HELP: Mtaji wa milioni 2 ndani ya dar VS mshaara wa laki 6 kwa mwezi mkoani Rukwa.

MYWEWE

Member
Jul 20, 2012
83
100
habari zenu wakuu.. naomba msaada wa mawazo, nko njia panda kidogo.
Mimi ni kijana 25yrs nlianza maisha ya kujitegemea kama miaka 2 iliopita baada ya kumaliza elimu yangu ya diploma, makazi yangu ni dar es salaam., katika shughuli zangu za vibarua nliweza kupanga chumba na kunua kila kitu kinachotakiwa ndani,, nakujiwekea balance ya 2M, kutokana na msukosuko wa uchumi wa nchi yetu kwa sasa wachina wamerudi kwao ivo sina shughuli yoyote ya kuniingizia kipato kwa sasa..., Ivo nkawa nafikilia nianze biashara yyte kwa balance angu hii ya 2M, wazo langu la kwanza ilikua nifanye biashara ya kibanda cha chips pia ntafute mtu wa kunisaidia sababu sina uzoefu wa biashara hii, pili nifungue center niuze vifaa vya simu na umeme. NOTE (SIJAWAI FANYA BIASHARA YOYOTE KATIKA MAISHA YANGU)..,
Nkiwa bado nafikilia wazo langu ili la kufanya biashara, last week nmepata kazi kampuni flani nmepangiwa niende mkoani Rukwa kama kituo changu cha kazi.., ntapewa mshaara wa laki 6 kwa mwezi contract ya mwaka mmoja, nasita kukubali offer hii sababu naona mwaka mmoja ni mfupi sana kuanza upya makazi sehemu nyingine, nawaza niondoke na vitu vyangu vya ndani "naona ni ghalama kubwa sana kuvisafirisha mpaka rukwa", au nitafute kijana akae apa aniiangalizie chumba ilo pia naona ntaongeza ghalama ya kulipa kodi sehem mbili.
.
.
Najua umu kuna vijana wenzangu na watu wazima wenye ushauri mzuri na mawazo mapana zaidi ya kimaisha., naomba ushauli wenu lipi ni jema kati ya hayo, au nifanye jambo gani sahihi zai..
NAWASILISHA.
 
Katika maisha yako siku zote jitahidi kufanya kile ambacho moyo wako unataka! Naamini wewe mwenyewe kati ya hivo vitu viwili kipo kimoja ambacho moyo wako unakitaka zaidi, cha kufanya sikiliza moyo wako, Fanya kile unachokipenda utafanya kwa ufanisi na kwa juhudi kubwa
 
Nenda kwenye mshaara wa laki 6 uko mkoani. Ndio sehemu sahihi kwenda kuwekeza kwenye biznes ya mazao ya chakula na nafaka.
Kwa mtaji na kiasi chako icho kinatosha sana kwa hii idia ya mazao tena kwa mkoa tajwa hapo.
Kipindi cha mkataba wako wa mwaka mmoja ndio mda wakujivunza kwenye secka hii mkuu.
Piga ndege wawili kwa jiwe moja fanya ivyo kiongozi.
Hutajuta kwa huo mkoa ni fulsa sana kwa kiasi icho.
 
Katika maisha yako siku zote jitahidi kufanya kile ambacho moyo wako unataka! Naamini wewe mwenyewe kati ya hivo vitu viwili kipo kimoja ambacho moyo wako unakitaka zaidi, cha kufanya sikiliza moyo wako, Fanya kile unachokipenda utafanya kwa ufanisi na kwa juhudi kubwa
shukran.
 
Nenda kwenye mshaara wa laki 6 uko mkoani. Ndio sehemu sahihi kwenda kuwekeza kwenye biznes ya mazao ya chakula na nafaka.
Kwa mtaji na kiasi chako icho kinatosha sana kwa hii idia ya mazao tena kwa mkoa tajwa hapo.
Kipindi cha mkataba wako wa mwaka mmoja ndio mda wakujivunza kwenye secka hii mkuu.
Piga ndege wawili kwa jiwe moja fanya ivyo kiongozi.
Hutajuta kwa huo mkoa ni fulsa sana kwa kiasi icho.
iko poa, shukran.
 
Mimi ningekushauri uuze vitu ulivyonavyo,then kaanze maisha huko..sababu unaweza kufungua biashara na hiyo 2m na biashara isiende vizuri..
shukran..
but naona nkiuza afu nkanunue vitu vya ndani kule, asa vifaa vya Electronics, cost ake ni kubwa sana mkoani.
 
shukran..
but naona nkiuza afu nkanunue vitu vya ndani kule, asa vifaa vya Electronics, cost ake ni kubwa sana mkoani.
1. Nenda kaongeze mtaji wako kwa kuweka savings kwa mshahara utaokuwa unapata.

2. Huwazi au hufikirii sawa kwa sababu unashindwa kupata suluhisho kuhusu vitu vyako vya ndani. Mpe ndugu akuhifadhie lakini pia nenda kaulize kusafirisha itakuwa shs ngapi. Usiseme ni ghali lakini hujui bei yake.

3. Hiyo biashara unayotaka kuifanya, utaifanya ukiwa huko unapokwenda.

4. Kawaida ukipata kazi kwenye Kampuni au NGO na wakakuajiri sehemu ambayo sio wilaya au mkoa wako, huwa wanatoa relocation fee na hela ya kujikimu mpaka upate Nyumba. Tumia hiyo hela kuhama.
 
Usiuze Electronics devices zako usiuze kabisa. Kitanda, godoro, sijui meza uza. Fedha utakayopata beba vifaa vyako vya Electronics hadi kwenye standi ya fuso pale Jangwani (sijui kama bado wapo) pakia mzigo mkutano..... Rukwa. Kutokea hapo fuata mawazo ya Brother kawombe hapo juu
 
Biashara kwasasa kuifanya bila back up itakusumbua kisaikolojia Sana, jikite kuomba kazi tena biashara ifanye kama nanma ya kuingiza faida ya kula,na nakushauri usiwe na anuani rasmi,yaani kuwa machinga tu,wakati ukisubiri kazi za hapa hapa dar au atleast mikoa karibu na dar,

Huko rukwa mbali sana,afu kahela kenyewe unakokafukuzia ni kadogo, ukijitahidi sana kukasave utabaki kama na 3m au 4m,Otherwise ingekuwa ni permanent,afu Rukwa utapauka mkuu,komaa tu Dar as salaam,hiyo mivitu ya ndani ndo huwa inasumbua Sana baki nayo tu.
 
Cha kwanza jiulize wewe unaamini nini katika kufikia mafanikio cha pili jiulize hayo mafanikio unataka uyapate lini na wapi Sasa hapo ndio unakuja na hitimisho kwamba:-

Kama unaamini unaweza kutoboa kwa kujiajili pasipo kuajiliwia amini inawezekana na ninavyoijua dar kwa capital ya 1.5 mil unaweza kuzalisha ukapata kiasi zaidi ya laki 6 unayotaka kuifuata mkoani kama ukiweka mipango madhubuti na kujituma sana.

Kama unaamini unaweza kutoboa kupitia kumtumikia mwajiri wako itabidi uamue kwenda mkoani au kuendelea kutafuta kazi nyingine hapo dar

Mwisho chagua sehemu sahihi kwako unayoamini wewe ukiishi hapo ni lahisi wewe kufanikiwa kati ya Dar au mkoa mwingine
 
Back
Top Bottom