu ukasisimka kama nimepigwa shoti ya umeme.Sikuwafokea.Nikawajibu kistaarabu tu: Ni heri nisiwe Diwani kuliko kuwa Gamba.Walionyesha kushtuka.Hawakuchelewa kuaga.

  Eti WanaJF,nimekosea hapo?
   
 2. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #2
  Jun 4, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 1,115
  Trophy Points: 280
  Nadhani kwa kutii kile moyo wako unapenda, haujakosea.
  The unseen is illustrated by the seen.
   
 3. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #3
  Jun 4, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  mkubwa!ulikosea kitu kimoja,kwanza ungewaanzia hapohapo u-M4C(ungewavua magamba ukawavalisha magwanda) alafu mwisho ndio ungewapa hilo jibu,il wakirudi huko kwa waliowatuma washangae jamaa waliondoka wakiwa gamba na wamerudi na magwanda
   
 4. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #4
  Jun 4, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  ​Uko sahihi mkuu! watu wa pwani wanahitaji ukombozi wa fikra, ipo siku na wao wataikataa ccm
   
 5. N

  Ngoshanzagamba Member

  #5
  Jun 4, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Hongera kwa kumkana shetani na ghiliba zake tena ukamshuhudia Mungu mbele ya watu wa mataifa....Ila inekuwa heri kama ungefanya yafuatayo..
  1. Kukubaliana nao halafu uwaombe ukae nao mjadili mstakabali wa kata yenu- Naimani wangekubali hilo kwani wwe umewakubalia kwenye lao la kuwa kiongozi wao.....
  2. Hapa ungapata nafasi ya kuwa maana ya SISI TUNA MUNGU NA WAO WANA UFISADI wakiwa wote, pamoja na ugumu wa mioyo yao watu wa PWANI, naimani wasingeeuka nyuma ili wawe jile la CHUMVI bali wanekuamini na kukufuata wewe Jabali lao.. Hapo ukombozi unetimia....

  Ila hongera sana kwa kile umekifanya...
  2.
   
 6. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #6
  Jun 4, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  usichangamane nao shetani naye ananguvu ila big up
   
 7. mashami

  mashami Senior Member

  #7
  Jun 4, 2012
  Joined: May 8, 2012
  Messages: 183
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  naomba uongoze katika kutoa elimu ya uraia,pia m4c maana hao wananchi wahitaji ukombozi wa kifikra
   
 8. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #8
  Jun 4, 2012
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Hujakosea, kama kweli wanakutaka watakukubali kwa chama chochote.
   
Loading...