Hembu Msome huyu Jamaa - Dr. Pona

Ndallo

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
7,619
4,292
Wakuu leo kuna jamaa kapita ofisini kwangu akajitambulisha kua yeye ni Dr. Pona toka India na yeye anatibu magonjwa sugu! Lakini chakunishangaza katika form yake aliyoniachia kuna gonjwa number 12 isome hapo chini halafu toa ushauri wako.

Dr. Pona.jpg
 
Wajinga ndio waliwao, atapata watu, japokuwa ni juzi tu riport ilitoka jinsi babuwaloliondo alivyoua watu
 
Ungemuhoji vizuri kuhusu hiyo pointi namba 12 na kama anaweza pia kumfanya mtu mrefu awe mfupi,Ungetuandikia. Maana ni kitu hakijawahi kusikika katika maisha hasa kwa maumbile ya mtu kuzaliwa nayo
 
Ungemuhoji vizuri kuhusu hiyo pointi namba 12 na kama anaweza pia kumfanya mtu mrefu awe mfupi,Ungetuandikia. Maana ni kitu hakijawahi kusikika katika maisha hasa kwa maumbile ya mtu kuzaliwa nayo

Nimemuuliza lakini akaniambia sio rahisi kumfupisha mtu mrefu!
 
Si mmeona mpaka number zake za simu pamoja na barua pepe yake? yuko hapa A-Town maeneo ya Moshono!
 
A quack, a charlatan.

Ganga ongo.

Watu washaona Babu wa Loliondo kachuma wanataka kufuata nyayo.
 
Teh teh teh,Haya haya watu wafupi,mjitokeze,hatimaye shetani kawasikia..kama Fatuma,Zubeda Irine na Zawadi walikukataa,sasa lazima wakae!
 
Namba saba inawezakunihusu mie maana kila siku na itwa Sura Ngumu kweli nimeamini wajinga ndio waliwao.
 
kwa wale wenye DSTV kuna kipindi kinaitwa SCAM CITY kipo Channel ya NAT GEO, wiki iliyopita walionyesha india ndio centre ya medical scam duniani. yaani kama unavyoona hapa bongo mtu anapanga frem kuuza vitu ndio india kulivyo na madaktari feki kila kona wamepangisha fremu. yule mtangazaji alipata hadi cheti chake cha kifo kilichotolewa na registered hospital ili familia yake wakalipwe insurance. India madaktari fake ni wengi kuliko registered doctors.
 
Umenisaidia sana mkuu,nina tatizo sugu kati ya hayo,nitamtafuta! Imani huponya!
 
Back
Top Bottom