Hello

Gizzo

Member
May 8, 2008
6
0
kanisa katoliki laipa shavu serikali ya JK
JK akiwa na Askofu Norbert Mtenga na Naibu Waziri wa Miundombinu Dk Milton Mahanga na msafara wa baba Askofu Mtenga leo Ikulu jijini Dar

Na Mwandishi Maalumu


KANISA Katoliki limeishukuru Serikali ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa ushirikiano ambao Serikali hiyo imekuwa inatoa katika kuendeleza shughuli za huduma na miradi ya Kanisa hilo.



Kanisa hilo pia limesema kuwa halina tatizo lolote na Serikali na limeisifia uhusiano mzuri ulioko kati ya Kanisa hilo na Serikali, likisisitiza kuwa litaendelea kushirikiana na uongozi wa Rais Kikwete katika kutoa huduma mbalimbali kwa Watanzania.

Shukurani hizo zilitolewa Ikulu, Dar es Salaam, jana, Alhamisi, Julai 23, 2009, na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Kanisa Katoliki la Songea, Askofu Nobert Mtega wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais Kikwete.

Askofu Mkuu Mtega alikuwa sehemu ya ujumbe wa Shule ya Chekechea ya Mtakatifu Scholastica iliyoko Ukonga, Dar es Salaam, na uongozi wa Shirika la Watawa la Benedictine la Masista wa Mt. Agnes Chipole wa Songea, ambao ulikutana kwa mazungumzo na chakula cha mchana na Rais Kikwete kumshukuru kwa mchango wake katika kuendeleza shule hiyo.

Pamoja na kwamba iko Ukonga, shule hiyo ya Mt. Scholastica inaendeshwa na Shirika la Watawa la Benedictine la Masista wa Mt. Agnes Chipole lililoko chini ya Jimbo Kuu la Kanisa Katoliki la Songea ambalo kiongozi wake ni Askofu Mkuu Mtega.

Ujumbe huo wa shule hiyo ulimshukuru Rais Kikwete kwa mambo mawili makubwa ambayo kiongozi huyo ameifanyia shule hiyo ambayo pia ni mlezi wake.

Rais Kikwete aliahidi mwaka 2002 na tayari amefanikisha kuipatia shule hiyo viti 100, na eneo la ujenzi wa ujenzi wa shule za msingi na sekondari na zahanati la ekari 16 (sawa na hekta sita).
Eneo hilo ambalo awali lilikuwa mali ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), pia litatumika kujenga nyumba ya watawa wa shirika hilo, iliyobomolewa katika eneo la Ukonga kupisha ujenzi wa bomba la mafuta la TAZAMA.

“Mheshimiwa Rais, mimi nimekuja mwenyewe. Baada ya kusikia Mama Mkuu wa Watawa wa Mt. Agnes Chipole wanataka kuja kukuona na kukushukuru na mimi nikaona nije kwa nia ya kukushukuru, kwa niaba ya Kanisa katika Jimbo la Songea na pia kwa niaba ya Kanisa katika Jimbo la Ukonga, ambako pia tunaendesha shughuli zetu,” alisema Askofu Mkuu Mtega.

Alisisitiza Askofu Mkuu Mtega: “Aidha, napenda kushukuru na kupongeza ushirikiano mzuri kati wa wananchi wa Ukonga na shule yetu ile ya chekechea na pia kupongeza kazi nzuri inayofanywa na Mbunge wa Ukonga, Mhe. Makongoro Mahanga.” Mbunge huyo aliandamana na ujumbe huo kwa ajili ya mkutano huo na Rais Kikwete.

Wakati wa mkutano huo, Rais Kikwete pia alionyeshwa michoro ya ujenzi wa shule za msingi, sekondari, zahanati na nyumba za masista katika eneo hilo la ekari 16. Ujenzi huo uliopangwa kuanza mwakani, umekadiriwa kugharimu shilingi bilioni nne utakapokamilika.

Naye Rais Kikwete alimweleza Askofu Mkuu Mtenga na ujumbe wake kuwa alikuwa amefurahi kusikia kuwa Jeshi la Wananchi lilikuwa limekubali kutoa eneo hilo na kuwa tayari hati miliki ya kiwanja hicho, Ploti Nambari 351, imetolewa kwa Watawa wa Benedictine wa Mt. Agnes Chipole.

“Nawashukuru sana kwa kuja. Sote tulishukuru Jeshi kwa kusaidia kupata eneo hili. Nafurahi pia kusikia kuwa mmefikia hatua hii, mipango yenu ni mikubwa kweli kweli…mimi kama mlezi tutaendelea kusaidiana kwa chochote…mipango yenu mikubwa lakini hakuna kubwa lisilowezekana.”
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom