Wanafunzi wa St. Joseph Tawi la Boko waulalamikia Uongozi wa Chuo kwa kuwataka walipe ada wakati huu wa #COVID19

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,802
11,961
Wanafunzi wa Chuo hicho Tawi la Boko wameulalamikia Uongozi wa Chuo hicho kwa madai kuwa wamepewa taarifa ya kutakiwa kulipa karo ya Chuo ilhali masomo yakiwa yamesitishwa kutokana na #CoronaVirus

Inadaiwa kuwa Uongozi wa Chuo umetishia kuwarudisha mwaka wa masomo kama hawato tekeleza maagizo ya kutakiwa kulipa fedha hizo

Aidha, chuo hicho kinadaiwa kuwa kimefungua Makundi ya WhatsApp kwa ajili ya kuendeleza masomo kwa njia ya Mtandao lakini Wanafunzi wanadai hakuna kinachoendelea kwenye makundi hayo
 
Sasa malalamiko ya nini wanafunzi, hamjashikiwa bunduki kulipa hiyo ada, unalipa ukiondoka na mnyama covid19 inakuaje? Hakuna kulipa, acheni kuwa na mawazo mgando, hiyo elimu mnayoipigania mkija kitaa hasa awamu hii ndio mtajutia muda wenu.
 
  • Thanks
Reactions: rr3
Hivi vyuo vinazngua kinoma, kila chuo na utaratibu wake kwa mfano chuo cha uhasibu arusha eti bado kinaendeleza masomo online study .
Lakini ninavyojua karo hulipwa kwa asilimia 100 mwanafunzi anapojiunga. Je, hawa wanadai karo ya nyongeza? Je, kusoma online wanafunzi wanalazimishwa? Maana mitaala iliyopo ni face to face, hivyo masomo ya online ni nyongeza tu.
 
Mama ndalichako ingilia kati
Hawezi kuingilia kati unless wanadaiwa karo ya ziada. Maana mwanafunzi anatakiwa kulipa mara moja karo ya mwaka. Kama walikubaliana na chuo kulipa kwa awamu, hiyo ni jukumu la mwanafunzi kutimiza wajibu wake.
 
Hapo akili zao zinawaza pesa tu, hawana muda wa kufikiria ni kwa namna gani huu ugonjwa umeathiri shughuli nyingi za kiuchumi.
Mimi sipendi kutetea mtu ila ningependa huyo mleta lalamiko anijibu kama hiyo karo wanayoitaka ni ziada au karo ya mwaka wa masomo. Karo hutakiwa kulipwa mwanzoni kabla mwanafunzi hajaanza masomo. Lakini kwa huruma ya vyuo, hukubali kupokea kwa awamu mbili au zaidi.

Hata kama kuna tatizo la Corona lazima makubaliano yatimizwe maana hivi ni vyuo vya binafsi ambavyo havipati ruzuku kutoka serikalini, kwa mantiki hiyo hulipa walimu na wafanyakazi mishahara kutokana na karo. Je, karo isipolipwa walimu wao watalipwa kutoka wapi?

Pili naona vyuo vingi vinafundisha online kama kuwasaidia wanafunzi wao. Hata serikali kupitia TIE wanaanza kutoa mafunzo kupitia TV na Redio kwa wanafunzi wa Primary na Secondary
elimu.jpeg
 
Back
Top Bottom