Heri James: Waliokamtwa na rushwa UVCCM Mbeya washughulikiwe, aonya wafuasi wao

blix22

JF-Expert Member
Jun 23, 2013
213
645
*HERI JAMES: WALIOKAMTWA NA RUSHWA UVCCM MBEYA WASHUGHULIKIWE, AONYA WAFUASI WAO*

Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Heri James ametoa msimamo mkali dhidi ya kundi la vijana wanaodaiwa kujitokeza kutetea watoa rushwa ambao wanashikiliwa muda huu.

Inadaiwa kuwa Vijana hao walikuwa wakitaka kuachiliwa huru kwa Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mbeya na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Singida waliokamatwa kwa rushwa.

Heri James amesema kuwa hajafurahishwa na kundi dogo la vijana wanaobeza juhudi za kukamatwa kwa viongozi hao na badala yake wanataka waachwe.

*"Nasikia kuna kundi flani la vijana wanaolalamika kukamatwa kwa Mashango na Nyiraha najua watakuwa ni wanufaika wa rushwa hizi, sasa ngoja tumalize uchaguzi huu ili nao tuwawajibishe mmoja baada ya mwingine" alisema Heri James*

Aliongeza kuwa *"lazima watu wote wazingatie misingi ya viongozi wakuu wa chama wa kuichukia rushwa,hivyo yeyote anayepingana na misingi hiyo, si mwanachama halisi wa CCM kwani anaweza kuwa pandikizi"* Alisema Heri James.

Mwenyekiti huyo alisema kuwa inadaiwa vijana hao walikuwa wakipanga mikakati yao wakiwa Dodoma carnival na kutaka kufanya vurugu.

Baadhi ya watuhumiwa wanaotajwa kuunga mkono wala rushwa ni Shaban, Komba na Kidutu ambao wameonekana kuwa vinara wa kundi hilo.

*"Harakati zao zitawapeleka pabaya kwani bado ni vijana,na kama wanatumiwa na watu basi wajitazame kama wao"* alisema

Amewataka vijana hao kuacha mara moja harakati hizo na kuacha sheria ichukue mkondo wake kwa waliokamatwa.

Mwenyekiti huyo aliyasema hayo akiwa na Naibu Katibu Mkuu mara tu baada ya kumaliza kikao cha kamati ya Utekelezaji ya UVCCM Taifa jijini Dodoma ambacho alieleza kuwa kimejadili na kuazimia mambo mbalimbali kuelekea uchaguzi huo.
 
Kumbe ccm wanaichukia rushwa kwa kuwa viongozi wao wakuu wanaichukia na sio msimamo /miiko ya/ wa chama
 
Back
Top Bottom