Heri kuoa kwenye familia masikini au kuoa kwenye familia iliyokuzidi kipato?

Kifaru86

JF-Expert Member
Apr 22, 2017
1,734
3,802
Kuna sehemu kulikuwa kuna mjadala mkubwa tulikuwa tunazungumzia suala la kuoa tukawa tunangalia aina mbili za familia faida na hasara.

Mwanaume kuoa familia ya kitajiri ambayo imewazidi kwenu uwezo na kuoa familia maskini wapi kuna afadhali?
 
Ukioa familia masikini kila siku ndugu wa mwanamke shida haziiishi ukoo mzma unakutegemea wewe mara leo hivi mara kesho vile.

Ukioa familia yenye kipato cha juu sana kuliko ninyi ujiandae maana kuna fedhea hatari huko mbeleni ndoa yako itakuwa inaendeshwa na mama mkwe pia tegemea ndugu zako kuzalauliwa.
 
Kwanza unachotakiwa Kujua kama mtoto wa kiume ni kwamba hauoi Familia ya mtu ila unaoa Mwanamke.

Kuhusu Suala la kutafuta ni wajibu Wako Mtoto wa Kiume Kukaza Tako Mambo Yaende Mpate mafanikio Pamoja.

Ikumbukwe Pia imeandikwa Mwanaume atakula kwa jasho.Kwa Maana ya Utafutaji wake na Sio Kutengemea Kitonga kutoka katika Familia ya Mwanamke.
 
Umaskini na utajiri umeingiaje kweny suala LA kuoa? Basi utakuwa unataka kunyanyasa mtu au unyanyaswe/kitonga?

Andaa maisha yako,huo umaskini na utajiri sio wenu
 
Kuna sehemu kulikuwa kuna mjadala mkubwa tulikuwa tunazungumzia suala la kuoa tukawa tunangalia aina mbili za familia faida na hasara.

Mwanaume kuoa familia ya kitajiri ambayo imewazidi kwenu uwezo na kuoa familia maskini wapi kuna afadhali?
Kwa sasa pumzika kidogo, jiepushe na mapenzi kabisa, akili ikae sawa, upone majeraha ndio urudu sasa ulingoni
 
Back
Top Bottom